More than serious nahitaji mume wandugu

jena

Member
Mar 6, 2011
17
21
Wana JF, mimi ni mwanadada na leo nimeona nijitoe muhanga kabisa maana ninahitaji mume/mchumba. Niko tayari kupokea kukosolewa ila kwa yule aliyeko kwenye shinda kama yangu tafadhali ni PM.

Mimi ni Mkristo ninayempenda Mungu na ninahofu ya Mungu ndani yangu, tayari niko kwenye umri wa kati ya 30-33 na ninahitaji mume wa kati ya 33 na kuendelea. Awe na elimu ya kujitosheleza, mfanyakazi au aliyejiajiri.

Kabila lolote Tanzania na pia awe Mkristo. Hili swala naomba tu mchukulie kwangu ni kitu halisi hapa sina utani na wala siko kwa ajili ya kumpotezea mtu muda. Na katika hili pia namshikirisha Mungu nikiamini mume/mke mwema anatoka kwa Bwana.

Na pia kwa wale watakao nishauri na kunitia moyo kwenye hili nawashukuru. Kaka zangu popote pale ulipo na unajiona kweli unahitaji mke naomba uni PM lakini kama ni swala la mzaha au kujaribisha naomba usipoteze muda.
 
karibu sana jukwaani dada Jena......nakuhakikishia hapa JF utapata mume mwema.....ila ujiandae kwa masihara lakini usikate tamaa....wapo walio single na wana heshima zao....nakutakia kila la kheri na Mungu akubariki katika jambo hili
 
Dah haya vijana wenzangu mie vigezo vimegoma!bibie anaonyesha hana zengwe!kuvutia zaidi weka plain CV!
 
Mimi niliku tayari uwe mke watatu nadini yangu inaruhusu kuo mwenye dini tofauti. lakini umesisitiza lazima mkristu. ukichenji maindi ni juzee hapa jkwani sio kule PM
 
Good Jena, you sound very clear and serious safi sana, nakuombea kwa mwenyezi upate mwenza roho yako itulie na utampata tu wala usikonde dada angu!
 
Wana JF, mimi ni mwanadada na leo nimeona nijitoe muhanga kabisa maana ninahitaji mume/mchumba. Niko tayari kupokea kukosolewa ila kwa yule aliyeko kwenye shinda kama yangu tafadhali ni PM.
Mimi ni Mkristo ninayempenda Mungu na ninahofu ya Mungu ndani yangu, tayari niko kwenye umri wa kati ya 30-33 na ninahitaji mume wa kati ya 33 na kuendelea. Awe na elimu ya kujitosheleza, mfanyakazi au aliyejiajiri. Kabila lolote Tanzania na pia awe Mkristo. Hili swala naomba tu mchukulie kwangu ni kitu halisi hapa sina utani na wala siko kwa ajili ya kumpotezea mtu muda. Na katika hili pia namshikirisha Mungu nikiamini mume/mke mwema anatoka kwa Bwana. Na pia kwa wale watakao nishauri na kunitia moyo kwenye hili nawashukuru. Kaka zangu popote pale ulipo na unajiona kweli unahitaji mke naomba uni PM lakini kama ni swala la mzaha au kujaribisha naomba usipoteze muda.

Mi nipo singo lakin hapo kwenye RED nimeshafeli, maana huo umri mi bado
 
Mimi niliku tayari uwe mke watatu nadini yangu inaruhusu kuo mwenye dini tofauti. lakini umesisitiza lazima mkristu. ukichenji maindi ni juzee hapa jkwani sio kule PM

Akuanzishie sredi au?
 
Muombe apunguze! Sijaona aliposema there is no room for negotiating!

Mmmmh! Ingekuwa bidhaa inauzwa ningesema apunguze, sasa hapo anazungumzia fyucha yake. Haina cha mapunguzo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom