Mpenzi wangu ameathirika,nipeni ushauri nifanyaje ?.

Pole sana kijana, ila hakuna njia zaidi ya kuachana na huyo dada maana tayari ameisha athirika pamoja hivyo tumieni ushauri mliopewa angaza na pia usimuache kwa haraka subiri hadi atakapokubaliana na hiyo hali ndipo muongelee maisha yenu ya badae na hali halisi ya wewe kutomuoa tena.
 
unless kama una yale mapenzi ya tamthilia...move on dude...24 is too young for such commitment
 
Ujinga wa kusex na mtu mwenye VVU inakuwa taabu kufeel utamu hata kama utatumia condom.Yaan waweza ogopa hata mavuzi yake.Real i say
 
Pole sana, hapo kwenye rangi labda mwenzio alikuwa ana wasiwasi kuhusu afya yake hivyo akaona ni bora mkapime wote ili kujua kama ni wazima, au alishajua kama yeye ni muathitrika ila alikuwa anashindwa namna ya kukwambia kwamba yeye ni muathirika hivyo akaona njia nzuri ni kwenda kupima wote ili ujue hali yake badala ya yeye kukwambia. Ni vizuri kwenda sehemu nyingine mbili tofauti ili kuhakikisha hayo majibu hayana makosa.

Mimi ni kijana wa miaka ishiri na nne ninaishi hapa mkoani Arusha na pia ni mwanachuo ktk chuo kimoja kilichopo karibu kabisa na hospitali ya seliani mjini.
Ninae mpenzi wangu ambae tunapendana sana na mapenzi yetu yalianza miaka miwili iliyopita na ktk miaka yote hiyo hatakuwahi kukutana kimwili kwa kuamini kuwa sisi tunatakiwa kuwa mume na mke siku za baadae.
Kwa muda sasa mpenzi wangu huyo alikuwa akinishauri mara kwa mara juu ya swala la kupima na ndipo siku ya jana mimi na yeye tulipoenda kupima ktk kituo cha Angaza kilichopo mjini hapa na majibu yalotoka ni kwamba mpenzi wangu huyo ameathirika na mimi nipo salama.
Kusema kweli toka majibu hayo yatoke mpenzi wangu huyo alilia sana kwa kuamini kuwa nitamuacha na ukweli ni kwamba nampenda sana na sijajua mpaka muda huu kwanini aliamua kunishawishi tukapime.
Bado moyo wangu unampenda sana.
Naombeni ushauri nifanyaje,nimuache au nifanye nini ?
 
aisee hongeren kwa kucheck afya nina da pole xana kwa dda yangi hataki kabixa!kkubwa ucmtenge ila ucwe na uhucano nae kwa sababu ww bado kijana mdogo na maisha bado wko kuwa nae karibu na company ya kawaida.ila very xcory kwa kutahifisha penz lako la ukwweli omba utampta wa ukwel mwngne na yeye atampta mwenzie tu na ataishi kwa furaha kabixa.

hiki kiswahili cha wapi?
 
Pole sana kijana, ila hakuna njia zaidi ya kuachana na huyo dada maana tayari ameisha athirika pamoja hivyo tumieni ushauri mliopewa angaza na pia usimuache kwa haraka subiri hadi atakapokubaliana na hiyo hali ndipo muongelee maisha yenu ya badae na hali halisi ya wewe kutomuoa tena.

ni kweli mkuu,pole kaka
 
Endeleeni kuwa wapenzi bila kufanya ngono kwa miaka mingine 3, hopefully dawa itakuwa imepatikana by the time you are 27 ndipo mfunge ndoa.

Kama alivyosema BAK huenda alikuwa anajijua afya yake na alitaka kukulinda; so usimuache kwani mkataa pema pabaya panamuita. Waweza pata mwingine hiv negative lakini within a year akausomba au wewe ukautafuta kungine na kuambukizana.
Anyway ni namna nyingine ya kulitazama swala lako.
 
Last edited by a moderator:
Pole sana kijana, ila hakuna njia zaidi ya kuachana na huyo dada maana tayari ameisha athirika pamoja hivyo tumieni ushauri mliopewa angaza na pia usimuache kwa haraka subiri hadi atakapokubaliana na hiyo hali ndipo muongelee maisha yenu ya badae na hali halisi ya wewe kutomuoa tena.

Ushauri mzuri, ila hiyo ya kutomuoa ndiyo inayofanya maambukizi yaendelee. Hivi muathirika hana hamu ya ngono?

Au kuna ushauri nasaha utakaomuondolea hamu ya ngono.

Unafikiri kama kwa uwazi wake ameachwa, akikutana na mwingine atakuwa wazi?
 
mungu wangu na mi sijapima eti mpaka leo kama hujaathirika usimwache mapema hii wala msifanye mapenzi cha msingi mshauri mawatafute ndugu zake uwaeleze jambo hilo na umkabiz ktk mikono salama utafute wa kumuoa ila uendelee kuwasiliana nae usimwache mpweke inauma sana kwa kweli na hongereni kwa ujasir wa kwenda kupima coz mwenzenu mm naogopa!

Unaonekana mtundu mtundu wewe,, mh!! sa unaogopa nini?
 
Pole sana, cha msingi hapa tutakuwambia mara usimwacha mara vile. Rudini kwa washauri nasaha wataongea nanyi pamoja na muwe wazi kuwa mlikuwa marafiki ambao mlitegemea siku moja mtaoana. Hapo mshauri nasaha atakuwa na pa kuanzia na atakuwa anawapa elimu kiasi kwamba hata huyo binti atakuja kuridhika siku moja kuwa hamtaweza kuishi pamoja. Vinginevyo kama mkiamua kuishi pamoja napo pia kuna elimu mtapewa jinsi ya kuishi. Kuna dada mmoja alimpata boyfriend na walipenda kupima wakakuta boyfriend ana VVU. Walipewa elimu na wakawa wapenzi rasmi kwa kutumia condom tu na wapo fresh for 6 years now ila ni nchi za wenzetu. Hata Tza inawezekana tu kama mtapata elimu ya jinsi ya kukukutana kimwili na pia hata kama mnataka kuzaa kuna jinsi mnafundishwa kukutana the very day. Kila kitu kinawezekana pale wataalam wanapoelezea uhalisia na ukweli wa jambo. Use them.

Thank God! u pointed that,,,kikwetu kwetu bado saaana,,
 
Nimefanya utafiti mdogo tu kutokana na baadhi ya replies hapo juu nimegundua UNYANYAPAA ndio unaua zaidi kuliko UKIMWI wenyewe. yeye kuwa na AIDS hakuzuii wewe kumpenda.
 
Back
Top Bottom