Mpenzi wangu ameathirika,nipeni ushauri nifanyaje ?.

No war

Member
Jun 28, 2013
26
8
Mimi ni kijana wa miaka ishiri na nne ninaishi hapa mkoani Arusha na pia ni mwanachuo ktk chuo kimoja kilichopo karibu kabisa na hospitali ya seliani mjini.
Ninae mpenzi wangu ambae tunapendana sana na mapenzi yetu yalianza miaka miwili iliyopita na ktk miaka yote hiyo hatakuwahi kukutana kimwili kwa kuamini kuwa sisi tunatakiwa kuwa mume na mke siku za baadae.
Kwa muda sasa mpenzi wangu huyo alikuwa akinishauri mara kwa mara juu ya swala la kupima na ndipo siku ya jana mimi na yeye tulipoenda kupima ktk kituo cha Angaza kilichopo mjini hapa na majibu yalotoka ni kwamba mpenzi wangu huyo ameathirika na mimi nipo salama.
Kusema kweli toka majibu hayo yatoke mpenzi wangu huyo alilia sana kwa kuamini kuwa nitamuacha na ukweli ni kwamba nampenda sana na sijajua mpaka muda huu kwanini aliamua kunishawishi tukapime.
Bado moyo wangu unampenda sana.
Naombeni ushauri nifanyaje,nimuache au nifanye nini ?
 
Mshukuru Mungu wako kuwa uko salama na muhimu kwa huyo unayemuita mpenzi wako ni kuwa kupata hivyo virusi sio mwisho wa kuishi na wala hawezi kufa leo ila ajilinde na asiwaambukize wengine na dawa zipo nafikiri ulipata ushauri au mlipata ushauri wa kutosha kutoka kwa waliowapima
Ajitahidi kula na kutumia dawa ipasavyo na wewe kuwa nae karibu tuu kwa ushauri
Kwanza zingatia masomo yako hilo ndo la muhimu na naamini itafika kipindi utapata wako wa kuoana nae
 
Tulipoenda kupima kila mtu alienda kivyake na mimi nilidai kuwa nimemsindikiza na lilipokuja suala la kuchukua majibu kila mtu alimshirikisha mwenzake lakin hatukujitambulisha kuwa sisi ni wapenzi.
Jibu ktk swali la Amu.
 
msipanic na majibu ya kwanza,,,karudiani hata sehemu nne tofauti sometime vipimo huwa vinatoa majibu fake..ilitokea
 
Aisee pole sana kijana. Bila shaka mlipata ushauri nasaha juu ya hilo. Kinachotakiwa ni kuutendea kazi.Hakikisha anafwata masharti ya daktari kwani huo sio mwisho wa maisha yake. Anaeza akawa muathirika na akaishi miaka mingi kuliko hata yule asiyeathirika.
 
Mlipewa ushauri nasaha kabla na baada ya kupima,nadhani ule ni muhimu kuliko utakaopata hapa JF....cha kukuongezea ni kwamba hiki ni kipindi ambacho unatakiwa kuonesha upendo wako kuliko wakati mwingine kwa mwenzio!
 
mungu wangu na mi sijapima eti mpaka leo kama hujaathirika usimwache mapema hii wala msifanye mapenzi cha msingi mshauri mawatafute ndugu zake uwaeleze jambo hilo na umkabiz ktk mikono salama utafute wa kumuoa ila uendelee kuwasiliana nae usimwache mpweke inauma sana kwa kweli na hongereni kwa ujasir wa kwenda kupima coz mwenzenu mm naogopa!
 
najaribu kuvaa viatu vyako....................mmh ngumu kwa kweli !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
aisee hongeren kwa kucheck afya nina da pole xana kwa dda yangi hataki kabixa!kkubwa ucmtenge ila ucwe na uhucano nae kwa sababu ww bado kijana mdogo na maisha bado wko kuwa nae karibu na company ya kawaida.ila very xcory kwa kutahifisha penz lako la ukwweli omba utampta wa ukwel mwngne na yeye atampta mwenzie tu na ataishi kwa furaha kabixa.
 
nenda na wewe ukapime tena huenda virusi havijaonekana!! Kila baada ya miezi mitatu nenda kapime
 
Pole sana, cha msingi hapa tutakuwambia mara usimwacha mara vile. Rudini kwa washauri nasaha wataongea nanyi pamoja na muwe wazi kuwa mlikuwa marafiki ambao mlitegemea siku moja mtaoana. Hapo mshauri nasaha atakuwa na pa kuanzia na atakuwa anawapa elimu kiasi kwamba hata huyo binti atakuja kuridhika siku moja kuwa hamtaweza kuishi pamoja. Vinginevyo kama mkiamua kuishi pamoja napo pia kuna elimu mtapewa jinsi ya kuishi. Kuna dada mmoja alimpata boyfriend na walipenda kupima wakakuta boyfriend ana VVU. Walipewa elimu na wakawa wapenzi rasmi kwa kutumia condom tu na wapo fresh for 6 years now ila ni nchi za wenzetu. Hata Tza inawezekana tu kama mtapata elimu ya jinsi ya kukukutana kimwili na pia hata kama mnataka kuzaa kuna jinsi mnafundishwa kukutana the very day. Kila kitu kinawezekana pale wataalam wanapoelezea uhalisia na ukweli wa jambo. Use them.
 
nenda na wewe ukapime tena huenda virusi havijaonekana!! Kila baada ya miezi mitatu nenda kapime

Katika post ameweka wazi kuwa walikuwa hawajawahi kukutana kimwili kwa kuwa walikuwa na malengo. Ila pia si vibaya akipima kwa afya yake.
 
Maadamu hamjaoana, ni vyema mahusiano yenu yakaishia kama kaka na dada.
 
Kaka itakua ni vigumu kuendelea nae ila usiwe mbali nae na usije kujaribu kumtenga kwa namna yeyote ile mfanye awe rafiki yako WA karibu sana endelea kumpenda.
 
Back
Top Bottom