Moyo ukikataa unaweza sema kwa mwenzio?

<br />
<br />
izo imani potofu unaonekana unapenda pochi eeeeh?
mie najua kuzitafuta za kwangu, ila huo ndio ukweli usiopingika kwamba watu wanachungulia una nini mfukukoni, nina mifani michache ya maclass mate wangu wa sec walikuwa wanasema kabisa, "mie nimetoka kwenye umaskini siwezi tena kuolewa kwenye umaskini"
 
Ni kweli inatokea hivyo.. Lakini kwa nini watu wanatumia "Moyo" wangu umekataa. Moyo hausemi, moyo ni maumbile. Ukweli kilichokataa ni akili yako ya kichwani.

Kama unakubali kilichokataa kiko kichwani..Basi kumbuka akili kichwani inachangiwa na mawazo. Mawazo yanatokana na Maisha. Mawazo, akili, maisha havigandi.. vinabadilika.. Hivyo kusema imechukua miaka mitano ni uongo!

Ukweli ungesema.. nimebadilika kimawazo....Sina upendo kama wa mwanzo.... Nikiendelea hivi nitakuumiza zaidi....Tuachane!
 
Wanajamii naomba tuijadili hii changamoto kwa kina

Hivi kuna mapenzi ya kujilazimisha kupenda?
Na kama umejigundua ulipenda kusiko sahihi unaweza kumwambia mwenzio waziwazi kuwa unajilazimisha tu?

Nauliza maswali haya kutokana na kisa nilichosimuliwa na mtu wangu wa karibu sana (Mars) kuhusu kuvunjika kwa uhusiano wake na aliyekuwa mpenzi wake (Venus), na hiki ndicho kilichotokea
Mars: Yaani pamoja na kukaa kwa miaka yote bado unasema hujanipenda na wala hujawahi kunipenda
Venus: Nakwambia kweli kwa miaka yote mitano, nimejitahidi mno kujiforce na kujiweka karibu sana na wewe lakini naona MOYO wangu mzito na unakataa kabisa kukupokea

Mars:
Mbona nimekupa na nimekufanyia kila kitu kwa uwezo wangu wote?
Venus: Yaani wewe ni Mwanaume wa shoka, kila kitu nilichotaka nakipata na pia ni mzuri mno hata kwenye 6x6 na wala sina tatizo kwa hilo,
tatizo ni MOYO, nimejaribu kujibembeleza na kujipa moyo sana kuhusu mapenzi yangu kwako, lakini MOYO umekataa kabisa na najiona ni kana kwamba kuna kitu najidhulumu au nakudhulumu.
Nakwambia ukweli kwa miaka yote niliyokuwa na wewe sijawahi wala sina mtu wa pembeni,nilijaribu kukuweka karibu sana, lakini kuna kipindi nakuwa mpweke na kujiona sipo sahihi kuwa na wewe (kilio)

Mars:
Tatizo ni nini sasa
Venus: Tatizo ni MOYO unakataa kabisa, najiona napwaya na nina hofia kuwa siku za mbele tutakuja achana kwa shida na matatizo, ni bora tuachane ingali mapema na mimi niupe MOYO wangu unachokitaka, kuliko kujilazimisha kuwa na wewe, naomba nisamehe kwa niliyosema (Kilio tena),
Hapo kwenye red, ina maana kabla ya ndoa ilikuwaje? kwani alilamlazimishwa kufunga naye ndoa au amegundua moyo unakataa baada ya ndoa? hebu na ajichunguze kwa makini huenda yeye ndiye mwenye matatizo, kama anachotaka anapewa kwa muda wote huo, huyo ni ibilisil anataka kusambaratisha ndoa hiyo
 
unajua kuna ile ntamzoea na tutawezana tu,
ndoa nyingi zipo kwenye hali ya kuishi ili mradi kulinda heshima kwenye jamii na kwa watoto,
 
Inatisha ila ni ngumu sana kumwambia mtu ulie kua nae kimapenzi kuwa ulikua umpendi mi ningeshindwa
 
Ni kweli inatokea hivyo.. Lakini kwa nini watu wanatumia "Moyo" wangu umekataa. Moyo hausemi, moyo ni maumbile. Ukweli kilichokataa ni akili yako ya kichwani.

Kama unakubali kilichokataa kiko kichwani..Basi kumbuka akili kichwani inachangiwa na mawazo. Mawazo yanatokana na Maisha. Mawazo, akili, maisha havigandi.. vinabadilika.. Hivyo kusema imechukua miaka mitano ni uongo!

Ukweli ungesema.. nimebadilika kimawazo....Sina upendo kama wa mwanzo.... Nikiendelea hivi nitakuumiza zaidi....Tuachane!

unajua mtu akiandika MY sweetHEART, Corner of my HEART, broken HEART nk huwa zinaeleweka sana na inaonekana kuwa ni normal,
lakini unaposema MOYO maswali kama yako ndio yanajitokeza
 
Back
Top Bottom