Moshi: Yaliyojiri Mei Mosi 2017, Rais Magufuli amwaga ajira Elfu 52, madaraja kupanda....

Kuna watu uelewa wao mdogo mpaka unashangaa. Hivi maamuzi ya mwaka wa fedha mpya na maslahi ya watumishi kwa utamaduni wetu Tanzania hufanyika lini ?
Leo kama amesema tusubiri mwaka ujao inamaana si mwaka wa fedha wa 2017/18 bali ni 18/19.
Ikumbukwe kasema kwamba mwakani tukikutana wakati kama huu tutarajie mambo mazuri.Mtoa mada yuko sahihi kabisa,
Hapa tusijifariji bajeti hii ya 2017/18 haongezi wala hapunguzi kitu.
 
Kesho naamkia kwa mkurugenzi kuichukua check yangu kwani alinihamisha tangu january na sioni dalili ya kunilipa.
Nitaicharge simu yangu nikamfungulie you tube yenye hotuba hii ua leo na akiniletea fyoko namripoti magogoni kwa kubeba bango kubwa lenye maandishi " mkurugenzi wa manispaa x ameyadharau maagizo yako, tafadhali mtumbue kwa kuyarudisha matumaini ya serikali ya viwanda".
 
Mkuu ametulia sana Rais leo hii ni tofauti na hotuba zake zote Mungu anashuhudia.
(UMEONGEA NA MUNGU SAA NGAPI AKAKWAMBIA ANASHUHUDIA HOTUBA NI NZURI ? MHESHIMU MUNGU KWA MANENO NA VITENDO ! )

Kwanza iwe hotuba yenye matumaini na kutekelezeka
 
punguza chuki fuatilia vizuri!! mh kasema nyongeza pamoja na kupanda madaraja ni bajeti ijayo!! halafu unakuja kueneza chuki,hakuna kinachoweza kufanyika bila mipango!!
Angesema leo kuwa kuna ongezeko la mshahala utekelezaji wake ndiyo ungekuja bajeti ijayo. Sasa kama hayajasemwa sijui yatafanyikaje. Anyway ngoja tungoje kama usemavyo huenda mtateta pembeni
 
Kiukweli ni aibu kwa serikali yake kukosa mbinu kabisa ya kuboresha maslahi ya watumishi....Kasema anarudisha madaraja hayo madaraja sio kwamba ndo ameongeza mishahara ayo yapo kisheria kila baada ya miaka 4 unapanda daraja lingine,Kasema anarudisha Annual increment hii haina maana sana kwani ipo kisheria ila ongezeko lake lintegemea daraja lako la mishahara hivyo wapo watakao pata 18,000. 26,000/ na wengine hadi 34,000.....Hilo nalo hua lipo kisheria na linapaswa kufuatwa kwa kila mwaka kuongezewa....Tatizo kwa watumishi wengi wa Umma ni KODI na Kutopandishiwa Mishahara....Tulitegemea Rais aseme ameongeza 20% au 30% thats all.....na sio annual increment kwan 18,000 ni nini kwa sasa ni sawa na kilo 7 za Sembe tu hizo nazo ni za kuchekelea kweli?
 
  • Thanks
Reactions: BOD
Sherehe za May Mosi zimemalizika ,na kufana huko Kilimanjaro.Rais amesema kwa budget ya mwaka huu kutakuwa na annual increments ,Promotion kwa wafanyakazi na ajira mpya 52000.
 
Wafanyakazi hawakutaka hotuba nzuri bali walitarajia kusikia Rais akiwahakikishia kwamba maslahi yao yataboreshwa katika mwaka wa fedha 2017/18. Watumishi wameendelea kunyongea chini ya chama cha kitapeli (CCM)
 
Kwa kweli tuweke itikadi zetu pembeni. Mheshimiwa Rais ametoa hotuba nzuri sana kwa mustakabali wa taifa letu. Hotuba yake imejaa matumaini mazuri kwa Watanzania. Akiendelea na hotuba za namna hii taifa litakuwa moja. Tujitahidi kumshauri kwa busara na hekima ili tufike mbali. Toa pia pongezi zako kuumpa moyo Rais wetu
Kwanini uwalazimishe wengine kuunga mkono?
 
Kuzungumza masuala ya ndege kwenye siku kuu ya wafanyakazi ndio kutoa hotuba ya kihistoria?


Tukubali tu bado hatujapata Rais.

Na awamu hii tumekula gharasha!
Mkuu sio habari ya ndege tu, bali ameongea mambo mengi tu mazuri kama yakitekelezwa cha msingi tuzidi kumshauri kwa busara. Kwani hili taifa ni letu sote
 
Back
Top Bottom