MO Dewji anawazidi vipi utajiri Bakhresa na Rostam Aziz?

Huyu jamaa utajiri wake wa magumashi na kiwanda cha juice eti ndiyo tajiri namba moja. Ukija kwa Bakhressa
ana meli, ngano, soda, kiwanda cha sukari chenye thamani ya bilioni 600, Azam TV na Azam Pesa.

Rostam Aziz anayemiliki kampuni ya ndege, caspian, Tigo Tanzania, Taifa gas, inakuwaje tunaambiwa huyu mbabaishaji eti ndiyo tajiri wa Tanzania? Ama anafanya ubabaifu aonekane hivo?
Punguza chuki mkuu AF pia penda kufatilia Mambo kwa Kina sio Juu kwa juu Mo alinunua viwanda vingi vya Textiles za kutengeneza vitenge na Kanga , wax kutoka serikalini Kipindi cha Ubinafsishaji na Vingi alivinunua kwa Bei chee na vingine alivipata Bure maana aliingia kama mwekezaji hadi akaja kuvipata moja kwa moja , yale mashamba ya mkonge ya serikali kule pwani na Tanga na Pale Makanya jamaa aliyapata kwa bei sawa na Bure , mo ana Kampuni ya Bima Mo assurance kumbuka taasisi za Bima ni taasisi zenye return kubwa sana kwenye investment zake na Pia mo kwa sasa wewe Unamjua tu kupitia mo energy Lakini ambacho hujui ni kuwa ana Vituo vya mafuta Star oil vingi tu, anatengeneza kila Kiti kuanzia sabuni , majani ya Chai , viberiti , mafuta ya safi hadi betri za redio zinaitwa Golden bell
 
Acha ujuaji sasa hizo star oil bakheresa zenji ana united petrolium
Sasa hivo viwanda vya kanga utapanga faida yake anayokwendq kutengeneza kwenye kiwanda cha sukari?
Hivo viberiti na mafuta utapanga na kiwanda cha ice cream na choclate?
Kuwa serious waweza miliki vitu vingi ila vya hovyo
 
Naamini Rostam Azizi ndiye Tycoon namba moja hapa nchini, hawa wengine ni Chawa tu.

Fuatilieni vizuri ukweli mtaujua.

Huyu Mwamba ni level ingine.

Hope one day nitazidi hapo alipofikia.
soma hapo, au gugu forbes 2022
IMG_20221108_174845.jpg
 
Hilo mbona lishajadiliwa sana humu na watu wakaliweka sawa.

Hii post ni ya kwenye moja ya hizo thread iliwekwa na mtaalamu Chief-Mkwawa

Hizi ni data chache ambazo zinaweza kukufumbua macho
1. asilimia 5 ya wafanyakazi wote waliopo kwenye formal sector Tanzania ni waajiriwa wa metl, kwa lugha nyengine katika kila watu 20 walioajiriwa kwenye formal sector mmoja ni metl

2. mo ameajiri watu 24,000

3. metl ipo nchi 12 Africa na ipo pia nje ya Africa nchi chache

4. asilimia 3.5 ya pato la taifa linatokana na mo

so hizi ni baadhi ya comparison za mo na bakhresa

-mo wafanyakazi around 24,000 bakhresa around 8,000
-metl nchi 12 na azam nchi 8
-metl pato 1.5 billion na azam pato 800 million

hizo data zote nimetoa about pages ya website zao.
Azam Worldwide - Azam Bakhresa Group
About Us | MeTL

kifupi mkuu mo ana hela kuliko bakhresa na wala hawalingani, maana amemzidi zaidi ya mara mbili.

watu wanashindwa kuamini sababu Bakhresa vitu vyake vyote vipo kwenye brand moja ya azam, ila mo ana viwanda na brand na biashara nyingi sana.

Mo kama mzalishaji
mafuta ya nyumbani
-mafuta maisha
-mafuta safi
-blueband mo margarine
-mafuta mpishi
-mafuta sunflower

vinywaji
-maji ya maisha
-maji masafi
-juice za pride
-soda za mo

nguo
-hakuna kampuni kubwa ya nguo kusini mwa jangwa la sahara kushinda metl. wana viwanda karibia kila mkoa wakitengeneza bidhaa za kanga na vitenge.

Vyakula
-unga wa ngano
-sukari
-korosho (mo cashew)

baiskeli
hapa kuna baisikeli za kawaida na za miguu mitatu za NABICO

mafuta ya magari
kampuni ya mo ya star oil ni moja ya wasambazaji wakubwa wa mafuta. uwezo wa lita milioni 5 kwa siku.

sabuni
-sabuni za royal
-sabuni za taifa
-sabuni za poa

mo kama mfanya biashara anaeagiza vitu nje
-agent wa LG tanzania analeta vitu kama mashine za kufulia, oven, mafridge na bidhaa nyengine za lg
-Agent wa TCL tanzania na TV zake
-analeta mitumba ya nguo
-AC za airlux
-battery za remote
-tractor za kulimia
-na mengine mengi kama big G, biscuit, tambi etc

mo kama muuzaji vitu nje ya nchi
jamaa anauza vitu vingi sana nje ya nchi kama
-katani
-korosho
-mbao
-nta
-choroko
-bidhaa nyengine tulizozitaja juu.

angalia hio diversity then compare na bakhresa.

Hatari
 
Wewe wakati unaangalia azam energy ndio zimuweke gsm au bakhresa wawe no moja kumbe wenzio Forbes wanajua utajiri wa mo ni zaidi hizo juice na chapati mo amewekeza hadi uarabuni na bado hujaambiwa kuhusu hisa nse
 
Safi mafuta(Dumu, Ndoo kubwa na ndogo), Mo Viberiti, Mo Protector, Mo Beauty na Aloevera, pia wakala wa sukari zote(Sukari pakti, 25kg, 50kg). La kuongezea vinywaji vyake ndio vinauzika sana kuliko vinywaji vyovyote vile kwa Tanzania kwa sasa. Bakheresa bidhaa yake inayotembea sana ni ngano tu
Bakheresa anafeli kuweka price ya vitu vyake juu kuliko wengine
Mfano kisimbuzi hataki kuendana na bei ya soko
Njoo kwenye energy drink nako hivo hivo an

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
 
Huyu jamaa utajiri wake wa magumashi na kiwanda cha juice eti ndiyo tajiri namba moja. Ukija kwa Bakhressa
ana meli, ngano, soda, kiwanda cha sukari chenye thamani ya bilioni 600, Azam TV na Azam Pesa.

Rostam Aziz anayemiliki kampuni ya ndege, caspian, Tigo Tanzania, Taifa gas, inakuwaje tunaambiwa huyu mbabaishaji eti ndiyo tajiri wa Tanzania? Ama anafanya ubabaifu aonekane hivo?
Said Salim Bakhresa amegawa utajiri wake kwa watoto wake, Azam tv ya yusuf sio said
 
Mo kawekeza mabiashara yenye kuleta pesa nyingi kuliko SSB. Azam anasubiri sana kwa METL
 
Back
Top Bottom