22nd
JF-Expert Member
- Aug 1, 2010
- 495
- 137
Una sema kweli lakini tuludi nyuma, Daradara ni biashara sidhani kama utapenda ufanye biashara kila siku upate hasara. Kwa ustaarabu wa huyo konda wa kuchukua wanafunzi sita alionyesha utu kabisa, kuliko wale ambao huwa wanawagomea wanafunzi kabisa. Kama utakuwa unafanya biashara utanielewa nina maana gani. Jioni huyo konda atatakiwa apeleke marejesho ili atetee kibarua chake. Lakini kuna watu mjini huwa wanadhani hizo daradara zinatolewa rudhuku na serikali. Akipakia wanafunzi wachache basi na daradara nyingine nayo ije ichukuwe wengine kuliko wote kulundikana kwenye gari moja kama vile imegeuzwa school bus.
Sijasema huyo konda ana makosa wala kuibeza hiyo kazi yake,coz sina hiyo style ya kudharau watu, simdharau ninayemjua na nisiyemjua pia.
ninachosema mimi hapa watanzania kumuona huyo konda eti educated kisa tu ameongea kiingereza, jamani,mpo dunia ya ngapi? kiingereza ni lugha tu kama lugha nyengine.