MOH kusomesha mtoto wa mkubwa UK ni uungwana?

Ndugu yangu haya ni maneno yako au? Nilidhani umejitambulisha hapo juu kuwa ni alumni wa MUCHS!

Hebu nitajie mwalimu mmoja tu pale muchs aliyekufundisha surgery, medicine, obs, psychiatry, paediatrics,
Ent, ophthalmology,...Kote huko awe yeye tu anakufundisha. Si ndio wanavyofanya mafundi bomba!

Hata kwenye specialisations kuna many subjects na kila moja linatakiwa mtu aliyebobea. Natumai umenipata.
kaa chini utulie na kuelewa mfano wa fundi bomba!
 
jamani muda mwingine tusiwe tunalalamika sana, hawa kwanza wengi ni waajiriwa chini ya hii wizara, halafu kama watu hawana admision za huko UK basi wawape tu scholarship? tuwe tunajishughulisha jamani , mbona yupo mmoja amepata toronto , canada hujamwongelea? Hata mimi mara ya kwanza nilikuwa na mentality kama yako kuwa aaaah ni watoto wa vigogo tu wanapata , siyo kweli niliwahi kujaribu na mimi nikapata tena UK. Tatizo ni kupata admision UK ndiyo tatizo , by the way masters yenyewe hapa UK ni mwaka mmoja tu.

Wengi ya hawa wanafunzi wanafamilia tayari hivyo muda mwingine kwenda mbali sana inawawia vigumu.

Nadhani hujaelewa vizuri anachojaribu kukisema mtoa mada hapa,,issue hapa sio kupata chuo UK,canada au USA,.suala la msingi ni wangapi ambao waliapply na wanastahili lakini wakanyimwa na badala yake kupewa hawa wasio na shida kabisa!?!

Usiwatetee hawa sababu hata mimi yaliwahi kunikuta,..nilipomaliza form six mwaka 2005 tuliapply scholarship za telecom&electronics za china pale wizara ya elimu ya juu.,.wametoa majina ya waliopata including waliokuwa na division III wakituacha sisi wenye div I,..na kulikuwa hakuna mwenye admission wala mean testing iliyokuwa imefanyika kujua hali zetu za kiuchumi,.rushwa tu.
 
nawe muda mwingine uwe unafikiria na kuchunguza kabla ya kuchangia. unahakika paediatric dentist inatolewa kwa mwaka mmoja?
una hakika ndio yeye tu aliyepata admission uk? hoja ilikua why kumfadhili mtoto wa mwenye uwezo wa kusomesha ,tena uk ambapo ni expensive sana,huku watanzania zaidi ya 100 wakikosa sponsor ktk vyuo vya ndani ya tz(waliopata admission ni zaid ya 200 na waliopata sponsor ni only 90).why asingesomeshwa muhimbili ambapo pia digree hiyo inatolewa?

Nadhani huna taarifa za kutosha , ni hivi home tution fee hapa UK ni kama poundi 3000 (kama million 7.5 za kibongo) na internationals ni poundi 10,000 inachofanya wizara ni kulipa home tution fee na inayozidi unajilipia mwenyewe . pale IMTU watu siwanalipa tution fee million 7? kuna tofauti gani mnayosema? mumewe anazo sasa kwa nini asimuongezee hizo poundi 7000 za juu? by the way kwa hiyo kozi tuition fee siyo gharama kama unavyosema unless angekuwa anasoma PhD ningekubali.

Acheni kuwwadanganya watu bwana huwezi kusomesha watu 200 kwa tuition fee ya mtu mmoja UK. Mathalani kama analipa tution fee ya poundi 10,000 kwa mwaka ni sawa na millioni kama 25 za kibongo na kama mtu anasoma pale chuo cha IMTU ambacho ni milioni 7 kwa mwaka , mbona inasomesha watu watatu (3) tu? hivi hesabu ndogo tu jamani zinawashinda? masters UK ni mwaka mmoja tu huku bongo ni miwili kwa mantiki hiyo aliyopo bongo atatumia millioni 14 hali wa UK millioni 25.
 
Hivi watu mbona hamjishughulishi kabla ya kuandika, soma link ya muhas nilotoa juu utaona wanafunzi watatu wamedahiliwa kwa paediatrics dentistry kusoma Muhas na hawajapata sponsorship ya wizara zaidi ya huyo Salma anaelipiwa UK. Wewe ndio mnafiki kwa sababu unatetea kitu usichokijua.

MUHIMBILI UNIVERSITY OF HEALTH AND ALLIED SCIENCES(MUHAS)
SELECTED APPLICANTS FOR POSTGRADUATE PROGRAMMES FOR ACADEMIC YEAR 2011/2012
................
119 Dr. MARO, Daniel Iskander M Tanzanian Paediatric Dentistry
120 Dr. KAWIA, Hassan Mohamed Idd M Tanzanian Paediatric Dentistry
121 Dr. MITURO, Twalha Hamisi M Tanzanian Paediatric Dentistry
Au hiyo ya UK ni special paediatrics dentistry?

Mleta mada wa awali, Takeurabu, kwa nini anapotosha mambo kwa kudai kwamba ''ninavyofahamu mimi pale MUHAS waliosomea peadiatric dentistry ni wawili tu! na hii kozi haitolewi hapa nchini, nafikiri Dr salama atakuwa amekidhi vigezo vya kuwa mhadhiri na ndio maana chuo kimem-recommend aende akasome nje ili aje kufundisha, otherwise katika hali ya kawaida watu huwa hawaombi kozi hii. nina uhakika katika kozi hiyo atakuwa ni yeye pekee aliyeomba ''. Naomba urejee ukurasa wa 87 wa prospectus ya MUHAS kwa mwaka 2012/13 panaposema ''We offer undergraduate and postgraduate studies in the field of restorative dentistry, oral and maxillofacial surgery, preventive and community dentistry, orthodontics and paediatric dentistry. '' Sasa nani ni mkweli, wewe au prospectus ya MUHAS, hapa mwenzako kapotolo kakuletea data.Kwa kuwa JF ni kijiwe cha great thinkers, let us practice kihivyo, please do your homework properly.
 
QUOTE=Pasco;2850733]Olecranon, nakuomba usiingie kwenye long list ya 'hate preachers' wa humu jamvini.
Kila Mtanzania kwanza ni Mtanzania ndipo mengine yote yanafuati ni jinsia gani, ni kabila gani, ni familia gani, ameolewa na nani etc. Kuwa mtoto wa rais, hakumuondolei haki yake kama Mtanzania mwingine yoyote.

Bahati nzuri au mbaya, nimetokea kumfahamu huyu binti, Dr. Salama na pia nawafahamu baadhi ya watoto wengine wa JK japo sio wote nane, kwa opinion yangu, kati ya watoto wote wa JK ninaowafahamu mimi, Dr. Salama pekee ndie anaesimama mwenyewe kama Salama bila ile pride ya mtoto wa rais ambayo nduguze wanayo!. She is so humble na down to earth, fortunately kaolewa na kijana mwenye uwezo kumlipia shule popote, lakini huko hakumuondolei right yake ya kupata fellowship kama rai mwingine yoyote. Hata kama unatoka familia ya mamilioneo, kupata fellowship kunakuongezea heshima kwa sababu ili kuipata lazima uishindanie na wengine toka nchi mbalimbali duniani. Wizara sio determinant nani anapata, sponsors ndio determinant, japo recomendation ya wizara pia inanguvu.

Kama huyo dr ana sifa, na ameomba kama Mtanzania mwingine yoyote, sasa ndio anyimwe eti kwa sababu ni mtoto wa rais?.

Wanabodi, tuendelee kumsakama JK kwa maroroso yake, ya chama cheke na serikali yake, au tuwasakame watoto wake wanaofanya wanayoyafanya simply kwa sababu baba ni rais, lakini nawaomba sana tusiisakame familia ya rais kwa mambo yasiyohusika, hiyo scholarship ni issue ya proffesionalism hata kama preferential ime play part lakini she deserves and she is capable!

Please leave her alone!.[/QUOTE]

Pasco;
Ha ha ha
Kweli natoa pongezi kwa walimu wetu huko mashuleni kwasababu inaonesha dhahiri walikuwa na kazi kweli ya kudeal na watu tulivyo na uelewa tofauti ivi.

Anyways,nadhani ishu ya msingi hapa ni wewe kwanza kuelewa kuwa scholarship (kwanza sio fellowship kama ulivyoziita) zinatolewa kuwa guaranteed kwa kiasi kikubwa na wizara yenyewe.kwa ivo hilo suala la kwamba ameshindana na nani aliye wapi duniani ni suala la kufikirika tu,huna hakika nalo.,unataka kuniambia yeye ndo mwenye akili kuliko hao madaktari wenzie wote!?

Ziada,una mahaba tu na huyo salama.suala la yeye kuwa humble ama arrogant halihusiani hata chembe na hii mada yetu...
 
Nilisoma mahali fulani mwanzoni kabisa majina hayo yalipotolewa, kwa upande wa Salama Kikwete iliandikwa anaenda kusomea "Orthodontics" ambayo nadhani ni Specialization kwenye dentistry.
 
Nadhani huna taarifa za kutosha , ni hivi home tution fee hapa UK ni kama poundi 3000 (kama million 7.5 za kibongo) na internationals ni poundi 10,000 inachofanya wizara ni kulipa home tution fee na inayozidi unajilipia mwenyewe . pale IMTU watu siwanalipa tution fee million 7? kuna tofauti gani mnayosema? mumewe anazo sasa kwa nini asimuongezee hizo poundi 7000 za juu? by the way kwa hiyo kozi tuition fee siyo gharama kama unavyosema unless angekuwa anasoma PhD ningekubali.

Acheni kuwwadanganya watu bwana huwezi kusomesha watu 200 kwa tuition fee ya mtu mmoja UK. Mathalani kama analipa tution fee ya poundi 10,000 kwa mwaka ni sawa na millioni kama 25 za kibongo na kama mtu anasoma pale chuo cha IMTU ambacho ni milioni 7 kwa mwaka , mbona inasomesha watu watatu (3) tu? hivi hesabu ndogo tu jamani zinawashinda? masters UK ni mwaka mmoja tu huku bongo ni miwili kwa mantiki hiyo aliyopo bongo atatumia millioni 14 hali wa UK millioni 25.

Master's Course kwenye dentistry specialization yoyote ni miaka miwili full-time kwa UK. Fees yake ni Pound sio chini ya 30,000 kwa mwaka, ina range kati ya Pound 30,000-35,000 kutegemea na chuo. Hii fee ni kwa Oversea students. EU/Uk wanalipa pound kati ya 9,000 hadi 12,000. Kwa hiyo ukijumlisha na gharama zingine kama usafiri, upkeep allowance, accomodation, insurance, vitabu, stationaries, dissertation publication, nguo kwa ajili ya baridi n.k. Gharama ya huyo Salama ni karibia pound ~50,000-60,000 kwa mwaka.
 
Ishu hapa ni nini hasa?
Je ni Salama kama mtoto wa Rais kupatiwa sponsorship, au ni kiasi cha pesa inayotumika kumsomesha Salama kwamba ni nyingi mno ingeweza kusomesha watanzania wengi ndani ya nchi. au ni kwanini Salama apewe sponsorship ilhali hajakidhi matakwa?

Kwa taarifa tu - Salama kama anakidhi matakwa au vigezo vya kumpa hiyo sponsorship ni haki yake kama ilivyo haki ya mtanzania mwingine yeyote na haijalishi anatoka familia yenye uwezo ama la. Aisbaguliwe kwa sababu ya nasaba yake. Ila kama umetokea upendeleo kwa vile yeye ni binti wa rais basi hapo ndio watu wapige kelele na kulalamika hadi kieleweke kama kitaeleweka.
 
Hapa mimi sikubaliani kabisa na Palalisote na wengine wa aina yake.kwanza siamini eti ni yeye pekee SALAMA kikwete kuwa ndo ameomba UK,tuachane na mambo ya siasa na ukada hapa.me mwenyewe ni kada mzuri wa chama cha mapinduzi na ndiyo maana napingana na hili kwani linashusha credit ya chama changu mimi kijana ambaye nini ndoto ya kuja kuwa kiongozi fulani kupitia chama changu,mbali ya uongozi nazungumza kama kada wa kawaida tu kuwa hili si sawa hata kidogo,mimi namfahamu vizuri mh Rais kuwa ni mtu mwenye hekima,huruma,busara na mpenda haki na mwadilifu lakini hawa watendaji wa wizara wanaongoza kujipendekeza kwa rais. Hata kama ni mtendaji wa wizara babake ana uwezo mkubwa wa kusomesha hadi kumaliza,tena mchangiaji mmoja amesema masters ni mwaka mmoja tu kwa hiyoo ndo kabissaaa ana uwezo huo na watoto wa wananchi wa kawaida wangepewa nafasi ile,acheni roho mbaya na ubinafsi nyinyi.
 
Hebu nisaidie wewe, kwa ninavyofahamu mimi, pamoja na mambo mengine hususani suala la uwezo wa mzazi...lingine la msingi ni academic standing; na more often than not, hii inakuwa ndiyo priority ya kwanza na zingine zinafuatia. sasa assume umebaki na majina mawili, salama kikwete na salama kintukute....salama kikwete ana second upper na kintukute ana second lower; je, scholarship ungempa nani hususani ukizingatia scholarship sio favor?!

I can't help on a hypothetical, weka vigezo walivyotumia MOH kupata hawa waliowachagua then tujadili kutokana na vigezo hivyo. Otherwise sina ninachofahamu kwa swali lako> Michakato halali huwa tunaiona kata UDSM wanapotoa vigezo vya admission kama cut off points, area of specialisation etc. Hawa MOH wametoa vague conclusion ambayo haitoa majibu bali inaongeza maswali.
 
jamani ktk kada ya afya kuna scholarship za kumwaga especially kwa post graduate.Za kina mama ndo usiseme maana hizo ziko nyingi mno.Hata ukitaka kwenda kusoma huko New Papua Guinea utapata sponsor tu hivyo hamna cha ajabu hapo.Huyo dada aliomba kama walivyoomba wengine hivyo tusilalamike tu bila kufanya uchunguzi

Criteria ya scholarship yoyote kigezo kikubwa huwa ni uwezo wa mwombaji ki-uchumi na ki-elimu. Scholarship zinalenga kusaidia wasio na uwezo wa kupata elimu kwa kukosa uwezo wa kifedha ingawa uwezo wa ki-elimu wanao. Hata kama ni nyingi kama unavyodai lakini hawatoi tu kama njugu bila kuwepo vigezo. Mtu anayezungumzwa je hana uwezo wa ki-uchumi?. Pia ukiangalia orodha utaona pia kwamba Taaluma anayokwenda kusoma UK inatolewa pia MUHAS na kuna watu kadhaa ambao wamepelekwa MUHAS na Wizara kwa ajili ya taaluma hiyo.
 
naona umeongea kihisia zaidi labda kwa vile unamfahamu huyu binti.
hapa hajalaumiwa baba mtu tena kuna mdau ameshauri wizara imuombe msamaha
baba yake salama kwa "uzembe" uliofanyika hapa, sasa chuki kwa familia ya kikwete ipo wapi hapa?

hapa suala ni dhana kwamba wizara ingeweza kusomesha wataalamu wengi zaidi
hapa nchini kama dk. salama angesomeshwa hapa nchini. je wizara inayosababu ya
ziada ya kuamuja kumsomesha dk. salama uk?

Olecranon, nakuomba usiingie kwenye long list ya 'hate preachers' wa humu jamvini.
Kila Mtanzania kwanza ni Mtanzania ndipo mengine yote yanafuati ni jinsia gani, ni kabila gani, ni familia gani, ameolewa na nani etc. Kuwa mtoto wa rais, hakumuondolei haki yake kama Mtanzania mwingine yoyote.

Bahati nzuri au mbaya, nimetokea kumfahamu huyu binti, Dr. Salama na pia nawafahamu baadhi ya watoto wengine wa JK japo sio wote nane, kwa opinion yangu, kati ya watoto wote wa JK ninaowafahamu mimi, Dr. Salama pekee ndie anaesimama mwenyewe kama Salama bila ile pride ya mtoto wa rais ambayo nduguze wanayo!. She is so humble na down to earth, fortunately kaolewa na kijana mwenye uwezo kumlipia shule popote, lakini huko hakumuondolei right yake ya kupata fellowship kama rai mwingine yoyote. Hata kama unatoka familia ya mamilioneo, kupata fellowship kunakuongezea heshima kwa sababu ili kuipata lazima uishindanie na wengine toka nchi mbalimbali duniani. Wizara sio determinant nani anapata, sponsors ndio determinant, japo recomendation ya wizara pia inanguvu.

Kama huyo dr ana sifa, na ameomba kama Mtanzania mwingine yoyote, sasa ndio anyimwe eti kwa sababu ni mtoto wa rais?.

Wanabodi, tuendelee kumsakama JK kwa maroroso yake, ya chama cheke na serikali yake, au tuwasakame watoto wake wanaofanya wanayoyafanya simply kwa sababu baba ni rais, lakini nawaomba sana tusiisakame familia ya rais kwa mambo yasiyohusika, hiyo scholarship ni issue ya proffesionalism hata kama preferential ime play part lakini she deserves and she is capable!

Please leave her alone!.
 
Bottom line Kapotolo ana hoja ya msingi kwa watendaji wa wizara.

Kama nimekuelewa vyema Dr. Salama angeweza kabisa kusomeshwa na private sources of finance.

Na hivyo wataalam wengine wangepata nafasi ya hizo funds zilizokua tied kwa kumsomesha Dr Salama U.K.

Ila chondechonde tutakizika MUHAS miaka si mingi kama chuo kinachotoa madaktari walioiva vyema kifani.

Mjadala mwema!
Wakuu kuna jambo hapa la kujifunza wana JF. Haswa ukifuatilia sana mtiririko wa mjadala huu mpaka Alwatan kuja kuelewa somo utaona kuwa wakati mwingine humu mijadala inaporomoka zaidi kwa hisia tena mara nyingi ni hisia zenye mielekeo fulani mbayo watanzania tusingestahili kuziendeleza.
Nampongeza sana Kapotolo kwa uvumilivu wake ameendelea kuwa mvumilivu na kujieleza bila jazba mpaka ikaeleweka. Asante sana kwa hilo Mkuu.
Lakini kusema kweli mada hii kuanzia pale mwanzo kama msomaji unapenda kuangalia mambo taratibu bila hisia huhitaji facts nyingi sana kuona kuwa kuna haja ya kutumika busara zaidi kwenye kufanya maamuzi kama haya. Tatizo la Tanzania siyo umaskini wa kiuchumi zaidi bali busara na utaalamu na kuacha kutukuza siasa tena za kijinga!
 
Afadhali umenielewa Alwatan. Salama Kikwete tafadhali tunakuelewa hupendi makuu, kataa sponsorship ya wizara na hizo pesa zisomeshe wenzako watatu hapo MUHAS hata kama alwatan ameita chuo cha kata.
Nadhani angeshauriwa akatae hiyo scholarship, lakini afanye juu chini aende akachukue hiyo course kwa kutumia 'private means' siyo pesa za hii serikali iliyo hoi namna hii. Kama kweli Mume anauwezo na Baba yake tunajua anao uwezo hao ndiyo wachangie aende akatuletee utaalamu. Hata sisi tunasomesha watoto wetu kwa kujinyima hivyo hivyo. Ila isjeikawa tunapinga yeye kupewa scholarship ya halali mara usanii ukafanyika matokeo yake mzee akaandika kimemo, it could be worse! Wewe na mimi tukajikuta tunachangia sana tu.
 
Ahsante Kapotolo na wengine ukweli unabaki kuwa:

-Kozi ya Paediatric dentsistry inafundishwa MUHAS
-Kozi ya Paediatric dentistry ni ghali zaidi UK kuliko Tanzania
-Muda wa kozi zote kwa nchi zote (UK na Tanzania) unakaribiana kama sio kufanana
-Kati ya madaktari wa kinywa (DDS) watatu walioomba kozi ya Paediatric dentistry MUHAS ni wawili tu wamepata 'sponsorship'
-Kwa gharama alizolipiwa/atakazolipiwa Dr. Salama zingetosha kusomesha idadi kubwa zaidi ya wanafunzi wa kozi hiyo au nyingine hapa nchini
-Na kati ya wanafunzi takribani 200 wa kada mbalilmbali za afya waliopata 'admission' vyuo mbalimbali nchini kwa kozi mbalimbali, ni wanafunzi 90 tu ndio wamepata 'sponsorship' ya wizara (MOHSW)
-Mh. Rais ana alternatives (binafsi na za watu wa karibu wa taasisi za ndani na nje ya nchi zisizo na 'ties' zozote kama za 'suti za mwarabu wa Kempinski'!) za kuweza kumsomesha mwanae ndani au nje ya nchi.
-Haikua busara kutumia 'resources' kidogo zilizopo katika mgawanyo uliofanywa na wizara (ama kwa shinikizo au kujipendekeza!)
-Busara hii ingetumika kwa mtoto yeyote ambaye anaenda kusoma kozi yeyote inayofundishwa nyumbani haswa mwaka huu ambapo wizara inasema haina fedha.Ninamaanisha kozi kama OT na Internal Medicine (Nizhyn-nadhani Russia,ENT-Singapore na Surgery-Nairobi ambapo mtoto wa Mkurugenzi wa Bima ya Afya-NHIF naye ameenda kusoma!)
-Ukweli huu utabaki kuwa ukweli, kama hauingii kapumzike ukirudi soma tena kuanzia juu!! Mapenzi kwa Dr. Salama (kwa kuwa 'humble' na kusoma digrii ya kwanza hapa nchini) au familia ya Rais hayabadilishi ukweli huu.
 
Olecranon, nakuomba usiingie kwenye long list ya 'hate preachers' wa humu jamvini.
Kila Mtanzania kwanza ni Mtanzania ndipo mengine yote yanafuati ni jinsia gani, ni kabila gani, ni familia gani, ameolewa na nani etc. Kuwa mtoto wa rais, hakumuondolei haki yake kama Mtanzania mwingine yoyote.

Bahati nzuri au mbaya, nimetokea kumfahamu huyu binti, Dr. Salama na pia nawafahamu baadhi ya watoto wengine wa JK japo sio wote nane, kwa opinion yangu, kati ya watoto wote wa JK ninaowafahamu mimi, Dr. Salama pekee ndie anaesimama mwenyewe kama Salama bila ile pride ya mtoto wa rais ambayo nduguze wanayo!. She is so humble na down to earth, fortunately kaolewa na kijana mwenye uwezo kumlipia shule popote, lakini huko hakumuondolei right yake ya kupata fellowship kama rai mwingine yoyote. Hata kama unatoka familia ya mamilioneo, kupata fellowship kunakuongezea heshima kwa sababu ili kuipata lazima uishindanie na wengine toka nchi mbalimbali duniani. Wizara sio determinant nani anapata, sponsors ndio determinant, japo recomendation ya wizara pia inanguvu.

Kama huyo dr ana sifa, na ameomba kama Mtanzania mwingine yoyote, sasa ndio anyimwe eti kwa sababu ni mtoto wa rais?.

Wanabodi, tuendelee kumsakama JK kwa maroroso yake, ya chama cheke na serikali yake, au tuwasakame watoto wake wanaofanya wanayoyafanya simply kwa sababu baba ni rais, lakini nawaomba sana tusiisakame familia ya rais kwa mambo yasiyohusika, hiyo scholarship ni issue ya proffesionalism hata kama preferential ime play part lakini she deserves and she is capable!

Please leave her alone!.

Pasco, heshima mbele,

Nashawishika kukubaliana na wewe lakini vile vile nasema hapana. Kwa sababu zifuatazo.

1. Yes Dr. Salama ni mtanzania kama wengine na ana haki kama mtanzania yeyote. I fully agree with you.
2.Ana haki ya kuomba fellowship kama mtanzania mwingine yeyote. Yes. Halina ubishi hilo.

Sasa kwa nini napingana na hoja yako au nakubaliana na mleta mada? Hapa we are dealing with public money. Tax Payers money (hata kama ni outside scholarship ambazo zimetolewa kwa Tanzania). Ni serikali ya JK hii hii ambayo imeweka vigezo vya kupata mkopo wa elimu ya juu. na watoto wengi wamenyimwa mkopo kwa kigezo cha wazazi wao...upo? Sasa kama tunaangalia uwezo wa mzazi..let this index apply across the board maana na JK ni mzazi! Unataka kuniambia kwamba JK hana uwezo wa kumsomesha mtoto/watoto wake?

Jamani hakuna anaye-mu-attack Dr. Salama, ila tunajaribu kuonyesha kwamba hizi double standards hazifai. Kama kila anayefaulu angekuwa anaomba mkopo bodi (grades zake ndo zinaongea) kabisa nisingekuwa na shida na watoto wa wakubwa kupewa scholarship za kwenda kokote...after all wengine ni hard working na wana grades nzuri tuu. Tatizo ni pale wakubwa wanapotaka kuweka vigezo kwa watoto wa wakulima kama sisi..wakati wao wanawekeana vigezo vyao...thats the only problem I have.

Alternatively, kama Dr. Salama angeomba scholarship independently, hakuna ambaye angemsumbua au kumsema hata angekwenda wapi. Kinachosumbua hapa ni public money ambazo tunaambiwa zinatolewa kwa vigezo. Maana anaenda UK kwa mgongo wa wizara ambayo ni kodi zetu. Unanipata kaka?

Otherwise, naungana na wengine, kama wizara ingekuwa na watu wenye akili ambao hawafikirii namna ya kupewa favor na mkulu, hakika huyu binti wasingeweka jina lake hapa. Na by the way yeye pekee yake ndo anakwenda UK! what measure have they used? mimi sijui..maana scholarship za serikali niliachana nazo baada ya mlimani! (of which sasa nalipa deni langu la mkopo).
 
Olecranon, nakuomba usiingie kwenye long list ya 'hate preachers' wa humu jamvini.
Kila Mtanzania kwanza ni Mtanzania ndipo mengine yote yanafuati ni jinsia gani, ni kabila gani, ni familia gani, ameolewa na nani etc. Kuwa mtoto wa rais, hakumuondolei haki yake kama Mtanzania mwingine yoyote.

Bahati nzuri au mbaya, nimetokea kumfahamu huyu binti, Dr. Salama na pia nawafahamu baadhi ya watoto wengine wa JK japo sio wote nane, kwa opinion yangu, kati ya watoto wote wa JK ninaowafahamu mimi, Dr. Salama pekee ndie anaesimama mwenyewe kama Salama bila ile pride ya mtoto wa rais ambayo nduguze wanayo!. She is so humble na down to earth, fortunately kaolewa na kijana mwenye uwezo kumlipia shule popote, lakini huko hakumuondolei right yake ya kupata fellowship kama rai mwingine yoyote. Hata kama unatoka familia ya mamilioneo, kupata fellowship kunakuongezea heshima kwa sababu ili kuipata lazima uishindanie na wengine toka nchi mbalimbali duniani. Wizara sio determinant nani anapata, sponsors ndio determinant, japo recomendation ya wizara pia inanguvu.

Kama huyo dr ana sifa, na ameomba kama Mtanzania mwingine yoyote, sasa ndio anyimwe eti kwa sababu ni mtoto wa rais?.

Wanabodi, tuendelee kumsakama JK kwa maroroso yake, ya chama cheke na serikali yake, au tuwasakame watoto wake wanaofanya wanayoyafanya simply kwa sababu baba ni rais, lakini nawaomba sana tusiisakame familia ya rais kwa mambo yasiyohusika, hiyo scholarship ni issue ya proffesionalism hata kama preferential ime play part lakini she deserves and she is capable!

Please leave her alone!.
"Chloroquine ni chungu lakini ni dawa"
Mie sikubaliani na huu utaratibu wa watoto wa Viongozi kuomba mikopo.Ni kama ilivyo Loan Board.Wanatakiwa wapewe kipaumbele wale ambao wazazi wao hawana uwezo.Huyo mtoto hata kama anasimama kwa miguu yake,suala la Elimu angemuomba baba yake hela na siyo Kuwabania wengine ambao hawana alternative.yeye ana option ya kulipiwa na baba yake hata angemuombea wafadhili toka nje.Hapa kisha tupunguzia nafasi ya msomi mmoja kama yeye angeachia.:eyebrows:
 
Olecranon, nakuomba usiingie kwenye long list ya 'hate preachers' wa humu jamvini.
Kila Mtanzania kwanza ni Mtanzania ndipo mengine yote yanafuati ni jinsia gani, ni kabila gani, ni familia gani, ameolewa na nani etc. Kuwa mtoto wa rais, hakumuondolei haki yake kama Mtanzania mwingine yoyote.

Bahati nzuri au mbaya, nimetokea kumfahamu huyu binti, Dr. Salama na pia nawafahamu baadhi ya watoto wengine wa JK japo sio wote nane, kwa opinion yangu, kati ya watoto wote wa JK ninaowafahamu mimi, Dr. Salama pekee ndie anaesimama mwenyewe kama Salama bila ile pride ya mtoto wa rais ambayo nduguze wanayo!. She is so humble na down to earth, fortunately kaolewa na kijana mwenye uwezo kumlipia shule popote, lakini huko hakumuondolei right yake ya kupata fellowship kama rai mwingine yoyote. Hata kama unatoka familia ya mamilioneo, kupata fellowship kunakuongezea heshima kwa sababu ili kuipata lazima uishindanie na wengine toka nchi mbalimbali duniani. Wizara sio determinant nani anapata, sponsors ndio determinant, japo recomendation ya wizara pia inanguvu.

Kama huyo dr ana sifa, na ameomba kama Mtanzania mwingine yoyote, sasa ndio anyimwe eti kwa sababu ni mtoto wa rais?.

Wanabodi, tuendelee kumsakama JK kwa maroroso yake, ya chama cheke na serikali yake, au tuwasakame watoto wake wanaofanya wanayoyafanya simply kwa sababu baba ni rais, lakini nawaomba sana tusiisakame familia ya rais kwa mambo yasiyohusika, hiyo scholarship ni issue ya proffesionalism hata kama preferential ime play part lakini she deserves and she is capable!

Please leave her alone!.

Tatizo sio salama kama salama ila nafasi aliyo nayo mzazi wake! Hivi uilshawahi kujiuliza kwa nini coca-cola bottlers au pepsi wakiwa na promotion wanatoa note kuwa wafanyakazi na familia zao hawaruhusiwa kushiriki?! Na hata wakishiriki, hawatapewa zawadi pindi tu status yao itakapojulikana?!

Its a matter of common sense (ethics), integrity and understanding what conflict of interest means!
(Mambo ambayo wengi wetu tulishayazika)!
 
jamani muda mwingine tusiwe tunalalamika sana, hawa kwanza wengi ni waajiriwa chini ya hii wizara, halafu kama watu hawana admision za huko UK basi wawape tu scholarship? tuwe tunajishughulisha jamani , mbona yupo mmoja amepata toronto , canada hujamwongelea? Hata mimi mara ya kwanza nilikuwa na mentality kama yako kuwa aaaah ni watoto wa vigogo tu wanapata , siyo kweli niliwahi kujaribu na mimi nikapata tena UK. Tatizo ni kupata admision UK ndiyo tatizo , by the way masters yenyewe hapa UK ni mwaka mmoja tu.

nimekusoma lakini ninashindwa kukuelewa!!
Sidhani kama umeelewa mtoa maada alikuwa anamaanisha nini in any case I'll try my level best to "show you the light"
Starting with, do you know the difference between LEGAL and LEGITIMATE (and if you like OPPORTUNE)???
For someone who by any chance (as you claimed!!!) got the oppotunity of studying in developed country should know that OLECRANON brought here regarding the Ms Kikwete is completely and totally inopportune - it might be LEGAL but it's not LEGITIMATE. In country where the corruption reigns, where meritocracy is not even part of the vocabulary if you want to avoid any kind of suspect whatsover, then you should provide the full list of all applicants,their curricula,the requirements needed for that post ecc - if it happens to be that the Dentist(Ms.Kikwete) fulfils both financial(scholarships are ormally provided to those who can not afford the tuition fee by themselves!!!) and meritocratic requirements then I'll be the very first to send my congratulations to her - till then it's nothing but business as usual - that family seems to be from the vampire genealogical tree, it keeps on sucking our blood!!!

Hiyo pia ni njia mojawapo ya WIZI!!!! Sipendi kutumia neno FISADI maana from my point of view naona linapunguza makali ya maana halisi ya matendo wanayofanya ambayo ni WIZI!!!!

Back
Top Bottom