Tatizo sio salama kama salama ila nafasi aliyo nayo mzazi wake! Hivi uilshawahi kujiuliza kwa nini coca-cola bottlers au pepsi wakiwa na promotion wanatoa note kuwa wafanyakazi na familia zao hawaruhusiwa kushiriki?! Na hata wakishiriki, hawatapewa zawadi pindi tu status yao itakapojulikana?!
Its a matter of common sense (ethics), integrity and understanding what conflict of interest means!
(Mambo ambayo wengi wetu tulishayazika)!
Asante Mkuu kwa mchango huu, the problem here is ethics and conflict of interests! Hakuna lingine lingesababisha upuuzi kama huu kutokea. Kuna mtu anangoja cheo baada ya hilo!
Kwanza kama nchi yetu ingekuwa inaongozwa na viongozi wenye busara na wazalendo wa kweli ingukuwa marufuku kwa mtoto wa kiongozi yeyote kwenda kusoma nje! Kuruhusu hilo ndio sababu ya wao kusahau kuboresha elimu hapa nchini. Tena ingetakiwa hata mfanya biashara anayempeleka mwanaye nje wakati elimu hiyo inapatikana nchini awe anatozwa kodi ya ziada!
Waliosema kuna viongozi wameifanya nchi kuwa shamba la bibi, hawajakosea hata kidogo.
haaaa! Inasikitisha kuona viongozi waroho namna hii madarakani. Inakuwa kama tunaongozwa na genge la wacheza kamari!