Mramba na Yona kutumikia kifungo cha nje. Kufanya usafi hospitali ya Palestina, Sinza

Ama kweli tajiri tajiri tu ,mwizi maskini anakamatwa anapigwa kiberiti ila Tajiri anafungwa miezi 6 utaratibu wa Parole unafanyika ,waungwana huku wanasema ni kuwadhalilisha ,hii dunia sio fair ,mwanangu tafuta hela tu kwa nguvu zote
 
Mawaziri wa zamani wakati wa awamu ya Tatu, Basil Mramba (Waziri wa Fedha) na Daniel Yona (Nishati na Madini) sasa kutumikia kifungo cha nje hadi Nov. 5 kwa kufanya usafi wa mazingira katika Hospitali ya Palestina Iliyopo Sinza.

Ikumbukwe Julai 6, 2015 mawaziri hao walihukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela na kulipa faini ya milioni tano kila mmoja kwa kosa la matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara.
Ngoja nikatupe takataka pale hospitali ya Palestina,ili ''mla nyasi''apate kazi ya kufanya
 
Kuna mwanajamii mmoja alishawahi kulisema hili kabla lakini simkumbuki jina..ila ndio utawala wetu huo kutupoteza maboya..
 
Mawaziri wa zamani wakati wa awamu ya Tatu, Basil Mramba (Waziri wa Fedha) na Daniel Yona (Nishati na Madini) sasa kutumikia kifungo cha nje hadi Nov. 5 kwa kufanya usafi wa mazingira katika Hospitali ya Palestina Iliyopo Sinza.

Ikumbukwe Julai 6, 2015 mawaziri hao walihukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela na kulipa faini ya milioni tano kila mmoja kwa kosa la matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara.
Hii serikali ya ccm hatujui inatupeleka wapi, wakati vibaka walio iba kuku wanatumikia miaka 10 jera mijizi kama mramba wanaachiwa? Mungu ibariki tanzania
 
zilikua mbwembwe kuonesha mapambano dhidi ya ufisadi, uchaguzi umeisha inabid waachiwe. Sasa kwa hukumu hizi yanini kuingia gharama kuanzisha mahakama za mafisadi?
ukiingizia nchi hasara kubwa hivi unahukumiwa kufagia? Kunaseremala walikutwa na mbao walipigwa mvua ya kutosha.Kwa staili hii hamna mahali tutafika,madili feki yatazidi
 
Kipi bora

Kipi bora wakae jela wale bure au watumiwe ktk kufanya usafi na wale majumbani kwao. Wafungwa wanakula kwa kodi zetu. Tuombe tu na wengine waachiwe wafanye usafi kupunguza msongamano na kula bure jela
 
Fauu inaonesha kwako swala la kula unalipa uzito sana! Wanakula nini chazaidi mpaka iwe gharama Ivo? Wakifungwa hawawezi kupewa kazi mbalimbali za kufanya ikiwemo kufagia?
unapaswa kujua binadamu wote ni sawa,haipaswi kuhukumu watu kwa kutizama sura zao badala ya vifungu vya sheria
 
MoneyBag....mbona zile za ........hakuna aliyefungwa na bado wanapeta.....Itoshe wewe kukubali hakuna hakimu kama ALLAH hata vitabu vitakatifu vinasema hivyo.
Sasa bantu zile tunasubiria watuhumiwa wafikishwe mahakamani ndio maana hata president anataka mahakama ya majizi zifunguliwe mpm tuwafikishe kortin
 
na hospitali palivyo pachafu pale sinza,nawaonea huruma hawa wazee
Really! Watanzania ni wapumbavu, hawa wandugu walifungiwa hotelini sasa wametolewa wanarudishwa kwenye public eti watanzania wanashangilia.
Nakuomba ujionee huruma mwenyewe uliepumbazwa!
 
Really! Watanzania ni wapumbavu, hawa wandugu walifungiwa hotelini sasa wametolewa wanarudishwa kwenye public eti watanzania wanashangilia.
Nakuomba ujionee huruma mwenyewe uliepumbazwa!
ilitakiwa wawabakie huko huko jela mpaka kifungo kiishe,sipati picha mramba anakamata mopper pale anapiga deki
 
Je kulikuwa na kipengele cha kurudisha fedha walizoisababishia Serikali hasara? Kama ndiyo warudishe hizo fedha watakapomaliza kifungo chao. Na kama sivyo kurugenzi ya mashtaka na Mahakams ziseme kwa nini hakipo wakati iliwatia hatiani
 
Back
Top Bottom