Regia Mtema
R I P
- Nov 21, 2009
- 2,970
- 864
Wakuu.
Niliwahi kutoa sredi hapa kwamba nilikuwa na mpenzi wangu ambaye alikuwa wa kwanza nilikutana naye nikiwa chuo tukaachana siku ya wapendanao..Jamaa yangu huyu anatarajia kufunga pingu za maisha mwezi wa tano mwaka huu.Siku chache zilizopita alinipigia simu na kuniambia kwamba anatarajia kufunga pingu za maisha na kuniomba nimchangie ili kufanikisha harusi yake.ikumbukwe kwamba hatkumalizana vizuri na huyu jamaa ingawa amekuwa akilazmisha mara nyingi kwamba tuwe best friends,hili alilisema hata wakati tunaachana lakini kwangu mimi niliona ni upuuzi,sikujisikia kuwa karibu naye hasa kirafiki ingawa tumekuwa tukiwasiliana kwa njia ya simu mara moja moja kila mtu akimkukmbuka mwenzake.Nilimueleza bila kuficha kwamba sitamchangia hata senti moja kwani sijisikii kufanya hivyo.Ikumbukwe kuwa tuliachana tukiwa hatujagombana hata kidogo wala kuwa na makosa ya kupelekea kuachana.
Naombeni ushauri nafanya vibaya kutomchangia?