Mrope(Mb): "Hatuwezi kuokota Mawaziri mitaani, wawe Wabunge"

Bwana Mrope pia amewaponda wote wanaotumia mifano ya nchi nyingine duniani kujenga hoja yao. "Hao wanatumia mfano wa Marekani, hao Marekani wenzetu wameendelea, wana makompyuta kibao". Bwana Mrope alisisiza hoja yake huku akipigiwa makofi na wabunge walio wengi. Mheshimiwa Mrope aliyasema hayo wakati akichangia muswada wa uendeshaji wa Bunge unaojadiliwa hii leo.
----------------
Hivi ni kitu gani kilichowafanya watu wazima hawa kushangilia na kumpigia makofi Bwana Mrope.

Swali zuri sana na jibu lake pia ni rahusi sana.

(a) Wabunge wengi hugonbea wakiwa na matumaini ya siku moja kuukwaa uwaziri; kwa hiyo wazo la kuondoa utaratibu wa wabunge kuwa mawaziri liko kinyume na utashi wao wa ubunge.

(b) Maneno ya Mrope yanaonyesha kuwa Wabunge wana thamani kubwa, yaani siyo wa kuokota mitaani. Kama wewe ungekuwa mbunge ungejisikiaje katika mazingira hayo kama siyo kuunga mkono tamko hilo?
 
Mrope ni kafisadi ambako hakakupata nafasi, namkumbuka alivyokuwa mahiri wa kuchukua samani za serikali ndani ya nyumba kila alipopata uhamisho, namkumbuka alivyotetea kampuni feki za India zisizokuwa hata na ofisi achilia mbali kiwanda cha dawa mpaka akalazimisha kumtoa mkemia pale wizara ya Afya na kumrudisha kufundisha Muhimbili kwa vile tu alifichua uozo wa Mrope,na hapo ndipo wakurugenzi pale wizara ya afya wakatishia kugoma kufanya naye kazi baada ya kwenda kumuona Godfather wake BWM na kumueleza alivyokiuka kutenda haki kwa mkemia kwa manufaa yake, Mrope ninayemjua ana haki ya kutoa lugha hiyo kwani hapo alipo anaota Uwaziri ila siku hizi afya yake inatia wasiwasi sijui kama ataupata
 
EMPLOYMENT HISTORY
Company Name Position From Date To Date
Ministry of Health Permanent Secretary 1995 1998
TAMISEMI - Dar es Salaam Region Regional Development Director(RDD) 1994 1995
Chunya District District Development Director(DDD) 1992 1994
Ministry of Foreign Affairs - Holland Deputy Ambassador of Tanzania in Holland 1985 1991
Ministry of Natural Resources & Tourism - TAFICO Chairman and Managing Director 1978 1984
Prime Minister's Office - Lindi Region Regional Development Director(RDD) 1975 1977
Prime Minister's Office - Dodoma Region District Development Director(DDD) 1972 1975
Ministry of Natural Resources & Tourism Fisheries Officer 1968 1971
Haya ni matatizo tuliyonayo katika Tanzania pengine na Afrika nzima ,ingawa uzoefu ni jambo zuri lakini haina maana atumike mtu mmoja kusafirishwa kila cheo akimaliza hiki anapewa kingine ,yaani lijitu linazeeka huku likiwa limepewa nafaasi kibao za uongozi wa juu ,ndio yule mtoto aliohoji mbona viongozi wanarundikiwa nafasi tele za kazi ? Wakatri wanaomaliza kusoma na kusomea wanasota na shahada zao ambazo ni za kisasa ? Nurura auliwe !!

Kwa Tanzania kama ulivyo uraisi kutumikia ni miaka kumi hata ukiwa uongozi wako ni mzuri vipi unatakiwa uwe ndio mwisho wa utumishi wako katika ngazi za Serikali kazi ambayo itakukabili baada ya kumaliza kipindi chako ni kupokea pensheni.
sasa na hawa mambalozi labda tuseme baada ya miaka kumi au kumi na tano wawe wamemaliza kipindi chao cha kukaa kikazi serikalini hivyo hivyo kwa mawaziri ambao wanaweza kupewa miaka kumi mpaka ishirini na wao wawe wamemaliza kazi serikalini hivyo hivyo kwa nafasi za juu na za mwisho katika serikali.

Ni tatizo kuwa na Waziri tokea tupate Uhuru badu yeye ni waziri mpaka anaingia kaburini ,au anakuwa anapata kibarua cha kuhamishwa hamishwa katika ngazi za ukubwa ,sheri kama hizi zikifikiriwa na kupitishwa basi hawa mafisadi wachanga wataanza kujirekebisha na kuanzisha biashara zao na mapema badala ya kutegemea ajira za serikali ambazo wanaweka matumaini ya kuchota.
 
Nadhani kuna la kujifunza hapa na lazima tujenge hoja hapa bila kumjenga mtu au kumbomoa....tujenge hoja ya kuhusiana na ubora wa kuwa na mawaziri ambao sio wabunge. Mie nadhani ni hoja ya msingi kuwa na mawaziri ambao sio wabunge,kwanza itasaidia kuwafanya wasiwe na tabia ya kupendelea maeneo yao na pia wananchi ambao wanapata mawazo kwamba iwapo wana mbunge ambae ni waziri wa ujenzi basi wana paswa kupewa kipaumbele cha barabara za lami na iwapo mbunge huyo hatashindwa kuleta kitu cha upendeleo kwake basi hio ni sababu tosha ya kutoshaguliwa tena.....aidha wabunge wengi wana kuwa na matumaini ya kuwa mawaziri kwa kutoa rushwa kubwa ili wawe wabunge na baadae kupewa uwaziri,jambo ambalo mim i naamini kuwa pale yatakapotenganishwa ata nguvu za kugombea ubunge na matumizi makubwa ya rushwa yatapungua sana.
 
Last edited:
Na siku watakayo pitisha sheria kuwa wabunge wasiwe mawaziri kutakuwa kweupeee bungeni, akina mwenzangu mie tutakuwa na nafasi ya kuukwaa uheshimiwa maana hayo ma PhD yote yatakimbia huko
 
Kilichonichosha zaidi ni sababu aliyoisema kuhusiana na nchi nyingine akiitaja Marekani kuwa wao Wameendelea na wana Makomputa mengi...

Duh, sasa sijui sisi na umaskini wetu hao wabunge wetu huchaguliwa kwa sababu wao ndio kidogo wameendelea na wana hizo komputa!...
Hata haingii akilini ndio maana nasema kila siku tunajua sana kupinga kitu lakini sababu zenyewe huwa ni vichekesho vitupu...
 
Nadhani kuna la kujifunza hapa na lazima tujenge hoja hapa bila kumjenga mtu au kumbomoa....tujenge hoja ya kuhusiana na ubora wa kuwa na mawaziri ambao sio wabunge. Mie nadhani ni hoja ya msingi kuwa na mawaziri ambao sio wabunge,kwanza itasaidia kuwafanya wasiwe na tabia ya kupendelea maeneo yao na pia wananchi ambao wanapata mawazo kwamba iwapo wana mbunge ambae ni waziri wa ujenzi basi wana paswa kupewa kipaumbele cha barabara za lami na iwapo mbunge huyo hatashindwa kuleta kitu cha upendeleo kwake basi hio ni sababu tosha ya kutoshaguliwa tena.....aidha wabunge wengi wana kuwa na matumaini ya kuwa mawaziri kwa kutoa rushwa kubwa ili wawe wabunge na baadae kupewa uwaziri,jambo ambalo mim i naamini kuwa pale yatakapotenganishwa ata nguvu za kugombea ubunge na matumizi makubwa ya rushwa yatapungua sana.

.....In addition...........wakati wa kampeni.....wengine hutumia kigezo cha kufahamiana na Rais Mtarajiwa....na hivyo eti "atakuwa Waziri"...........nasema hii ni HATARI sana........kwa sababu ikitokea huyo mtu akawa Waziri.........na ili aweze ku-maintain yeye kuchaguliwa tena kuwa mbunge na hatimaye uwaziri........kuna uwezekano mkubwa wa kupendelea Jimbo lake na vile vile kutumia RUSHWA kuwalaghai wananchi ili arejee madarakani.

Tatizo jingine ni hii tabia ya Marais wetu kufanya Re-cycling.....let me quote Al Gore...."I like recycling, but this is RIDICULOUS"........Yes.....hii tabia ya ku-recycle viongozi iangaliwe kwa undani.........recycling ifanyike ili kuondoa tatizo na si kuendeleza tatizo

Mwisho napenda kuuliza swali kwa wana JF & Policy Makers Dr. Slaa, Zitto et tal

KUNA ATHARI GANI MTU AKITEULIWA KUWA WAZIRI NA WAKATI SI M-BUNGE Vs SYSTEM/UTARATIBU TULIONAO SASA?
 
Nadhani kuna la kujifunza hapa na lazima tujenge hoja hapa bila kumjenga mtu au kumbomoa....tujenge hoja ya kuhusiana na ubora wa kuwa na mawaziri ambao sio wabunge. Mie nadhani ni hoja ya msingi kuwa na mawaziri ambao sio wabunge,kwanza itasaidia kuwafanya wasiwe na tabia ya kupendelea maeneo yao na pia wananchi ambao wanapata mawazo kwamba iwapo wana mbunge ambae ni waziri wa ujenzi basi wana paswa kupewa kipaumbele cha barabara za lami na iwapo mbunge huyo hatashindwa kuleta kitu cha upendeleo kwake basi hio ni sababu tosha ya kutoshaguliwa tena.....aidha wabunge wengi wana kuwa na matumaini ya kuwa mawaziri kwa kutoa rushwa kubwa ili wawe wabunge na baadae kupewa uwaziri,jambo ambalo mim i naamini kuwa pale yatakapotenganishwa ata nguvu za kugombea ubunge na matumizi makubwa ya rushwa yatapungua sana.

NCHIMBI,J
Napenda kukupongeza kwa mchango wako ulioutoa hapo juu. Hadi ninafikia hiyo posting yako kwa kweli nilikuwa nimepata mfadhaiko mkubwa sana kutoka kwa wachangiaji wote waliokutangulia isipokuwa Gembe. Hoja iliyotolewa na Mh. Mrope ni muhimu sana na sisi hapa JF tulikuwa na wakati mzuri wa kuichangia hoja na kuelimisha umma ni kwanini wabunge wasiwe mawaziri. Lakini badala yake wachangiaji waliokutangulia wameingia katika mtego wa kumjadili Mrope yeye binafsi na kuacha hoja ya msingi.
Sasa ninachotaka kusema hapa ni kuwa kwa mwendo huu hapa JF itakuwa ni kama kijiwe cha kahawa, siku ikiisha na hoja imepotea. Ninashauri tutumie nafasi hii kuelimisha umma kwa kujadili hoja ya msingi na wala siyo Mrope. Mrope ni mwanasiasa kesho anaweza kuja na jingine litakalowafurahisha nafsi zenu, sijui mtasema nini?
 
Back
Top Bottom