MPOKI wa orijino komedi na misemo ya ajabu

Pure nomaa

JF-Expert Member
Dec 10, 2011
1,158
1,382
Wakubwa kwa wale ambao kwa namna moja ama nyingine tume kuwa tukifuatilia vipindi vya original komedi nadhani mtakubaliana nami kwamba huyu sylvester mjuni aka MPOKI amekuwa na misemo ya ajabu ambayo nashindwa kuelewa kwamba amesomea au kipaji binafsi tu.Baadhi ya misemo yake ni kama
1.nyoka hana kiuno ndo maana havai shanga
2kukaa karibu na godauni si kupata kazi
3.usimsifu babako kwamba anajua kukimbia bali msifu na baba wa mwenzio aliyemkimbizia baba yako
4kukaa karibu na shule sio kujua kusoma
5kukaa karibu na mahakama sio kujua sheria
6kama akili ni nywele basi watu wasingenyoa siku ya mtihani na mengine mingi

wakubwa naomba kutoa hoja
 
kwani mpoki ni nani? Si muigizaji na mchekeshaji? Hicho ni kipaji baba kama walivyo kina kanumba na kina John cena.
 
huyu ndo bepari la kihaya alizaliwa wakati Mungu anafunga mahesabu yake. Nashut down
 
Mbona sijaona msemo wowote wa kusisimua hapo. Isitoshe hii misemo hajatunga yeye na badala yake huwa anakopi tu kutoka kwa Gea Habib yule wa kipindi cha ''Kwa Raha Zako'' cha Clouds Fm.
 
huyo ni mzee w kuongea pumba!! hii ipo kwnye nyimbo yake mpya " BATA HATA AWE MCHAFU VIPI BADO ATATAGA YAI JEUPE"
 
Misemo anayoitumia iko mtaani sema kwa sab kaamua misemo iwe nembo yake anakuwa na kazi ya kuitafuta ili awape mashabiki wake sawa tu na Muhogo Mchungu alivyoamua kutumia methali....hata akiingia jf anaondoka na misemo mingi tu'
 
Mbona sijaona msemo wowote wa kusisimua hapo. Isitoshe hii misemo hajatunga yeye na badala yake huwa anakopi tu kutoka kwa Gea Habib yule wa kipindi cha ''Kwa Raha Zako'' cha Clouds Fm.

nawewe umezidi kumsifia Gea habibi na mawingu fm,kwani huyo gea ni nani?
 
Hii misemo imenikumbusha ile katuni ya Bingwa wa rivasi aka rivasi wa bingwa! Jamaa alikuwa anasema "Refarii kama umetoka choka!" akimamaanisha "Refarii kama umechoka toka"
 
Watu vigeugeu sana humu ndani. Mara Original Comedy wanatumiwa na CCM mara tena ooh Mpoki anajitahidi sana. Kweli hakuna dawa ya kutibu unafiki duniani na hasa ukiwa umeahaingia ubongoni.
 
Watu vigeugeu sana humu ndani. Mara Original Comedy wanatumiwa na CCM mara tena ooh Mpoki anajitahidi sana. Kweli hakuna dawa ya kutibu unafiki duniani na hasa ukiwa umeahaingia ubongoni.
JF ina members wengi sana, kwa hiyo ukisikia sabini wameponda, usishangae kesho yake themanini wamesifia kitu kile kile. Kama una ushahidi kwamba yule yule aliyeponda jana, leo hii amekuja kusifia, wewe muumbue tu kwa kuweka link za posts zake zinazokinzana humu!
 
Back
Top Bottom