MFALME WETU
JF-Expert Member
- Feb 1, 2021
- 2,608
- 6,217
Habari za sahizi keyboard masters..
Ni muda sasa nimekuwa kwenye mahusiano na huyu mrembo kutoka huko kaskazini, tulikutana chuo tukiwa classmates ila rasmi mahusiano yetu yalianza tukiwa mwaka wa pili semester ya kwanza.
Kipindi chote hicho sikuwahi kugundua kuwa anatumia sigara wala bangi zaidi ya pombe ambazo tulikuwa tunakunywa pamoja ila ghafla tu tulivyorudi chuo semester ya pili nilienda kumtembelea kwake bila taarifa nikashangaa kumkuta anavuta sigara tena kashikilia pakiti nzima ya Winston Sports.
Sikuongea kitu nikaamua kuondoka badae akanitumia meseji ndefu ya kuniomba msamaha kwa kunificha kipindi chote hiko ila akasisitiza hawezi kuacha hiyo tabia na mimi nikaona isiwe kesi ila nikamuweka kwenye list ya wanawake wa kujipigia pasina kuwa na malengo yoyote ya ndoa huko mbeleni.
Kipindi chote hicho yupo mjamzito nimekuwa nikimsititiza kupunguza matumizi ya pombe na kuacha kuvuta bangi na sigara akanambia kuwa kaacha sigara ila bangi hawezi kuacha kwa kuwa anaamini haina madhara.
Sasa wajuvi wa mambo naomba kujua kama kweli bangi haina madhara kwa mtoto au la na kama ina madhara naombeni ushauri nitumie mbinu gani kumshawishi aache kutumia.
Natanguliza shukurani