Mrejesho wa mama Neema. Je, nichukue milioni tano au niache?

GRAMAA

JF-Expert Member
Nov 1, 2014
1,155
3,402
Jana nilisalitiwa na mke wangu mama neema. Tulikwenda kumfumania nikiwa nipo na wazazi wake na baadhi ya ndugu zangu.
Tulipo fika huko kweli tulimkuta mke wangu yupo na yule jamaa wa TANESCO. Aisee inauma sana usiombe ikukute.
Nilitaka kuleta fujo ila wazee walifanikiwa kunituliza na kuniambia nijikaze.
Mwisho wa siku yule jamaa akaomba msamaha sana nakuahidi siku ya tarehe 13 atatoa
milioni tano kama fidia na faini.

Kweli mke wangu atembee na mwanaume mwingine mi nipewe milioni tano? Inaniuma sana tena sana. milioni tano inapoza nini kwa mke jamani.
Wanawake wanawake wanawake ni adui wakubwa sana duniani jamani kuweni makini haya mambo yanauma sana usiombe
 
chukua mpunga huo ila ujiandae kwa swali kutoka kwa mama ney hela zikiisha nafikiri unajua atakuuliza nini!!!!
 
Usichukue hiyo hela ni machukizo kwa Bwana. Maandiko yanasema na hapa nitanukuu Mtu asimuache mkewe ISIPOKUWA KWA UZINZI. Tekeleza maandiko, Amen
 
Kimsingi agano la kale linaruhusu talaka based on sababu yoyote ile. Agano jipya linakataza talaka isipokuwa kwa uzinzi au uasherati.
 
Kila siku me humu mnaadvertise michepuko sasa ke wakichepuka ndio mnawaona wabaya. Ngachoka mie lol
 
funguo inayofungua kufuli nyingi inaitwa MASTER KEY..lakini kufuli inayofunguliwa na funguo nyingi ni USELESS
 
Usikubali hiyo pesa utajishushia heshima yako kama mwanaume au mume

Kumkuna ameshamkuna na labda watazidi kuendelea kwa siri

Dawa ya huyo ni kumletea mke wa pili au ajue unamchepuko

Usipokee hiyo pesa utachekwa na kuumia roho zaidi na hata huyo mke wako atazidi kukudharau hakuna cha pesa wakati mke ametoa K yake kw mwanaume, je wewe kweli ni maskini hivyo? Au hiyo pesa utaifanyia nini zaidi ya kuendelea kumtunzia mchepuko wake sijui mpenzi wake ambaye ni mke wako.

Siku nyingine ita watu wa familia yako pia, sio watu wa upande wake tu ni kama haukuwaita.

Ila usipokee hizo pesa kabisa amekudharau kwa kusema atakulipa.

Mkeo inabidi umuonyeshe wewe ni mwanaume na ukampime tena na wewe ipime kwa mwaka mmoja ujao. Mkeo ataendelea na tabia hiyo na labda ana wengine husiowajua wanamdu

Ukienda nje kale na mpira.
 
Jana nilisalitiwa na mke wangu mama neema. Tulikwenda kumfumania nikiwa nipo na wazazi wake na baadhi ya ndugu zangu.
Tulipo fika huko kweli tulimkuta mke wangu yupo na yule jamaa wa TANESCO. Aisee inauma sana usiombe ikukute.
Nilitaka kuleta fujo ila wazee walifanikiwa kunituliza na kuniambia nijikaze.
Mwisho wa siku yule jamaa akaomba msamaha sana nakuahidi siku ya tarehe 13 atatoa
milioni tano kama fidia na faini.

Kweli mke wangu atembee na mwanaume mwingine mi nipewe milioni tano? Inaniuma sana tena sana. milioni tano inapoza nini kwa mke jamani.
Wanawake wanawake wanawake ni adui wakubwa sana duniani jamani kuweni makini haya mambo yanauma sana usiombe

Lakini, ulikusanya ushahidi kwa madhumuni gani?
 
Usiache pesa wewee kwani usipochukua ndio atakuwa hajagegedwa piga pesa endelea na maisha usiache jamaa akala bure aiseee
 
Ni upumbafu ulioje kuiacha hela. Chukua hela na kisha toa talaka
 
Nina wasiwasi na serikali ya kichwa chako. Pole, nahisi mama neema amekushika masikio hadi kojoleo hukohoi wala hufurukuti.

Siku nyingine akichepuka usilete uzi hapa maana unatudhalilisha wanaume wote.
 
Back
Top Bottom