Mramba na Yona kutumikia kifungo cha nje. Kufanya usafi hospitali ya Palestina, Sinza

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeridhia waliokuwa Mawaziri wastaafu Basil Mramba na Daniel Yona kutumikia adhabu ya kifungo cha nje kwa kufanya usafi katika maeneo ya kijamii ikiwemo Hospitali ya Sinza Palestina.
Hatua hiyo inatokana na Mramba ambaye alikuwa Waziri wa Fedha na Yona aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, kupitia Mawakili wao kuwasilisha barua mahakamani hapo kutoka Magereza kuhusu kutumikia kifungo cha nje.
Mawaziri hao wa zamani waliwasilisha barua hiyo ya kuitaarifu mahakama yenye kumbukumbu namba 151/DA/3/11/223 ya Desemba 5, mwaka jana, wakiongozwa na jopo la mawakili wao watatu Peter Swai, Cuthbert Nyange na Elisa Msuya.
Katika barua hiyo waliyoiwasilisha kwa Hakimu Mkazi Mfawidhi Cyprian Mkeha ilikuwa na kichwa cha habari kisemacho‘Wafungwa wenye sifa ya kutumikia vifungo vyao chini ya Mpango wa Huduma kwa Jamii”.
Hakimu Mkeha alisema mchakato huo ulianza baada ya Magereza kuwasilisha barua hiyo mahakamani hapo kwa kupeleka majina ya watu wanaotumikia kifungo cha nje ikiwemo mawaziri hao.
Alisema mahakama haihusiani na mchakato huo, kwani ilishamaliza kazi yake ya kuhumu, hivyo jukumu la kutumikia kifungo cha nje ni kazi ya Magereza.
“Baada ya kuleta barua hiyo kisheria mahakama inaishinikiza Ustawi wa Jamii ili ifanye uchunguzi kutokana na majina yaliyowasilishwa mahakamani,”alisema.
Hakimu Mkeha alisema kupitia barua hiyo, Mawaziri hao wa zamani wamepangiwa kutumikia adhabu ya kufanya usafi kwenye Hospitali ya Sinza Palestina kwa saa nne za kila siku.
Alisema awali kabla ya mahakama kuridhia adhabu hiyo, iliwaita Mawaziri hao kwa ajili ya kuwahoji kama wameridhia na adhabu watakayopangiwa sambamba na vipengele vinavyowahusu.
“Kutokana na barua hiyo mahakama ikaona ni vyema kuwaita wahusika wenye ambapo tuliwahoji kama wanaridhia kutumikia adhabu hiyo, ambapo walikubali ndipo tukaridhia,”alisema.
Kuhusu masharti yaliyotumika kuwapatia kifungo hicho, alisema kinatokana na sheria ya Jamii namba 6 ya mwaka 2002, kifungu cha 3(1).
Alisema baadhi ya vigezo vinavyotumika kwa wafungwa kutumikia adhabu ya nje ni muangalio wa ripoti yao ilikuwa inasemaje, umri, washtakiwa kama walishawai kutiwa hatiani, makosa namna yalivyo, kama wanafamilia, pia kama wanakubali kuitumikia jamii, kama wana ajira, tabia za mshtakiwa na umbali wa eneo analokaa na anapofanyia adhabu hiyo.
Inakumbukwa kuwa Oktoba 2, 2015 katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ilitoa hukumu ya rufaa dhidi ya mawaziri wastaafu, Basil Mramba na Daniel Yona ambapo Jaji Projest Rugazia, alikubaliana na hoja kwamba kwa mujibu wa mashtaka yaliyowatia hatiani kwa matumizi mabaya ya Ofisi na kwa mujibu wa kifungo cha 35 cha adhabu PC ambacho Mahakama ilikitumia walipaswa kupewa adhabu ya kutumikia kifungo cha miaka miwili na si miaka mitatu.
Katika rufani hizo, Mramba na Yona, waliwasilisha hoja tano kupinga hukumu iliyotolewa Julai 6, mwaka jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, na jopo la Mahakimu watatu, likiongozwa na John Utamwa.
Aidha DPP alipinga adhabu waliyopewa mawaziri hao kwa madai ni ndogo, pia hakimu alikosea kumuachia huru aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Gray Mgonja na pia iliiomba mahakama iamuru washtakiwa walipe fidia ya fedha walizosababisha hasara.
Katika uamuzi huo Jaji Rugazia alikubali hoja ya kina Mramba kuwa walipewa adhabu mbili kwa kosa moja.
“Haikuwa sahihi kuwashitaki kwa kosa la kusababisha hasara wakati kosa hilo lilishakuwa kwenye makosa mengine ambayo ni la tano hadi la 10,” alisema.
Aidha, alisema Yona aliunganishwa kimakosa katika shtaka hilo, hivyo alifuta shitaka hilo pamoja na adhabu ya kifungo cha miaka mitatu jela na faini ya Sh milioni tano iliyotokana na kosa hilo.
“Ninaondoa shitaka la kusababisha hasara, ninafuta adhabu ya kifungo cha miaka mitatu jela na faini ya Sh milioni tano, hivyo Yona na Mramba watatumikia kifungo cha miaka miwili kwa kila kosa,“ alisema.
Katika uamuzi huo, Jaji Rugazia alisema, “Nakubali Kifungu cha 6 cha Kanuni ya Adhabu kinachotaka mahakama itoe amri washitakiwa walipe fidia, lakini siwezi kutoa amri hiyo.”
Pia alikataa hoja za kina Mramba kuwa hati ya mashtaka ni batili, pia alisema hakukuwa na njama zozote kwa upande wa Jamhuri kutoita mashahidi waliosaini mkataba huo ili kuathiri upatikanaji wa haki, kwa kuwa utetezi walikuwa na haki ya kuomba watu hao wawe mashahidi wao.
Alisema wasitumie maelezo ya aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, kuficha kosa kwa kuwa alitoa maelekezo kutokana na barua aliyoipata kutoka kwa Mramba na hakujua kama tayari Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) ilishatoa angalizo la kutokutoa msamaha huo.
Kwa upande wa Mgonja, Jaji Rugazia alisema anahalalisha kuachiwa kwake huru baada ya kutopatikana na hatia. Alisema, “Siwezi kuilaumu mahakama kwa kumuachia huru”.
Katika hukumu hiyo, mawaziri hao walihukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela na kulipa faini ya Sh milioni tano, baada ya kupatikana na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya Sh bilioni 11.7.
Kwa mara ya kwanza washtakiwa hao walifikishwa mahakamani mwaka 2008, wakikabiliwa na mashtaka ya kuisababishia serikali hasara ya kiasi hicho cha fedha kutokana na kutoa msamaha wa kodi kwa Kampuni ya kukagua madini ya dhahabu ya M/S Alex Stewart ya Uingereza.

.: WALIOITIA HARASA SERIKALI BILIONI 11,WATOKA GEREZANI,NI MRAMBA NA YONA,WAKAA MIEZI MINNE TU,SOMA HAPO KUJUA
Mpekuzi blog
 
adhabu za ki-tz noma
Hizi mbona zipo huko kwa walioendelea inaitwa community service hulipwi. Watu badala ya kupelekwa gerezani wapoteze pesa kukulipa wanakuacha ukae nyumbani ujilishe ila ufanye kazi bure. Naomi Campbell alifalishwa magwanda na kufagia bararani ilimuumiza sana
 
Binafs nna mawazo tofaut,hukumu hii ya kifungo cha nje ni kama kumshka sharubu JPM,na hapa ndo inaonesha kuwa nchi hii nchi hii hakuna nia ya dhat ya kupambana na ufisaf hata kidogo.Hawa jamaa hawajamaliza mwaka jela,na wataanza kuonekana uraiani hivi karibuni,bado kuna mashaka ya kupambana na ufisad pesa waliyokwiba ni nyingi haiendan na kifungo walichopewa,tena huko ndan wamenusa tu.Hii inanipa picha ndo zitakuwa hukumu za MAHAKAMA YA MAFISADI
 
Mkapa alimfunga Nalaila Kiula Waziri wa Mzee Mwinyi kwa Rushwa, Jakaya kawafunga Yona na Mramba na still mahusiano kati ya Rais mtangulizi wake hayakuathirika Nasubiria kuona wakifungwa at least Mawaziri watatu ili twende na speed. Alianza mmoja then wawili sasa iwe watatu
Sasa huyo Mramba na Yona nao utasema walifungwa kweli wewe kwa hasara ile?
 
Kipi bora

Kipi bora wakae jela wale bure au watumiwe ktk kufanya usafi na wale majumbani kwao. Wafungwa wanakula kwa kodi zetu. Tuombe tu na wengine waachiwe wafanye usafi kupunguza msongamano na kula bure jela
Wangapi wanaokaa jela na kula bure?hao wazee walipaswa kupelekwa magereza ya Kilimo like Mtego wa Simba,Mbigiri au Kiberege huko Morogoro wawe wanalima,hasara walioisababisha ni kubwa sana mdau haiendan na kifungo haiendan na hicho wanachokifanya au watakachokifanya Sinza.Kama umesahau nakukumbusha,they stolen 11 bil
 
Hizi mbona zipo huko kwa walioendelea inaitwa community service hulipwi. Watu badala ya kupelekwa gerezani wapoteze pesa kukulipa wanakuacha ukae nyumbani ujilishe ila ufanye kazi bure. Naomi Campbell alifalishwa magwanda na kufagia bararani ilimuumiza sana
Mdau si kwa wizi wa bil 11 hata kama inauma walau adhabu ingekua miaka 10 na wametumikia miaka 8 so miwli wanakuja kuzibua mavu hapo Sinza,sasa Hawa walihukumiwa mitatu,wamekaa jela frm July 2015 now wanakuja uraian,
Mramba na Yona walipaswa kuwa magereza ya Kilimo huko Moro au Tanga wanazalisha chakula tu
 
Mbona hasara iliyotokea ni kubwa kuliko hiyo faini waliyotoa pamoja na kifungo hicho??
 
Hizi mbona zipo huko kwa wdepartment delea inaitwa community service hulipwi. Watu badala ya kupelekwa gerezani wapoteze pesa kukulipa wanakuacha ukae nyumbani ujilishe ila ufanye kazi bure. Naomi Campbell alifalishwa magwanda na kufagia bararani ilimuumiza sana


Hata hpa Tanzania hii adhab ya kifungo cha nje mbona ipo sn Community Service Department iko chin ya Wizara ya Mambo ya Ndani inahudumiwa na Social workers lkn wahusika wakuu ni Probation officers Uko Dunian hiz adhab zinajulikana sn kwasababu mara nying uwa wanapewaga Maceleb na kule wamejipanga wanavitendea kaz mf Uniform,vifaa vizur vya kufanyia etc.Huduma kwa jamii wako kwenye ofis zote za mahakama hp Tz na kaz yao kubwa ni kusikiliza kes za wafungwa,kuwafanyia uchunguz,home visit km mshtakiwa anatokea nyumban na km yuko gerezan inabid amfate gerezan.Wahusika rasm wa vifungo vya nje kwa mujib wa sheria ya Tz ni wale wafungwa walihukumiwa chini ya miaka mitatu na wenye kes ndogo ndogo,km kuiba kuku,wanaokamatwa uko mitaan wavuta bang,wanaogombana majumban kes za mtaan,na uwasilisha riport yao kwa hakim kabla ya hukumu na km mtu akihukumiwa chin ya miaka mitatu inabid apewe kifungu cha nje na alipe lile den.Mfn mzur ni, kes ya mtu ameibiwa boda boda/bajaj yake na dereva wake.Mshtakiwa,anaweza kufungwa kifungo cha nje uyo dereva cha mwaka mmoja na akaambiwa amlipe hela Mshtak mwenye boda boda,hii inasaidia kupunguza msongamano wa watu magerezan na pia inampa mda yule mshtakiwa kutafuta hela ya kulipa lile den.Den linatakiwa lilipwe ndan ya kifungo chake mf amehukumiwa mwaka 1 na thaman ya boda ilikua ni 1.5m Inabid alipe ndan ya uo mwaka.Mshtakiwa anapewa masaa manne tu ya kufanya kaz kwa siku,chini ya uangaliz wa afisa huduma kwa jamii(Social worker/social welfare/probation officer) mpk pale atakapomaliza kifungo chake,pia afisa huduma kwa jamii anakua na file lake lenye details zake zote siku atakayoanza kutumikia kifungo chake mpk atakapo maliza mshtakiwa kutumikia kifungo chake na iyo form inakua na yafuatayo.Tarehe,mda,kifungo chake,picha yake na sehem ya kusign unapofika na unapoondoka lzm usign ili wahakikishe kwel unatumikia adhabu yako,pia wadhamin wake wawil nje ya wale waliomdhamin mahakaman kwenye kes na lazima aripot kila siku jumataru mpk ijumaa kwa mda atakaopangiwa na afisa.Hawa wafungwa walioko kifungo cha nje ufanya kaz kwenye ofis zozote zile za serikal wapo weng sn sema tu kwa Tz huwez kuwagundua kwasababu hawana uniform.Ukienda mabibo kwenye yale mabwaya ya dawasco wako wanasafisha mabwawa,kawe hospital,palestina,magomen hospital,ofic za serikal za mitaa nk.na wanapangiwa placement kutokana na mahal anayoish.Pia mshtakiwa akishindwa kutumikia adhabu yake ya kifungo chake cha nje,adhab inabadilishwa na anarud tena gereza.Vilevile hp kunakuwa na wafungwa wa aina mbili direct from court hukum ikishatolewa na hakim aende kifungo cha nje na kuna wale wanaotoka gerezan. .
 
I hope na wafungwa wengine nao watapewa adhabu kali ya "kifungo cha nje". Usanii mtupu!

Halafu eti serikali hii inataka kuleta mahakama za mafisadi! Kama hukumu zenyewe ni kama hizi bora waache tu, kuliko kutuhadaa wananchi!

Serikali ya JPM imewapa vyeo watuhumiwa wa Escrow, na kabla hatujasahau inataka kuwatoa mafisadi jela kijanja eti wakafagie, Uliona wapi mtu aliyeitia hasara serikali mabilioni ya fedha anahukumiwa kufagia, hukumu ya aina hii ipo katika sheria gani na kifungu gani?

Naona wakubwa wakiendelea kulindana tu, usanii uleule unaendelea!

Mkuu binafsi nafikiri Jaji pamoja na wakuu wa magereza wanajaribu kutingisha kiberiti i.e waone current Administration ita react vipi, sioni any plausable reason ya sakata hili la kushangaza!

Juzi Dk.Magufuli alitoa kauli nzito kuhusu Mahakama zetu nchini, hivi inaingia akili kwamba kuna Jaji yeyote mwenye ujasiri wa kujaribu kuwapunguzia makali ya adhabu wahujumu uchumi, anawapa kifungo cha nje eti kwa kuheshimu mapendekezo /recommendation ya mkuu wa magereza, yaani wanapewa adhabu kama ya dereva aliye gonga traffic lights!!

Ukweli wa mambo hawa jamaa were supposed to serve their full term in a slamner bila msamaha, mbinu hizi za kutaka ku-water down adhabu yao kiujanja janja kita set a very bad precedence kwa Serikali iliyopo madarakani, kwani mwezi wa tisa ni mbali kwa nini wasibaki gerezani mpaka tarehe ya mwisho ya kutoka kifungoni? Wangapi wanaozea magerezani kwa kesi zenye kutia shaka!
 
Duh,maisha kweli hubadilika.Ya mungu mengi.Zamani ungewaambia hivyo kipindi wapo kwenye kiyoyozi cha wizara ya fedha pale,wangekuambia nenda kale nyasi!
Wewe utazidi kuwa masikini wa fikra. Hawa walihongwa mabilioni na kusababisha serikali ikose mabilioni na nchi ipoteze rasilimali ya dhahabu, eti unashangilia watakosa viyoyozi vya wizarani.
Mtanzania wa kawaida ataendelea kula mlo mmoja wakati hawa wandugu na jamaa zao wanaishi kama wapo peponi.
Inasikitisha kuona watanzania wanashangilia sarakasi za usanii!
 
Mdau si kwa wizi wa bil 11 hata kama inauma walau adhabu ingekua miaka 10 na wametumikia miaka 8 so miwli wanakuja kuzibua mavu hapo Sinza,sasa Hawa walihukumiwa mitatu,wamekaa jela frm July 2015 now wanakuja uraian,
Mramba na Yona walipaswa kuwa magereza ya Kilimo huko Moro au Tanga wanazalisha chakula tu
Kesi waliyohukumiwa haikua ya wizi bali kusababisha hasaara wakiwa ofisini na watumishi wa umma. Kuhusu kifungo si kosa lao hakimu anatoa hukuma ktk maeneo ya adhabu ya kosa lenyewe na vipi waendesha mashitaka walitaka hukumu iweje. Kama serikali haikukataa rufaa walikubaliana na adhabu. Usishangae ya kina yona oscar kaua na kakaa ndani miezi
 
Back
Top Bottom