Msaada jamani kwa wanaotumia gesi.

KIBURUDISHO

JF-Expert Member
Mar 28, 2011
1,002
274
Wanajf wenzangu mambo vp? Naombeni kuuliza kwa wenye uzoefu wa kutumia nishati ya gesi kwa matumizi ya nyumbani kwa kupikia.Mahitaji yangu ni familia ya watu watatu mimi waifu bintinti wa kazi na mtoto.Naomba mchanganuo wa matumizi kama ifuatavyo:
Mtungi wa kg30 unatumika kwa muda gani?
..................... kg20..................................................?
......................kg15..................................................?
Tafadhali sana naombeni msaada wenu.
 
Yako mambo mengi hujafafanua vizuri kwa mfano familia yako inakula mara ngapi kwa siku? Menu yenu ina milo aina ngapi( course ngapi)? chakula aina gani? Kwa mfano kupika maharage ni tofauti na kupika sausage. Pia inategemea unatumia pressure cooker au la. Lakini very generally speaking familia yako inaweza ikatumia mtungi wa kilo 15 kwa muda wa mwezi mmoja, yaani 54,000/-
 
Matumizi ya Gas yanategemea ni chakula gani unapikia.Kwa familia yako 30 kg inaweza kukutosha kwa mwezi kwa matumizi ya jiko tu la plate 1 au 2.
 
Family of 3, 15 kg inakaa 2 months kama unatumia pressure cooker kwa maharage na nyama. Otherwise mwezi na nusu inatoboa. Angalia urahisi wa kutumia, chakula hakinuki moshi, na ni haraka (ndani ya nusu saa unaweza pata mlo kamili)
 
Hivi kimahesabu zaidi kg1 ya gesi inatumika kupika kwa saa ngapi au dk ngapi?
 
Mitungi ya gas oryx ipo ya 38kg, 15kg, 12.5kg (sio mingi) na 6kg. Makampuni mengine madogo sijui.
Mtungi wa 15kg ndio wa matumizi ya familia. Kwa famili kama yako kama unatumia vizuri unakaa miezi miwili hivi
 
Back
Top Bottom