Mradi wa Ufugaji wa ng'ombe

Mkuu sina uzoefu kwenye nyanja hii lakini jitahidi kuzingatia yafuatayo:
1. Hakikisha unayo maji ya uhakika - ama eneo liwe na mto au uchimbe kisima, itakusaidia sana.
2. Kuwa karibu na soko ili upunguze gharama za usafirishaji na utunzaji wa maziwa
3. Hakikisha unao wataalamu washauri ili iwe rahisi kukabili changamoto mbali mbali za ufugaji.
Vinginevyo nikutakie kila la heri mkuu na nakuombea ufanikiwe ili siku nyingine urudi hapa jamvini kutotobolea siri ya mafanikio.
 
Wakuu nawasalimu sana. Napenda kabla ya yote niappreciate michango yenu hasa katika forum hii, imekuwa ikinisaidia sana. Sasa turudi kwenye uzi huo hapo juu:
Naomba mwenye ushauri juu ya jambo hilo anisaidie please, nipo dar natamani kuanza mradi huo januari mwakani. Mpango ni kuwa na ng'ombe bora kama 10 hivi (wenye uwezo wa kutoa minimum of 10 liters/ng,ombe per day), shamba kwa ajili ya kufugia na kuotesha malisho ya mifugo hiyo (about 6 acres). Naomba ushauri kuhusu yafuatayo:

Mbegu bora ya ng'ombe wa maziwa

Eneo lililopo nje kidogo ya mji ambalo naweza kulitumia( kwa kulinunua)

Ushauri wa namna bora ya kufanya mradi huo.

Please kwa anaejua possible costs za eneo na ng'ombe wazuri nitashukuru.
Aina nzuri ya ng'ombe ni wale chotara wa kienyeji na kisasa ambao wanaweza kuhimili joto la Dar. Pia wa kisasa watazalisha kiasi hicho unachotaka endapo watapata matunzo mazuri.
 
Ng’ombe wanafugwa kwa ajili ya nyama na maziwa lakini pia hutoa mazao mengine kama ngozi, mbolea na hutumika kama wanyama kazi. Zaidi ya asilimia 95 ya ng’ombe hutumika kama wanyama kazi. Zaidi ya asilimia 95 ya ng’ombe wanaofugwa hapa nchini ni wa asili ambao huzalisha nyama na maziwa kwa kiwango kidogo ikilinganishwa na wale wachache walioboreshwa. Ng’ombe walioboreshwa wamegawanyika katika makundi mawili, wale wanaofugwa kwa ajili ya nyama na wanaofugwa kwa ajili ya maziwa. Ili kuwawezesha ng’ombe kuzalisha mazao bora ya nyama, maziwa na ngozi mfugaji anapaswa kufuata kanuni za ufugaji bora. Ili kujua kanuni hizo za ufugaji bora soma hapa SEKTA YA MIFUGO TANZANIA
 
Ndugu wasomaji, natafuta ng'ombe wa maziwa mwenye uwezo wa kutoa lita kuanzia 21 na zaidi kwa siku, awe wa uzao wa pili na na ana mimba ya 8months au zaidi. sema na bei. sihitaji dalali. Samahani kama kuna mtu anafahamu wapi naweza pata, naomba anisadie.

uliwapata au bado?
 
Kuna mwarusha mmoja anao ila anadai aliwatoa nje ya nchi sijajua ni wapi ila ni balaa kwa maziwa, anao mitamba ila sujui bei yake
 
hivi bei ya ng'ombe mwanamke mwenye umri wa mwaka na nusu hadi mitatu ni sh ngapi jamani?

Ungefafanua ingependeza, je wa maziwa, je wa nyama, au hawa wa kawaida? Au Chotara, hata wa kawaida wapo wale wenye pembe ndefu a.k.a ankole na hawa wa pembe fupi a.k.a zebu. Tuweke wazi tukusaidie.
 
Hebu waone RUVU JKT waweza kupata pale....

JKT nao wanafuga ng`ombe wa biashara?, ninachojua ni kwamba pale Ruvu ukivuka mto kama unakwenda Chalinze upande wa kulia kuna ranch ya serikali ya ng`ombe, labda kama una maanisha hivyo. Wale wa kule kambini ni mchanganyiko sio breed moja. Labda wameanza nao kufuga.
 
Habar JF Mimi ni fugaji mkoani Kilimanjaro,nina ng,ombe (4) wote ni jike,tatizo ni chakula chao kinapatikana kwa shida,ningependa kushiriki na wanajf ni namna gani naweza kuepuka shida ya lishe ya mifugo.ukizingatia sitaki kushindwa katika huu ufugaji maana tiyari nimewekeza ktk ufugaji.ni matumaini yangu kuwa mtanipa muongozo wa namnaya kumonitor hawa mifugo ili wasinishinde.
1)nipeni mbinu ya kuhifadhi chakula cha mifugo kwa usalama
2)Ni namna gani samahani ni nyasi aina gani zinazokua kwa haraka zaidi.ahsanten
 
Mkuu, tangu jana ninashindwa kuelewa na ninapata woga mkubwa wa huko tunakokwenda kwa mstakabali mzima wa mabadiliko ya hali ya hewa!
Ninavyofahamu chakula cha msingi cha ng'ombe, wa aina yoyote, ni nyasi/majani na maji safi na salama ya kunywa ya kutosha! Sasa, unapolalamika kuhusu chakula cha ng'ombe wanne (haijalishi jinsi yao) ukiwa Moshi, Kilimanjaro, sisi tulioko Bukundi, Meatu, Simiyu na Majirani zetu wa Kishapu, Shinyanga na huko Singida wafanyeje?
Moshi, Kilimanjaro, nnayoifahamu mimi au kuna Moshi nyingine? Hata hivyo nitarejea na "mchango" kidogo wa mawazo baada ya muda mfupi!
 
Habar JF Mimi ni fugaji mkoani Kilimanjaro,nina ng,ombe (4) wote ni jike,tatizo ni chakula chao kinapatikana kwa shida,
Pole sana inabidi uwe na plan B kwamba usipopata ya kununua uwe na eneo la kuotesha au ufuate mbali zaidi. Ufugaji au biashara yoyote ina changamoto zake, kuna msimu chakula kingi au bei rahisi utapata faida tunza ili kipindi cha kiangazi faida ndogo uweze kuikabili hiyo hali. Ukikata tama leo kesho unashangaa wenzio tatizo wamelipatia ufumbuzi. Jaribu kuwasiliana na wafugaji wenzio wapi wanapata majani hasa wale wadogowadogo ndo changamoto zinafanana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom