Mr Sugu na Mkoloni Wajiunga Rasmi na CHADEMA

Regia Mtema

R I P
Nov 21, 2009
2,970
864
Muda mfupi uliopita wanamuziki maarufu ndani na nje ya nchi Mr Sugu pamoja na Mkoloni wamejiunga rasmi na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA).

Wanamuziki hawa walikuwa wametangaza kujiunga kwa na CHADEMA leo kupitia vyombo mbalimbali vya habari katika Ofisi za Makao Makuu ya Chama hicho Kinondoni Dar es Salaam.

Kujiunga kwao kunafanya idadi ya wanamuziki mashuhuri kuongezeka katika kujiunga na chama hicho baada ya Nakaaya Sumari kujiunga hivi karibuni na kutangaza azma ya kugombea Ubunge.

j934ug.jpg

Habari ndio hiyo. Big Up!
 
ukijua wa mbele wenzio wajua wa nyuma................
 
nawapongezaa sana sugu na mkoloni kwa uamuzii huo makini...

kambii safii sana hiyoo hata kupambana na wale jamaa wa kudhulumuu wasanii(CEG)....
 
Nawapongeza, kupanga ni kuchagua!...Nakiamini chama hiki, kwahiyo mtu yeyote anaye-attempt kubadilika nampongeza!...Nampongeza sana Nakaaya kwa uamuzi huo pia, na yule ni model katika kizazi cha mabadiliko...Big-up to all who dream for changes!
 
Muda mfupi uliopita wanamuziki maarufu ndani na nje ya nchi Mr Sugu pamoja na Mkoloni wamejiunga rasmi na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA).

Wanamuziki hawa walikuwa wametangaza kujiunga kwa na CHADEMA leo kupitia vyombo mbalimbali vya habari katika Ofisi za Makao Makuu ya Chama hicho Kinondoni Dar es Salaam.

Kujiunga kwao kunafanya idadi ya wanamuziki mashuhuri kuongezeka katika kujiunga na chama hicho baada ya Nakaaya Sumari kujiunga hivi karibuni na kutangaza azma ya kugombea Ubunge.

Habari ndio hiyo. Big Up!

Bolded sijui kama hapa vyombo kama ITV TBC Clouds vitakuwepo mana hawa wote wanafiki wakubwa hawawezi kureport hii kitu

nawapongeza sana wewe wapiganaji wa ukweli sio kwenda kulala
 
Mwanakijiji, Anyisile, X paster, Compaq tunaomba mistari vijana wameshajiunga
 
Ni wakati wa mabadiliko ya kweli na uhuru wa kweli, maisha bora kwa kila mtanzania hayawezi kuletwa na mafisadi wale wale wa chama kile kile chenye uozo ule ule eti kwa ari, nguvu, kasi mpya.Tunawapongeza mr 2 na mkoloni kwa uamuzi huo wa kishujaa.
 
tanzania itajengwa na majasiri.big up you men.acha wanafuki waoga wa maisha waendelee kuvaa tisheti na kuwatungia nyimbo mafisadi.najua mpaka uchaguzi ufike tutawajua wanafiki aka waganganjaa na wanamapinduzi halisi.bravooooooooooooooooooooooooooooooooo:dance::A S 103::clock:
 
1.jpg

‘Sugu’ akionesha kadi yake baada ya kukabidhiwa na Kaimu Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mnyika (kushoto).

Wasanii ‘the big names ‘ kunako Bongo Fleva, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, Fred Malick ‘Mkoloni’ na Gerald Mwanjoka ’G Solo’, asubuhi ya leo wamejiunga rasmi na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kukabidhiwa kadi zao za uanachama. Tukio hilo limechukua nafasi katika Ofisi za Makao Makuu ya CHADEMA, zilizopo Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

2.jpg

Sugu, Mkoloni na G Solo wakionesha kadi zao baada ya kukabidhiwa na kujiunga rasmi na CHADEMA. Kushoto ni kaimu katibu Mkuu wa CHADEMA aliyewakabidhi kadi hizo.

68fnup.jpg

Kaimu Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mnyika akifafanua jambo baada ya kuwakabidhi Sugu, Mkoloni na G Solo kadi zao.

2vjtw5g.jpg

Sugu akieleza sababu zilizomfanya ajiunge na CHADEMA.

334p4jo.jpg

Mkoloni naye alieleza sababu zilizomfanya achague kujiunga na CHADEMA.

mcgrpw.jpg

G-Solo pia alieleza sababu zilizomfanya ajiunge na CHADEMA.

UFISADI! UFISADI!

21kbazq.jpg

Kaimu Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mnyika, akionesha kwa waandishi wa habari nyaraka za siri kutoka Chama Cha Mapinduzi alizodai kuwa zina siri kubwa juu ya namna ufisadi wa kugawa na kuuza maeneo ya wazi ulivyokuwa unafanyika.

PICHA: RICHARD BUKOS, MUSA MATEJA
STORI: AZIZ HASHIM/ GPL
 
Thanx for the pics, japo hii maneno tayari imeshawekwa na Gender Sensitive!
 
big up big up .... SUGU AU UKIPENDA MR 2 na wenzako ni haki yenu kidemokrasia kujiunga na chama chochote kile mmetimiza na kufuata kanuni na utaratibu wa katiba ya nchi inavyosema ...... nilishawahi kusema taifa hili iposiku wale wazalendo wa kweli ndio watakao liongoza tunafahamu harakati za sugu na wenzake toka miaka ya 1995 kwenye taifa hili .......... na wameamua kutumia vipaji vyao kuingia kwenye maisha mapya .... MR 11, G-SOLO , MKOLONI hakuna kulala mpaka kieleweke , CHADEMA ndicho chama mbadala wadau wengine endeleeni kuiunga chadema mkono
 
Bolded sijui kama hapa vyombo kama ITV TBC Clouds vitakuwepo mana hawa wote wanafiki wakubwa hawawezi kureport hii kitu

nawapongeza sana wewe wapiganaji wa ukweli sio kwenda kulala
kamanda walikuwepo wasipo riport wanalao jambo na tulitoa nyaraka za ufisadi mnispaa ya kinondon
 
These guys have made my jioni better......CONGRATULATIONS wapambanaji wapya....

Na nawaambieni kagombeeni ubunge sehemu yoyote ile na kitaeleweka tu....haiwezekani nyie wote mgombee hata mmoja wenu asipate....ila mmpambane...maisha ya kitaa mnayajua so msituangushe just in case mungu atawajaalia mkaukwaa uheshimiwa......

Nice Move...Nice attitude....msiwe kama wale tuwaonao Bongo 5 wamevaa mitisheti ya kijani wakitoa ujumbe mavi kuwa wao wameshachangia nasi tuchangie.....nani aweza ongeza chumvi baharini???????? Yule fisadi Rostam anahitaji kuchangiwa??? tena kwa msg ya jero??? akiamua kusambaza nyekundu alizonazo zinatapakaa nchi nzima....eti nae ni mtanzania?????? Hongereni sana masela..

....SHAVU KUBWA
 
Muda mfupi uliopita wanamuziki maarufu ndani na nje ya nchi Mr Sugu pamoja na Mkoloni wamejiunga rasmi na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA).

Hii habari imeninisisimua sana kwani inaendelea kuitoa CHADEMA kwenye siasa kavu (Hardcore Politics) kwenda kwenye siasa za kisasa zaidi. Obama ushindi wake mkubwa ulichangiwa sana na wasanii lukuki waliokuwa wanamuunga mkono, kuanzia Oprah Winfrey had Jay zee. Haiwezekani kuvutia kura za wanawake na vijana kama ndani ya chama chako hakuna wasanii maarufu wanaovutia vijana na kina mama.

Haya mambo ya ufisadi yanatuvutia sisi watu wa rika la miaka 35 na kuendelea, lakini vijana wanavutwa zaidi na jumbe zilizo kwenye mfumo wa uburudishaji (edutainment)
Bravo Mr Sugu,solo, Mkoloni, Nakaaya. Bado tunamsikilizia Afande Sele na Masudi Kipanya!!
 
Big up vijana mmeonyesha uzalendo wa kweli maisha bila CCM yanawezekana
 
Huku ndio kufanya kwa matendo vijana wadogo ubongo mkubwa, sasa ndio naamini kwamba Mr II amepania kupambana na wababaishaji na Rushwa na uonevu na udhalimu wa nchi hii.

This is great kwa sababu jambo hili vijana msipolingoa hadi kwenye mizizi basi kizazi chenu pia kitabaki kinanyonywa kama hiki chetu, sisi wazazi wenu tumewaangusha tumeshindwa kuwalinda imebidi mkue kabla y awakati, fanyeni mna baraka zetu mungu atawaongoza. Ni sala tu magoti kwa sana wale wa swala tano salini sana ndio ukombozi pekee wa nchi yetu, tumeshafikishwa pa baya sana ni mungu tu aalikwe kwenye hili ili aendelee kuwatumia watu wake kutukomboa.

Hii timu ni balaaa wale wajikombi wanaochangia CCM kwa msg wamekwisha kwanza hawajui kutunga pili wamezoea kubebwa wanategemea Kilimanjaro awards kutoka vijana sina la zaidi na ninawaamini kwa sana nyie na dr slaa mkishikana hakika tutasonga mbele
 
Back
Top Bottom