Kuna siri gani ya mume kutangulia kufa?

gromyko

Member
Oct 21, 2023
64
87
Wanabodi napenda kuanza kwa kumshukuru Mungu kwa kutulinda na kutufikisha siku ya leo.

Pili nimepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu na Mbunge wa Monduli Laigwanan Edward Ngoyayi Lowasa kilichotokea tarehe 10/02/2024.Pia nimepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha ghafla cha aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa klabu ya Yanga wakili msomi Imani Madega ambaye naye amefariki tarehe moja na Lowasa.Bwana ametoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana lihimidiwe.

Baada ya kupokea taarifa za misiba hii mikubwa kwa taifa letu, binafsi nikawa nawaza kuhusu namna ambavyo wanaume ndio mara nyingi wanatangulia na kuwaacha wake zao. Nikajaribu kupitia orodha ya watu maarufu waliofariki na kuacha wake zao ikawa ni ndefu mno kwa kifupi naomba nitoe japo kwa uchache:-

1.Abeid Amani Karume(Mkewe yupo hadi leo)
2.Edward Moringe Sokoine
3. Aboud Jumbe Mwinyi
4. Mwalimu Nyerere
5. Ben Mkapa
6. JP Magufuli
7. Dr. Omary Ally Juma
8. Maalim Seif Sharifu Hamad
9. Bernard Camillius Membe
10.Kapten John Komba
11. Moses Nnauye
12. Jomo Kenyatta
Listi ni ndefu sana.Sina maana kwamba wanawake ndio watangulie ila kwetu kama wanadamu na waja wa Mwenyezi Mungu tunajifunza nini?
Nawasilisha.
 
Kifo ni siri ya Mungu,japo utapata majibu mengi tu hapa ila uhai wa Binadamu mpaka kufa kwake hupangwa na Mungu,

Hao uliowataja ni watu maarufu tu ndio maana tumewajua,swali lako lingependeza zaidi kama tungeweka orodha ya watanzania wote wajane ambao wamefiwa na waume zao.
 
za vijiweni ni kwamba wanasema wanaume hutumia nguvu nyingi kupambana na maisha na wanachakaa mapema. Kupiga ishu sana nako kunatajwa, pia wanasema wanawake wana ujazo na akiba ya chakula miilini mwao. Wanaendelea kusema mkifungiwa msipewe chakula na maji kwa muda mrefu atakayetangulia kufa ni mwanaume kwa kuwa hana nyama nyingi mwilini mwake. Wanasema makalio na mapaja ya mwanamke yana hazina nyingi ya mafuta na nyama za kutosha mpaka ziishe akondeane ni muda mrefu atakua ameishi
 
za vijiweni ni kwamba wanasema wanaume hutumia nguvu nyingi kupambana na maisha na wanachakaa mapema. Kupiga ishu sana nako kunatajwa, pia wanasema wanawake wana ujazo na akiba ya chakula miilini mwao. wanaendelea kusema mkifungiwa msipewe chakula na maji kwa muda mrefu atakayetangulia kufa ni mwanaume kwa kuwa hana nyama nyingi mwilini mwake. Wanasema makalio na mapaja ya mwanamke yana hazina nyingi ya mafuta na nyama za kutosha mpaka ziishe akondeane ni muda mrefu atakua ameishi
Ni kina nani hao wanaosema?
 
Kwa nini tusife mapema...

unnamed.jpg
unnamed-1.jpg


Cc: Mahondaw
 
Back
Top Bottom