Mrejesho mtaji wa laki 3: Nimeamua kuuza biashara ya matunda na genge

masanjuo

Senior Member
Oct 10, 2016
184
306
Habari Za uzima Wana jamii wenzangu,

Mimi ni Yule mdada nilieleta wazo langu kuhusu biashara Kwa mtaji mdogo WA laki tatu Tu. Nashukuru nmepata mawazo mazuri nmefatilia Kwa utulivu na nimesoma maoni ya kila mtu. Maoni yangu Nimeamua sasa kuuza biashara ya Matunda Na genge mpaka sasa nmefatilia process ya kupata eneo nmepata.

Sasa nafatilia utengenezaji wa Banda la kawaida tu ambalo naomba Mungu lisimalize laki moja Na mtaji wangu nataka ubaki Kama laki moja Tu hiyo ndo nitaanza nayo, matengenezo mengine nitatengeneza Kadri Mungu atavyonijalia.

Asante sana mmenifungua mawazo nilikuwa Nawaza Sana kitu cha kufanya, kila nikiwaza nashindwa kutokana mtaji kuwa Ni changamoto.

NB: Tuweni Makini humu ndani sio wote wema wakati nipo kwenye mchakato alitokea mtu huku DM akaahidi kunipa kazi nilifurahi Sana kazi yenyewe ni ya sheli Na akadai IPO Arusha. Kama kawaida mimi nilimsikiliza akaniunganisha Na meneja feki ili wanitapeli hela.

Ni story ndefu siwezi kueleza lakini mwisho wa siku huyu boss akaomba hela ya uniform kama sh laki 1 na elfu 30. Dah Mungu Yuko upande wangu sikufanikiwa kutuma, nadhani ningetuma leo ningekuwa Na majonzi mapya.

My take: Mtu kaomba ushauri afanye nini ili ajikomboe na Maisha Na utegemezi sasa usiwe Tena chanzo cha kumrudisha nyuma huyu mtu.

Asanteni na nawatakia siku njema

Pia, soma=>Nimetafuta kazi nimechoka, naweza kufanya biashara gani na laki tatu?
 
Kwa kuwa umeamua kusaidia ili kukomesha kwa wengine na angalau na yeye apate anachostahili itakuwa vyema Sana ukimtaja.

Ushauri wangu, unaona aibu au vibaya kumtaja wakati yeye hakuona vibaya kukuumiza!

Mtaje tafadhali tutakulinda
 
Habari Za uzima Wana jamii wenzangu Mimi ni Yule mdada nilieleta wazo langu kuhusu biashara Kwa mtaji mdogo WA laki tatu Tu..mashukuru nmepata mawazo mazuri nmefatilia Kwa utulivu nanimesoma maoni ya kila mtu ..maoni yangu Ni nmeamua sasa kuuza biashara ya Matunda Na genge mpaka sasa nmefatilia process ya kupata eneo nmepata sasa nafatilia utengenezaji wa Banda la kawaida Tu ambalo naomb Mungu lisimalize laki moja Na mtaji wangu Nataka ubaki Kama laki moja Tu iyo ndo nitaanza nayo matengenezo mengin ntatengeneza Kadri Mungu atavyonijalia Asante San mmenifungua mawazo nilikuwa Nawaz Sana ...kitu chakufanya kila nikiwaza nashindwa kutoka Na mtaji kuwa Ni changamoto.. NB tuweni Makini umu ndani sio wote wema wakati nipo kwenye mchakato alitokea mtu uku DM akahaidi kunipa kazi nilifurahi Sana kazi yenyew Ni ya sheli Na akadai IPO arusha Kama kawaida mimi nilimsikiliza ..akaniunganisha Na meneja feki ILi wanitapeli ela Ni story ndefu siwez kueleza Lakin mwisho wa siku uyu boss akaomb ela ya uniform Kama sh laki 1 Na elf 30 ..mwenyew avater ya wiztech umu ndani Dah Mungu Yuko upande wangu sikufanikiwa kutuma nadhani ningetuma Leo ningekuwa Na majonzi mapya ...my take ..mtu kaomba ushauri afanye nini ILi ajikomboe Na Maisha Na utegemezi sasa usiwe Tena chanzo cha kumrudisha nyuma uyu mtu Asanteni Na nawatakia siku njema
 
Back
Top Bottom