Mpinzani wa kweli alikuwa ni Rais Magufuli

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Sep 20, 2021
3,214
3,587
Upinzani wa Tz unatakiwa kuzaliwa upya kwa kutumia mifumo ya demokrasia komavu na pevu za USA na Uingereza ambapo mgombea anaposhindwa uchaguzi mmoja basi uchaguzi unaofuata hagombei tena bali anaachia ngazi kwa kutoa nafasi kwa sura mpya asilani. Sura moja ikizoeleka sana ni sawa na adui kuzoea mbinu zako za medani na kwamba huwezi kumshinda kamwe. Vyama vya upinzani vinaendeshwa kama vile makampuni ya biashara ambapo mwenye hisa kubwa ndiye mwenye sauti na ndiye mwenye hatima ya chama mikononi mwake. Demokrasia ndani ya vyama haiwezi kustawi kwy mazingira kama haya.

Kama wanaokihama CCM kwenda upinzani ni mtaji mzuri, iweje wahame tena upinzani kurudi CCM? Ni mamluki au kuna nini huko upinzani? Na kuna nini CCM wanakorudi? Au Watz waamini kuwa upinzani uliopo umetengenezwa na CCM kama ilivyokuwa kwa Mobutu Tseseseko wa iliyokuwa Zaire aliyesajili vyama feki vya upinzani 400? Siyo lazima uwe muasisi wa chama na uishi kuona ukiingia ikulu, bali unaweza kuishia kukiasisi chama tu na ukaishi kuona wengine ndiyo wanatumia chama chako ulichoasisi kwenda ikulu na siyo lazima anayeingia ikulu aishi huko kwa matakwa yako la hasha bali kwa matakwa ya katiba ya nchi anayoapa kuilinda na ni haki yake huyo aliyeko ikulu kutofautiana kimantiki na mitazamo na wewe muasisi wa chama hicho kilichompeleka rais huyo ikulu. Mzee Jawaharlal ChaCha Nehru hakuwahi kuwa rais lakini dunia nzima ilimheshimu kuliko marais wengi tu.

Mnisamehe kama nitakuwa mtovu wa nidhamu kwa kuamini kuwa mpinzani wa kweli si mwingine bali alikuwa ni rais JPM kwa kuwa tangu akiwa Waziri aliendelea kuwa na msimamo wa kihafidhina dhidi ya ufisadi, ukengeufu wa kimaadili na matendo mengine yanayofanana na hayo ambayo yayo hayo yamekuwa yakifisha jitihada za utoaji haki katika taifa. Hakusubiri mpaka awe rais au mpaka ahamie kambi ya upinzani kwanza. Na hii amefanikiwa kutokana na kuwa hakuwa na roho wa uwoga na aliamini katika ukweli usionafikiwa.

Rais JPM wa awamu ya 5 ndani ya miezi minane tu ya serikali yake, alishughulikia kwa vitendo halisi chagizo takriban zote za kambi ya upinzani ambazo hizo ziliiweka nchi njiapanda. Basi kwa rekodi na mizania hiyo twaweza kuamini kwamba rais JPM ndiye alikuwa mpinzani wa kweli aliyefanya upinzani pasina kulazimika kuhamahama vyama ambako kulitafsiriwa kuwa ni kutawaliwa na roho wa uwoga ambao ukikughubika basi huwezi kuchagiza mabadiliko chanya tarajali.

Hii inamaanisha kwamba hata ndani ya CCM pia kama ilivyo ndani ya upinzani kuna magugu ya mbigili yanayohitaji kung’olewa kwa greda kabisa. Mfano, CCM hakina haja kabisa na wala hakistahili kuruzukiwa na hazina ya serikali kwa sababu tangu kimeanzishwa kimemiliki rasilimali ambazo kama kingekuwa na usimamizi mzuri basi leo kingekuwa ndicho kinairuzuku serikali badala ya serikali kukiruzuku. Licha ya ruzuku inazopewa, hatujui Sukita iko wapi (ingeweza kulisha Dar kwa nafaka, samaki, nyama ya ndege na hayawani, mbogamboga, maziwa, mayai, jibini na siagi maana kingetumia fursa nzuri zilizopo za kilimo kwanza na matokeo makubwa sasa kujipanga kwa tija).

Aidha, umma haujui, labda CAG na PCCB wanaweza kujuwa wakikagua mapato ya viwanja vyote vya michezo vilivyo tapakaa nchi nzima ambavyo licha ya kukusanya mapato makubwa bado vimeendelea kudorora sana lakini pia tunatamani kusikia shule zile za upili (sekondari) za Jumuiya ya Wazazi wa CCM TAPA zilizokuwa takriban kanda zote za nchi yetu na kusomesha wanasiasa maarufu wa leo akiwamo Mama Margareth Sitta ziko wapi na zinaingiza shilingi ngapi? Mikataba ya ujenzi na hatimaye umiliki wa muda mrefu sana wa majengo ya vitega uchumi kwy viwanja vya Jumuiya za CCM UVCCM na UWT inahitaji kufafanuliwa pasina chembe ya shaka yoyote.

Halikadhalika, tukigeukia upinzani, hatuwezi kujuwa kwa uhakika wa takwimu zilizokaguliwa na mkaguzi wa serikali matumizi ya zile ruzuku unazopata toka serikalini, mfuko wa bunge, misaada toka kwa wafadhili wa ndani na nje, ada za wanachama nk. Wakati fulani kamati ya bunge ilipojaribu kuhoji hili, wajumbe wake ambao walitoka kambi ya upinzani walionja shubiri isiyomezeka kabisa na kuwa mwanzo wa mgogoro ndani ya chama sawa na migogoro ya vilabu vya mpira.

Yumkini mapato yote ya upinzani yana lengo moja tu kuu la kwenda ikulu na kwamba labda matumizi yake yamefungwa tu kwy posho za kuzunguka nchi kuendesha mikutano, maandamano na harakati zingine kama kurusha chopa hewani kwy kampeni nk na kwamba hayo yamefanyika kwa miaka mingi huku vitanda mawodini, madawati mashuleni, elimu bure, ukusanyaji wa mapato ya serikali vikisubiri mpaka JPM awe rais na kwamba wao walipougua walipanda ndege kwenda nje ya nchi ama kwa ukwasi wao binafsi, rasilimali-fedha za chama au kwa fadhila za serikali zinazotokana na vyeo vyao.

Falsafa ya JPM ya kazi tu haina budi kuheshimiwa na kutekelezwa na kila mzalendo wa nchi hii pasina kujali tofauti za kiitikadi na falsafa za makundi-maslahi katika jamii yetu. Lazima tupae na siyo kukimbia ili kufikia dira yetu ya maendeleo ya 2025. Ebu tafakari miujiza hii ya Israel na Shelisheli uone jinsi ambavyo tunahitaji kama taifa kuishi falsafa ya rais JPM kuhusu dhana nzima ya maendeleo.

Wastani wa pato la kila mtu Israel GDP per capita ni US$ 36,151.21 [2013], ikiwa na idadi ya watu 8,296,000 ml [2014] wakati Tz ni US$ 502.08 [2013] kwa mujibu wa Benki ya Dunia. Pato-ghafi la Israel GDP ni US$ 291.4 bl [2013], ukizidisha GDP ya Israel zikiwa katika US$ na GDP ya Tz kwa bei ya soko la US$ 1 = Tzs.1750 kwa mwaka huo, hutaamini kalkuleta yako [jaribu kukokotoa uone, kwa tafsiri nyingine ni kuwa ukigawa jibu lako hilo kwa miezi 12 ya mwaka wa fedha kutafuta wastani wa makusanyo ya mapato ya Israel kwa mwezi mmoja utagundua kuwa pato la mwezi mmoja la Israel ni bajeti ya Tz kwa miaka miwili kwa mwaka huo wa 2013], na hapo sasa uone bajeti ambayo Israel inatumia kwa watu 8,296,000 ml tu ambayo hii inaweza kulingana na idadi ya watu wa mikoa miwili tu ya Tz, dhidi ya bajeti ya Tz kwa watu 44,928,923 ml [Sensa ya 2012].

Wastani wa maisha [life expectancy] ya Muisrael ni miaka 84.0 kwa wanawake na miaka 80.02 kwa wanaume [2014], Tz wastani wa jumla wa maisha ni miaka 61 [2012]. Waisrael wanaishi kwa mbali zaidi miaka ya Biblia. Kama sera ya diplomasia yetu inalenga uchumi zaidi kwa nini tuendelee kuvunja uhusiano na taifa kama Israel ambalo ni uchumi wa 19 kwa ukubwa duniani kwa takwimu za mwaka 2013 huku ikiwa vitani tangu ilipopata uhuru wake mwaka 1948 hata leo (vita iliyovunja rekodi ya dunia kwa kupiganwa kwa miaka 73 hadi sasa na huenda ikaendelea milele) pasina kupumzika, tena na maadui zaidi ya moja? Huu ni uchumi pekee wa ajabu duniani unaokuwa katika vita ya miaka 73 sasa.

Tz ina ukubwa wa 945,203 km2, Israel ina ukubwa wa 20,770 km2, ukigawanya unakuta Israel inaingia kwa Tz mara 45.5. Shelisheli taifa ambalo ukubwa wake ni takriban ukubwa wa kata moja ya Tz; ina ukubwa wa 455 km2, ukigawanya kwa ukubwa wa Tz wa 945,203 km2 unakuta Shelisheli inaingia kwa Tz mara 2,077.4, lakini kasi [siyo ukubwa wa mapato] ya ukuaji wa sekta ya utalii ambayo ndiyo sekta mama ni kubwa kuliko ya Tz, huku fukwe za Shelisheli miaka ya mwisho wa 90s kuja 2000s zilikuwa katika kumi bora duniani zikitanguliwa na Miami ya USA. Je, Tz kama tukiendelea kupinga kila jitihada nzuri alizofanya rais JPM kwa kuacha kufanya kazi na kuendekeza kuzama kwy maandamano, mikutano ya hadhara, migomo, kususiasusia bunge, kufumuana vyeo ndani ya vyama vya siasa nk tutaweza kuifikia Israel?

Wastani wa pato la kila mwananchi (GDP per capita) inatakiwa ifikie US$ 3,000 (in nominal terms) ifikapo ukomo wa dira ya maendeleo ya taifa 2025, rejea chapisho la mpango wa maendeleo ya taifa 2011/2012-2015/2016 (ambayo imeainisha fursa za ukuaji ambazo hazijatumika) kama ilivyoandaliwa na ofisi ya rais tume ya mipango, toleo la Juni 2012 uk wa 2. Hivi sasa wastani wa pato la kila mwananchi wa kawaida wa Tz kwa siku linapigiwa propaganda duniani kuwa ni chini ya US$ 1, sasa tuna miaka kama 4 hivi kufikia ukomo wa dira ya maendeleo ya taifa 2025, tukiendekeza siasa za maandamano yasiyokoma, mikutano ya hadhara ya mara kwa mara, ususiaji wa vikao na mabaraza ya mihimili ya uendeshaji nchi ambako huko ndiko maamuzi yenye kubeba mustakabali wa uhai wa taifa yanafanyikia je, tuna uthibitisho upi usiotiliwa shaka kuwa kufanya siasa saa 24 kwa siku, siku 7 kwa juma, siku 30 kwa mwezi na siku 365 kwa mwaka na kwa miaka yote 5 ya kukaa madarakani; pasina kutekeleza falsafa ya kazi tutaweza kufikia pato hilo la US$ 3,000 kama tume ya mipango ilivyobashiri? Tangu dira hii iasisiwe na Mhe. Mkapa (Big Ben) 1995 hadi leo, licha ya jitihada nzuri zilizohakikishwa na serikali yake na zilizofuata, bado tumeendelea kukaririwa ngonjera ya uchumi kuwa Mtz wa kawaida anaishi chini ya US$ 1 kwa siku, sasa huku ambako kambi ya upinzani unataka kutupeleka je, tutafika kweli 2025 tukiwa na pato hilo la US$ 3,000? Hawaoni kwamba tunatakiwa tupae kabisa badala ya kukimbia? Hata baada ya JPM kuliingiza taifa kwy uchumi wa kati wa chini ukweli mitaani nchi nzima unadhihirisha kwamba Mtz wa kawaida ambao ndiyo 90% hawana pato hilo kwa siku. Baghosha!

majwalaoriko@yahoo.co.uk
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom