Mrema awaonya matajiri Vunjo

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,483
15,308
MBUNGE wa Vunjo mkoani Kilimanjaro, Augustino Mrema ameonya tabia ya baadhi ya matajiri kuwahonga baadhi ya watendaji wa vijiji na kata ili wasishiriki katika kazi za kujitolea hususan miradi ya maji katika Mji Mdogo wa Himo.

Mrema ameyasema hayo wakati wa ziara yake katika jimbo hilo iliyolenga kusikiliza kero za wananchi, lakini pia kuwashukuru kwa kumpa nafasi ya kuwaongoza kwa kipindi cha miaka mitano.

Amesema, kwa sasa jimbo hilo lipo katika mchakato wa utekelezaji wa mradi wa maji katika eneo la Himo utakaogharimu zaidi ya Sh milioni 500 ambapo Rais Jakaya Kikwete aliahidi kuchangia Sh milioni 150.

Mwanasiasa huyo amesema, pamoja na utekelezaji wa mradi huo, lakini bado kuna baadhi ya matajiri ambao hutoa rushwa kwa viongozi hao ili wasishiriki katika uchimbaji wa mitaro ya kupitisha mabomba ya maji.

“Hawa matajiri wanatumia fedha ili wasichimbe mitaro ya maji na fedha hizo viongozi hawa wanazitumia kwa ajili ya unywaji wa gongo na mambo mengine yasiyo na msingi, sasa naagiza mchezo huo uachwe mara Moja,” amesema Mrema.

Aidha, Mbunge huyo amesema, wananchi hao wameonesha imani kubwa kwake hivyo atatumia nafasi hiyo katika kutatua kero zao.

“Wapo baadhi ya watu nimeambiwa hawataki kutoka kujumuika na wenzao kwenye shughuli za kujitolea, lakini pia hawataki kutoa faini iliyopangwa badala yake wamekuwa wakiwahonga watendaji ili wasiulizwe, acheni la sivyo nitawaaibisha,” alisema.

Amesema, ni vyema watendaji hao kama wamekuwa wakipokea faini, waoneshe vitabu vya stakabadhi, lakini pia kuwasomea wananchi mapato na matumizi ya fedha hizo.

Habarileo
 
Huyu mzee na gongo sijui ana matatizo gani, tangu enzi za uwaziri yeye na gongo tu! Inawezekana ni mbaya ila asiifanye kuwa wimbo wake
 
Back
Top Bottom