Moshi: Yaliyojiri Mei Mosi 2017, Rais Magufuli amwaga ajira Elfu 52, madaraja kupanda....

Mkuu usiwe na mashaka nami huwa nasimamia ukweli. Ndio maana nimesema ni hotuba ambayo mheshimiwa hakuwa kichama bali amesimama kama Rais wa nchi. Tuwe wakweli ndugu
Sawa lakini hakuna jipya karudia yale yale ya wakati wa vyeti feki
 
Kuna watu uelewa wao mdogo mpaka unashangaa. Hivi maamuzi ya mwaka wa fedha mpya na maslahi ya watumishi kwa utamaduni wetu Tanzania hufanyika lini ?
Leo kama amesema tusubiri mwaka ujao inamaana si mwaka wa fedha wa 2017/18 bali ni 18/19.
Ikumbukwe kasema kwamba mwakani tukikutana wakati kama huu tutarajie mambo mazuri.
Hapa tusijifariji bajeti hii ya 2017/18 haongezi wala hapunguzi kitu.



maccm hayaelewi mshahara kuongezeka wasubiri 2019.
raisi akiongeza mshahara huwa haweki kimafumbo anafunguka na kiwango cha hela.
 
Wafanyakazi hawakutaka hotuba nzuri bali walitarajia kusikia Rais akiwahakikishia kwamba maslahi yao yataboreshwa katika mwaka wa fedha 2017/18. Watumishi wameendelea kunyongea chini ya chama cha kitapeli (CCM)
Lakini mbona nimesikia akisema kwamba mwaka huu, atapandisha madaraja na kuongeza mishahara ili maisha ya wafanyakazi yawe mazuri
 
Kwa kweli tuweke itikadi zetu pembeni. Mheshimiwa Rais ametoa hotuba nzuri sana kwa mustakabali wa taifa letu. Hotuba yake imejaa matumaini mazuri kwa Watanzania. Akiendelea na hotuba za namna hii taifa litakuwa moja. Tujitahidi kumshauri kwa busara na hekima ili tufike mbali. Toa pia pongezi zako kuumpa moyo Rais wetu
Lengo lako wewe si zuri hata kidogo. Huwezi kuwatafutia watz wenzako njia ya kushitakiwa kupitia sheria ya makosa ya Mtandao. Hotuba ya leo ilikuwa ni ya kujibu maswali tu ya vyama vya wafanyakazi, mambo muhimu juu ya wafanyakazi hayajatafutiwa ufumbuzi hata kidogo, mazungumzo yake mengi yalijikita kwenye kijibu maswali na kutoa ahadi tu.
 
Kwa kweli tuweke itikadi zetu pembeni. Mheshimiwa Rais ametoa hotuba nzuri sana kwa mustakabali wa taifa letu. Hotuba yake imejaa matumaini mazuri kwa Watanzania. Akiendelea na hotuba za namna hii taifa litakuwa moja. Tujitahidi kumshauri kwa busara na hekima ili tufike mbali. Toa pia pongezi zako kuumpa moyo Rais wetu
....we utakula hotuba!? Ni mda wa vitendo sio ahadi. Jamaa yetu yeye amachokisema na anachokitenda huwa ni tofauti, kauli zake nyingi zimejaa matumaini inapofika kufanyia kazi kauli zake masikitiko
 
Maskini Rais wetu, anatumia nguvu kubwa sana kuzinadi ndege na juhudi zake za miundombinu..Hata sehamu ambapo hazihusiki inabidi azitaje!

Zimechukua hela nyingi za wananchi, hivyo lazima anadi ili kila mwananchi aelewe.

Zaidi ya bilioni 400 kwa ndege moja sio jambo la mchezo....hiyo ni karibu nusu ya pato la Taifa kwa Mwezi.
 
Jamani kasema mambo yote yaliyofungwa yanafunguliwa mwaka kesho yani kuanzia mwez wa saba 2017/2018 msiende mbali kiasi hicho kama ww n mfanyakaz subir mwez wa saba in miez miwili tu bado kuanzia sasa msiwe na hasira kiasi hicho.
 
Kwakweli wananchi wengi wa hapa Moshi nimeona walivyomkubali...sisi waandishi wa habari tumeshangaa...tulidhani tupo Mwanza kumbe kwenye ngome ya Kaskazini. Kweli moto wa Magufuli hauzimwiiii hadi 2020
 
Hana msaada wowote kwa wafanyakazi kama yeye tu alishindwa kujipunguzia mshahara wake mnategemea atawajali nyinyi akina mwafulani ambao hambabaishi kwa makelele yenu
 
Back
Top Bottom