Moses Kulola, Askofu Mkuu wa Makanisa ya EAGT afariki dunia

Truly am very happy for this man of God. Ameifanya kazi yake na apumzike kwa amani. Kama tujuavyo amelala tutamwona tena. Kazi ipo kwetu mimi na wewe tutakuwaje siku yetu ikifika?
 
Mzee Ailey yatoa maisha yake toka wakati aw Juana hatamwisho kwaajili ya kumtumikia Mungu bila kutenda walk Kutamani Mali na kujilimbikizia ni Mfano aw kuitwa kwa viongozi aw Jamii Hassa watumishi aw Mungu .Kanisa la EAGT lime pasta pengo KUBWA

Ni matatizo ya keyboard au unatumia miwani isiyoendana na matatizo yako ya macho?
 
Ndugu acha uongo wa mchana kweupe, Mtumishi wa Mungu Askofu Kakobe mara nyingi amesema sana kuwa yeye ni mtoto wa kiroho wa Mtumishi wa Mungu Askofu Kulola. Mara kadhaa Askofu Kulola ameshaenda katika kanisa analolichunga Askofu Kakobe MWenge, moja kati ya hizo safari, Askofu Kakobe na washirika walimpa zawadi nyingi sana Askofu Kulola, ikiwa ni kuheshimu kazi kubwa ya Injili aliyoitenda Askofu Kulola. na hata katika ushuhuda wake Askofu Kakobe katika website yake hapa , http://bishopzacharykakobe.org/en/about-us/about-bishop-zachary-kakobe . utaona wazi wazi ameeleza kuhusu kuokoka kwake kutokana na mahubiri ya mtumishi wa Mungu, Askofu Kulola.
90
Hakika Mtumishi wa Mungu Askofu Kulola,amemaliza kazi na taji ya haki amevikwa. Jina la Bwana lihimidiwe

Bishop Zachary Kakobe is a Tanzanian national; born on Monday, June 6, 1955; in Kibondo, Tanzania. His spiritual journey began on Easter Sunday, April 6, 1980; when he was born again at a Miracle Healing Indoor Crusade, which was conducted by a renowned National Evangelist in Tanzania, Bishop Moses Kulola, at the Tanzania Assemblies of God Church, Ilala, Dar-Es-Salaam, pastored by Pastor Titus Mukama. In that evening, the Gospel message that was preached by Bishop Moses Kulola, made Zachary Kakobe to go forward to the pulpit, for salvation.
 
Arch Bishop Kulola ni kielelezo kizuri kwa Watumishi wa Mungu wa leo, Watu wa Mungu tuna mengi ya kujifunza kutoka kwake kama unyenyekevu na uadilifu. Hakupenda sifa, hakupenda vyeo na majina makubwa ya kutisha kama vile Nabii au Mtume kama wengi wanavyopenda kujulikana nyakati hizi.
 
Nimepokea taarifa kutoka kwa Rev. Daniel Kulola ambaye ni mtoto wa Bishop Moses Kulola kwamba, Askofu Kulola amefariki dunia muda mfupi uliopita.

Nitaendelea kuwapa updates.

Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina la bwana lihimidiwe.



RIP M S Kulola
 
Last edited by a moderator:
Rip askofu mzee moses kolowa. Poleni familia na waumini wote pamoja na watanzania wote
 
Kweli Mungu anawatu wake yani nijana nipo kitandan nasikiliza moja ya cd zake, kwakweli tumemkosa mtu wa thaman sana ktk ulimwengu huu. Ameyagusa maisha yangu na ninampenda sana mtumishi wa Mungu askofu Kulola. Kwangu nipengo kubwa nisijuwe vile litazibwa. Ila neno la Mungu umenifundisha sitolisahau nakuliweka hata siku tutakutana mji ule mtakatifu mbingun kwa Baba. Nitakukumbuka pale ukisisitizia neno kwakusema Yooo! Hallelujah. Dunia na ulimwengu wa watakatifu umempoteza mtu muhimu sana, najuwa. "Mungu ni Mungu mtakatifu" Askofu Kulola. Hallelujah mwendo umeumaliza nasasa yupo kwenye manshen yake kwa Baba anakula bata kaz kwetu tulio baki. Je tukaa ktk jumba amekaa Kulola? Neno lasema wale wanawaongoza watu kutenda mema watang'a milele na milele. Ask Kulola sasa amevishwa mwili utakao ng'aa milele namilele. Amina .
 
arch bishop kulola ni kielelezo kizuri kwa watumishi wa mungu wa leo, watu wa mungu tuna mengi ya kujifunza kutoka kwake kama unyenyekevu na uadilifu. Hakupenda sifa, hakupenda vyeo na majina makubwa ya kutisha kama vile nabii au mtume kama wengi wanavyopenda kujulikana nyakati hizi.

maneno mazito na ya ukweli kabisa haya....rip bishop kulola...mliopo eneo la tukio tupeni mwongozo..mazishi lini na wapi...nataka nikamsindikize bishop kwenye makao yake ya milele
 
Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu. Yeye huchanua kama vile ua, kisha hukatwa; Hukimbia kama vile kivuli, wala hakai kamwe. AYUBU 14: 1 - 2
Mzee wa UPAKO, Antony Lusekelo analifahamu fungu hili? Yeye huwa anadai kuwa hatakufa!
 
Mimi namkumbuka hasa wakati wa mahubiri yake pale TEMEKE alipokuwa anaendesha mikutano yake, nilikuwa nahudhuria na ilipelekea kupenda nyimbo za Injili hadi leo hii. Wakati nikiwa chuo nilikuwa nasoma huku nasikiliza nyimbo hizo na mambo yalikuwa yakipanda sana. Mahubiri yake yalijaa hekima sana na kweli hajawahi kujikweza kama mitume, manabii, na Maaskofu wakuu wa sasa.

Mwenyezi mungu awabariki familia na aweke roho yake mahali pema peponi
 
Pumuzika kwa amani Kulola, nayakumbuka mahubiri yako yalivyokuwa ya kutujenga na kututia moyo wakristo, hasa ulipohubiri habari za mpinga Kristo.....Je unapenda niseme.....je unapenda nikwambie.....! RIP
 
Askofu Kulola namchukulia kama mtumishi wa Mungu wa kweli. Ameanza kuhubiri injili miaka mingi sana, mimi binafsi nimeanza kumsikia kuanzia miaka ya 1980. Angekuwa na tamaa ya pesa, angekufa tajiri sana kuliko hawa tunaowaona.

Mtumishi Kulola, umepigana vita vema na umeshinda. Mungu akurehemu!
 
One of the best long serving and spiritual leader in tanzania and worldwide.alass our dear bishop.
 
Back
Top Bottom