Mohamed Mpakanjia is no more!

RIP Med Mpakanjia,Bwana ametoa na Bwana ametwaa,pole rafiki wa karibu wa Marehemu JB,pole ndugu, jamaa na marafiki...
 
Nilikuwa na maana ya kufunga lakini pia si taarifa sahihi na ndio maana nikasema, "wanasema" na kwamba, "kama ni kweli" basi Mungu aiweke Roho yake mahali pema peponi. Unajua kwa jinsi alivyojiweka tokea uhai wa Amina, kumekuwa na mambo mengi,baadhi yakiwa ni yale aliyoyapenda yatangazwe ama kuandikwa. Lakini sasa hivi hata jamaa zake wa karibu wanasema hawajui. Sujui maana yake nini hasa.

Halisi wewe unafaa kuwa mtunga riwaya maana unajuwa kuwa excite wasomaji,ebu fafanua zaidi bana...."Si taarifa sahihi, nikasema, wanasema, wanasema hawajui. Sijui...nini hasa"....RIP Mpakanjia.
 
Inna Lillahi wainna Illaihi Rajihunna.

Inshallah kama watazikia kwa mama yake temeke basi inshallah nitahudhuria maziko.
 
bwana Masanilo, Lisemwalo liko hivi (tena toka kwa wafanya kazi wenzie na liyumba); uhusiano wa Liyumba na Amina haukuwa wa siri kabisa

Safi kabisa. Amina alikuwa anaingia nyumbani kwa Liyumba makazi xxxxx kama nyumbani kwake!! Na huku akiwa ameolewa na Med!!! Haikuwa siri kwani hata kwenye gari walikuwa wanapanda wote wakati wanatoka huku wakivalia nguo almost same colour with luxury Liyumba's cars. Binafsi sikuweza kuamini kama binti yule mdogo umri sawa na Jennifer Liyumba bado haogopi hata wale mabinti wa Liyumba. This was a shame. Liyumba naye anaugulia keko!!!

Ndiyo maana wakati mwingine huwa napata hasira sana na hawa wanajiita celebrities kwa kufanya uovu tuu huku wakifahamu kuwa hawako salama na ni makusudi. After all na Med same same!! Hivyo walikutana vifaru kwa vifaru. Kisa pesa/utajiri ambao source ni questionable na ulimbwende wa kununua dukani. Pengine wakati ule hatukuwa tumepaa taarifa ya dawa za kuongeza hips, makalio, matiti na ku-firm uso na lots of destructive cosmetics.

Artificial life will be summarized by artificial death!!
 
bwana Masanilo, Lisemwalo liko hivi (tena toka kwa wafanya kazi wenzie na liyumba); uhusiano wa Liyumba na Amina haukuwa wa siri kabisa.. na ndo jamaaa alikwenda nae mpaka Dubai kati ya moja ya zile tripu zake za mwanzo za 'around the world in 80 dayz' ndo kujua kuwa Liyumba 'anagonga' si ndo akamsepesha

Du hebu tumuombeeni alale salama kwanza, mbona huu sasa utakuwa msiba mzito.
 
Mpwa Fidel80 hujawahi pitia moja ya viota vya Mpakanjia?


Mku Masanilo usianze kuulizia haya maana mishtuko ya moyo itakuwa mingi mno. Jua kuwa huu ni msiba wa wengi walio hai na ambao wameshatangulia mbele ya haki (kama kungekuwa na resurrection waje watambuane!!).

Wanadamu tuwe makini na maisha na maamuzi yetu. Maamuzi yako na yangu ndiyo yametupelekea kuwa jinsi tulivyo!!!
 
Hakuna mtu anaechekelea kifo hasa kisicho kuhusu unless huyo mtu kuulia mama yako au mtu wa karibu kwa kukusudia ingawa utapata tuu mixed feelings hapo, nasema hivo sbb naona ni vema tukiongelea hivi hizi tabua mbaya za kuambukiza au kutokuwa mtulivu enzi za uhai ili kila mtu ajifunze toka hapo,
tz kuna uchafu wa ngono mwingi sana na usipo kuwa mtu wa ngono unaonekana mshamba sana sasa kama hapa tunapigana vita ya mafisadi kwann tusipigani vita vya UKIMWI na hali unatumaliza???
huku mahospitalini hapafai, huko kinamwananyamala hospt ukienda hutaamini utayayo yaona utanyooka tabis tuu lzm, tuongelee kwa uwazi UKIMWI ili kuokoa maisha, ili kupigana na gonjwa hili

Nawakilisha
 
Mpakanjia huyu amechangia sana kuifilisi TRC ambayo leo ni TRL. Alikuwa ana tender ya ku-supply spare parts pale TRC, basi ilikuwa ni kujichotea tu pesa pale akishirikiana na baadhi ya mameneja na wahandisi pale TRC.

Anyway, apumzike kwa amani.
 
pumzika kwa amani Mpakanjia, naona sasa data ndio zamwagwa uwanjani, maana ukikaa vibaya nawe unajikuta humo
 
mzee Maana punguza hasira...hizi cheni hazikwepeki!!!

Mkuu Ochu zinakwepeka kama utaamua na ukadhamiria. Vinginevyo kama mtu hujafanya maamuzi jua siku moja utaingia ndani ya mduara tu ,it is like a vicious cirle!!! Ni kutafuta kila namna kujizuia kuingia ndani yake. Kama mpaka sasa hujainiga basi apa kuwa hutaingia kwa njia tulizozoea bali kwa bahati mbaya kama ajali ukikuta damu zimeingiliana, sindano, n.k. Vinginevyo stick to your relationship basi!!!! Je hii haiwezekani mkuu?? Tatizo kila bucha unataka ununue nyama, utayamaliza??

Inawezekana, play your part!! Na usisahamu kuzungumzia mambo haya hata ndani ya familia yako au yule mpendaye, iwe is always a sub-topic mnapokutana!!!

Rest in Peace Med wa Mpakanjia.
 
Mpakanjia huyu amechangia sana kuifilisi TRC ambayo leo ni TRL. Alikuwa ana tender ya ku-supply spare parts pale TRC, basi ilikuwa ni kujichotea tu pesa pale akishirikiana na baadhi ya mameneja na wahandisi pale TRC.

Anyway, apumzike kwa amani.
Aisee umenikumbusha... jamaa akajifanya ana garage basi gari zote za TRC eti zilikuwa zinaenda kufanyiwa service kwahiyo garage yake, na hasa 'utajiri' wa mpakanjia ndio ulipoanzia
 
3083838.jpg

Mohamed Mpakanjia

Nifahamishe.com
9/14/2009


MFANYABIASHARA maarufu na mdau mkubwa wa michezo na burudani nchini, Mohamed Mpakanjia amefariki dunia jana katika hospitali ya jeshi la Lugalo jijini Dar es Salaam ambako mkewe wa zamani Amina Chifupa alifariki. Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana katika hospitali hiyo ambayo pia alifikia aliyekuwa mkewe Amina Chifupa, Mpakanjia alifariki dunia katika hospitali hiyo majira ya saa saba mchana.

Chanzo cha habari cha Nifahamishe kilichopo katika hospitali hiyo kilisema kuwa mfanyabiashara huyo alifikishwa hopitalini hapo jumamosi iliyopita kutokana na kusumbuliwa na homa ya mapafu.

"Aliletwa hospitalini hapa jumamosi akisumbuliwa na matatizo ya homa ya mapafu. Wakati analetwa alionekana mwenye afya njema lakini hali yake ilibadilika ghafla leo na mauti kumfika," kilisema chanzo hicho cha habari.

Katika uhai wake Mpakanjia alikuwa ni miongoni mwa watu waliotoa mchango mkubwa katika maendeleo ya michezo na burudani hasa kutokana na kusaidia wasanii, wanamuziki na bendi nyingi za muziki hapa nchini.

Alikuwa mfadhili mkuu wa bendi ya DDC Mlimani Park 'Sikinde', Tanzania One Theater 'TOT Plus'.

Pia alidhamini albamu za pamoja za wanamuziki Ramadhani Masanja 'Banza Stone', Ally Choki na kiongozi wa Msondo iitwayo 'Sisi ndiyo Sisi' ya mwaka 2005.

Kwa upande wa sanaa alitoa mchango mkubwa kwa kuwasaidia wasanii wengi wa sanaa ya filamu na maigizo kwa kuwawezesha kifedha kukamilisha kazi zao hizo.

Mungu ailaze roho yake pema peponi.

AMEN


Source: Nifahamishe.com
 
Mpakanjia huyu amechangia sana kuifilisi TRC ambayo leo ni TRL. Alikuwa ana tender ya ku-supply spare parts pale TRC, basi ilikuwa ni kujichotea tu pesa pale akishirikiana na baadhi ya mameneja na wahandisi pale TRC.

Anyway, apumzike kwa amani.

Ndiyo maana mimi Maane ni Mchukia dhuluma na fisadi wa aina yoyote ile akifa sitalia hata kama ni ndugu yangu.

Hebu tizama jinsi gani watanzania wazalendo wale wa kipato cha chini, means of transport ni reli. Usafiri hakuna, wanalala station na watoto wadogo/wachanga/. Serikali wala haingilii kati kutaka wahindi walipe hata gharama za malazi maana wao ndiyo wamekuwa cause of the problem.

Hizi over expenditures na fake garages kama hizi ndizo zimechangia kuua shirika la reli na mengine kama hayo.
 
AISEE:mbona watu mnasita sita kutaja gonjwa lililomuua huyu mpaka njia?/?

NAWAPA DAKIKA SABA MTAJE GONJWA LA SIVYO MI NALITAJA MWENYEWE:

huyu mtu gani bana kila siku anafungaaaaaaa ndoa hata kama ni uhuni huuu wake umezidiii.
Nikitoka hapa nikirudi sitaki kumwona mtu kabaki ,semeni gonjwa
 
AISEE:mbona watu mnasita sita kutaja gonjwa lililomuua huyu mpaka njia?/?

NAWAPA DAKIKA SABA MTAJE GONJWA LA SIVYO MI NALITAJA MWENYEWE:

huyu mtu gani bana kila siku anafungaaaaaaa ndoa hata kama ni uhuni huuu wake umezidiii.
Nikitoka hapa nikirudi sitaki kumwona mtu kabaki ,semeni gonjwa

We kama unaujua si uutaje huo ugonjwa?
 
Back
Top Bottom