Msaada: Gari yangu inatoa Mlio tofauti wakati wa kurudi reverse

mzizi1

JF-Expert Member
Oct 9, 2017
255
692
Habarini wakuu,

Naomba msaada hapa, gari aina ya ractis pale nikiwa ninarudi reverse kuna sauti fulani kama ya kitu kinagongwa mara kwa mara au kama kinatetemeshwa hivi.

Nilienda kwa fundi kucheck akanambia yawezekana ni exozi iligongwa mahali, akarekebisha lakini naona hali bado ni ileile haijabadirika.

Nahofia kuzembea hili
 
Ulivyosema gari nikajuq LC au Nissan Patrol.. au Discovery etc.. kumbe ractis.. (chombo cha usafiri).

Haya nirudi ktk mada.

Ukiweka gear ya reverse inashtuka? Na mlio unaosemea ni wakati inarudi au wakati ume engage gear ya reverse?
 
Duh!
 
Wakati nimeweka reverse mkuu, napiah sikujua ractis kama sio gari
 
Masega yapo kabisa salama mkuu
Au giabox ndo inagonga

Check Kama Hakuna leakage ya gia box fluid uko chini.

Iliwahi nikuta Kama hiyo nmeenda Chaka sehem flan.

Kumbe bati la chini likaachia nikalingoa kabisa kua ntalifungia mjini sahv linanipigia tu makelele.

Njiani nmezoa kijiti kimeng'oa pipe ya giabox na fluid kuanza kumwagika chini Bila Mimi kujua.

Kuna sehem nmepaki, wkt wa kuondoka napiga reverse, nikaskia mtetemo Kama chuma kinagonga chini nikapuuzia.

Nlkuja kustuka nmefk lami tena mlimani gari imeishiwa Nguvu, ule mlima sikuumaliza gar ikaanza kurud nyuma.

Nmeipaki sehem salama, nacheck chini matone ya brake fluid haya Hapa.

Nmemuita fundi, nikajikuta nmeikaanga na inanighalimu kununua giabox mpya
 
Back
Top Bottom