Mpanda: Machinga waiomba Serikali kuzifuatilia Kampuni za Mikopo

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,988
Wafanyabiashara wadogo maarufu kama machinga Mkoani Katavi wameiomba Serikali kuzifuatilia taasisi na kampuni za utoaji mikopo kwa Wafanyabiashara kutokana na kuwepo kwa malalamiko ya udanganyifu ikiwa ni pamoja na utoaji mikopo kandamizi.

Hayo yamebainishwa na Wafanyabiashara hao katika Baraza la Machinga Mkoani Katavi ambapo wamesema baadhi ya kampuni hizo zinatoa mikopo kwa kutofuata taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa sheria.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Machinga Wilaya ya Mpanda, Haji Mponda ameiomba Serikali kupitia Halmashauri za Wilaya kuwashirikisha Machinga hasa katika masuala ya Wafanyabiashara kabla ya maamuzi huku Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yusuf akiwahakikishia Machinga hao kwa namna bora Serikali inavyoendelea kuweka mazingira mazuri ya kibiashara.

Aidha, Jamila amewataka machinga hao kutotumika vibaya katika mambo ya kisiasa hasa katika uchaguzi ujao.
 
Back
Top Bottom