Licking Wounds
JF-Expert Member
- Nov 28, 2014
- 3,800
- 4,851
Unique Flower soma hapaHilo mbona lishajadiliwa sana humu na watu wakaliweka sawa.
Hii post ni ya kwenye moja ya hizo thread iliwekwa na mtaalamu Chief-Mkwawa
Hizi ni data chache ambazo zinaweza kukufumbua macho
1. asilimia 5 ya wafanyakazi wote waliopo kwenye formal sector Tanzania ni waajiriwa wa metl, kwa lugha nyengine katika kila watu 20 walioajiriwa kwenye formal sector mmoja ni metl
2. mo ameajiri watu 24,000
3. metl ipo nchi 12 Africa na ipo pia nje ya Africa nchi chache
4. asilimia 3.5 ya pato la taifa linatokana na mo
so hizi ni baadhi ya comparison za mo na bakhresa
-mo wafanyakazi around 24,000 bakhresa around 8,000
-metl nchi 12 na azam nchi 8
-metl pato 1.5 billion na azam pato 800 million
hizo data zote nimetoa about pages ya website zao.
Azam Worldwide - Azam Bakhresa Group
About Us | MeTL
kifupi mkuu mo ana hela kuliko bakhresa na wala hawalingani, maana amemzidi zaidi ya mara mbili.
watu wanashindwa kuamini sababu Bakhresa vitu vyake vyote vipo kwenye brand moja ya azam, ila mo ana viwanda na brand na biashara nyingi sana.
Mo kama mzalishaji
mafuta ya nyumbani
-mafuta maisha
-mafuta safi
-blueband mo margarine
-mafuta mpishi
-mafuta sunflower
vinywaji
-maji ya maisha
-maji masafi
-juice za pride
-soda za mo
nguo
-hakuna kampuni kubwa ya nguo kusini mwa jangwa la sahara kushinda metl. wana viwanda karibia kila mkoa wakitengeneza bidhaa za kanga na vitenge.
Vyakula
-unga wa ngano
-sukari
-korosho (mo cashew)
baiskeli
hapa kuna baisikeli za kawaida na za miguu mitatu za NABICO
mafuta ya magari
kampuni ya mo ya star oil ni moja ya wasambazaji wakubwa wa mafuta. uwezo wa lita milioni 5 kwa siku.
sabuni
-sabuni za royal
-sabuni za taifa
-sabuni za poa
mo kama mfanya biashara anaeagiza vitu nje
-agent wa LG tanzania analeta vitu kama mashine za kufulia, oven, mafridge na bidhaa nyengine za lg
-Agent wa TCL tanzania na TV zake
-analeta mitumba ya nguo
-AC za airlux
-battery za remote
-tractor za kulimia
-na mengine mengi kama big G, biscuit, tambi etc
mo kama muuzaji vitu nje ya nchi
jamaa anauza vitu vingi sana nje ya nchi kama
-katani
-korosho
-mbao
-nta
-choroko
-bidhaa nyengine tulizozitaja juu.
angalia hio diversity then compare na bakhresa.
Kati ya Mo Dewji na Bakhresa nani tajiri?
Hawa matajiri nani kamzidi mwenzake? Kuna ubishi unaendelea mahali,lakini naona kama Bakhresa kamzidi Mo kila kitu.www.jamiiforums.com