MO Dewji anawazidi vipi utajiri Bakhresa na Rostam Aziz?

Hilo mbona lishajadiliwa sana humu na watu wakaliweka sawa.

Hii post ni ya kwenye moja ya hizo thread iliwekwa na mtaalamu Chief-Mkwawa

Hizi ni data chache ambazo zinaweza kukufumbua macho
1. asilimia 5 ya wafanyakazi wote waliopo kwenye formal sector Tanzania ni waajiriwa wa metl, kwa lugha nyengine katika kila watu 20 walioajiriwa kwenye formal sector mmoja ni metl

2. mo ameajiri watu 24,000

3. metl ipo nchi 12 Africa na ipo pia nje ya Africa nchi chache

4. asilimia 3.5 ya pato la taifa linatokana na mo

so hizi ni baadhi ya comparison za mo na bakhresa

-mo wafanyakazi around 24,000 bakhresa around 8,000
-metl nchi 12 na azam nchi 8
-metl pato 1.5 billion na azam pato 800 million

hizo data zote nimetoa about pages ya website zao.
Azam Worldwide - Azam Bakhresa Group
About Us | MeTL

kifupi mkuu mo ana hela kuliko bakhresa na wala hawalingani, maana amemzidi zaidi ya mara mbili.

watu wanashindwa kuamini sababu Bakhresa vitu vyake vyote vipo kwenye brand moja ya azam, ila mo ana viwanda na brand na biashara nyingi sana.

Mo kama mzalishaji
mafuta ya nyumbani
-mafuta maisha
-mafuta safi
-blueband mo margarine
-mafuta mpishi
-mafuta sunflower

vinywaji
-maji ya maisha
-maji masafi
-juice za pride
-soda za mo

nguo
-hakuna kampuni kubwa ya nguo kusini mwa jangwa la sahara kushinda metl. wana viwanda karibia kila mkoa wakitengeneza bidhaa za kanga na vitenge.

Vyakula
-unga wa ngano
-sukari
-korosho (mo cashew)

baiskeli
hapa kuna baisikeli za kawaida na za miguu mitatu za NABICO

mafuta ya magari
kampuni ya mo ya star oil ni moja ya wasambazaji wakubwa wa mafuta. uwezo wa lita milioni 5 kwa siku.

sabuni
-sabuni za royal
-sabuni za taifa
-sabuni za poa

mo kama mfanya biashara anaeagiza vitu nje
-agent wa LG tanzania analeta vitu kama mashine za kufulia, oven, mafridge na bidhaa nyengine za lg
-Agent wa TCL tanzania na TV zake
-analeta mitumba ya nguo
-AC za airlux
-battery za remote
-tractor za kulimia
-na mengine mengi kama big G, biscuit, tambi etc

mo kama muuzaji vitu nje ya nchi
jamaa anauza vitu vingi sana nje ya nchi kama
-katani
-korosho
-mbao
-nta
-choroko
-bidhaa nyengine tulizozitaja juu.

angalia hio diversity then compare na bakhresa.

Unique Flower soma hapa
 
Ana ela kweli ila kaachwa mbali sana na mo, rostam ana $900bl mo ana $1.5tr kama nmekosea mtanisahihisha....

Inawezekana ana ela kumzidi mo lkn anaficha baadhi ya mali na ac zake zisijulikane
Hivi billion 900 Tena US dollar unaijua vizuri, Yani mo awe na 1.5Tr us dolar😁😂 elimu inahitajika kwa kweli
 
Ana ela kweli ila kaachwa mbali sana na mo, rostam ana $900bl mo ana $1.5tr kama nmekosea mtanisahihisha....

Inawezekana ana ela kumzidi mo lkn anaficha baadhi ya mali na ac zake zisijulikane
Alama ya $ unajua maana yake lkn? Maana tajiri wa Microsoft enyewe Hana hata 250bilion dollars
 
Tajiri gani viwanda vyake vichafu na vimechoka, magari mengi mabovu na wafanyakazi wake wengi wana hali duni kimaisha.
nilipata kuingia kiwanda chake East Coast Oil/Fats Kurasini, hali ni tete, kuchafu mno, kupo sagalabagala, vehicles zimechoka kinoma

injinia makeniko anakunja 300k basic/month, technician makeniko anakunja 180k basic / month
 
Huyu jamaa utajiri wake wa magumashi na kiwanda cha juice eti ndo tajiri namba moja.

Ukija kwa Bakhressa
Ana meli, ngano soda kiwanda cha sukari chenyd thamani ya 600 bilions
Azam tv, Azam pesa.

Rostam aziz anayemiliki kampuni ya ndege, caspian tigo Tanzania Taifa gas inakuwaje tunaambiwa huyu mbabaishaji eti ndo tajiri wa tz ama anafanya ubabaifu aonekane hivo.
Alfu nyongeza yake mishaara wake sasa kwa wafanyakazi wake Ni tabu tupi so ajabu afsa mwenye elimu kubwa akmlipa laki nne au tatu
 
Dukani kwangu.

AZAM- Ngano, Azam energy, Azam embe

MO-Mo extra, mo Tambi, mo poa bar soap, mo poa detergent, Mo taifa bar soap, Mo power betery, Mo malta, mo chocolate biscuit, Mo 29, Mo halisi.
Safi mafuta(Dumu, Ndoo kubwa na ndogo), Mo Viberiti, Mo Protector, Mo Beauty na Aloevera, pia wakala wa sukari zote(Sukari pakti, 25kg, 50kg). La kuongezea vinywaji vyake ndio vinauzika sana kuliko vinywaji vyovyote vile kwa Tanzania kwa sasa. Bakheresa bidhaa yake inayotembea sana ni ngano tu🤷🏾‍♂️
 
Back
Top Bottom