Mnyika tafadhali soma hii

Mleta hoja hakuandika kama ni tetesi, na tetesi si tuhuma za kuchafua watu. Tunachotaka humu ni ushahidi au facts zinazoweza kutusaidia kupata ukweli. Kipindi cha daladala huwezo kukifuatilia kupata ukweli. labda kama wale wanaozungumza wanafahamika, wanahojiwa kwa undani ili kuthibitisha madai yao, pia akili ya mwandishi mwenyewe kutambua uwezekano wa tuhuma yenyewe. Hata awe Makamba, januari, ngeleja, tutadai hayo ili kila mtu apate haki yake

Kwa mtazamo huo tuko pamoja mkuu! Asante.
 
Hizi ni habari za ndani kabisa na za uhakika, na tena huyu dogo kwenye akaunti yake ameingiziwa Tshs 280m kwenye benki fulani, muulizeni amepewa na nani ? asije kuwa anatumiwa na mapacha 3

Kaka nadhani utakuwa umekurupuka, Almost wabunge wote kawaida wakitoka kwenye uchaguzi na kuapishwa tu, cha kwanza ni kutafuta MIKOPO, Na hii MIKOPo huwa wantoa CRDB na NMB, Na average ya kila mbunge ni almost 200ML, kwahiyo mimi siwezi shangaa kuwa Mnyika ana 200+ kwenye akaunti.
 
kwa mtu mwenye akili zake sidhani kama anaweza kupoteza muda wake kwa kuangali hiko kipindi.:director:
 
sidhani kama mbunge aweza kuidhinisha eneo la kutupa taka!!!

Na kama alipewa hiyo rushwa basi mtoa rushwa si mfanyabiashara maana hajui namna ya kutumia fedha yake!!! IF SO THEN, HE GAVE THE WRONG PERSON!

ivi kwa mawazo haya na wewe unajinasibisha na ugreat thinker? umekosea kuweka ushabiki katika masuala ya kukemewa
 
Juzi kuna post moja nilichangia kuwa Mnyika hauwezi ubunge wa ubungo, nikasema walikuwa wanapangiwa maneno ya kuongea kwenye majukwaa na wananchi tukawaamini kuwa ni wapigananji kumbe ni kiini macho, sasa ona huo utumbo uliotajwa hapo juu, na mbaya zaidi kuna mwingine kaongezea kuwa kaingiziwa milioni 280 kwenye akaunti yake naamini hii itakuwa imeandikwa na mtu wa benki husika aliyoingiziwa hizo benki.unajua kama akaunti yako ilikuwa max ni milioni mara ghafla ukaingiziwa milioni mia2 lazima utajulikana tu siku hiyohiyo. Ududu huu bado tutasikia mengi
 
Kaka nadhani utakuwa umekurupuka, Almost wabunge wote kawaida wakitoka kwenye uchaguzi na kuapishwa tu, cha kwanza ni kutafuta MIKOPO, Na hii MIKOPo huwa wantoa CRDB na NMB, Na average ya kila mbunge ni almost 200ML, kwahiyo mimi siwezi shangaa kuwa Mnyika ana 200+ kwenye akaunti.

unachosea hakina makosa lakini kamuulize kama kapewa mkopo na benki gani kati hizo.bado naamini mpaka jamaa ameandika kuna milioni 280 kwenye akaunti ya Mnyika atakuwa huyu bwana ni mtu wa benki, na kama ni kweli ni mtu wa benki ni kwamba pesa iliyoingizwa kama mkopo huwa wanaona kwamba imeingizwa na nani kwa sababu gani. pesa nyingi kama hizo haziwezi ingizwa kienyeji enyeji na benki kubwa kama hizo
 
Kama ni kweli au sio kweli, mtoa hoja atusadie. Tusimshambulie mtoa hoja kama paka mwizi kwa kuwa anayetajwa ni Mbunge wa CDM. Naamini angekuwa wa CCM, mwanzisha hoja angesifiwa.

Mwaka 2008, Zitto Kabwe alipewa taarifa zote kuhusiana na ufisadi wa Group endowment wa PPF wa kugawana Tshs 220M kila mkurugenzi. Kwenye kikao akauliza kidogo, DG wa PPF akampiga na BUZWAGI la pesa, akawa anatetemekewa na PPF kama Mungu. Zitto akamshauri DG Erio awahonge Gazeti Raia Mwema akampa na namba za wahariri. Baada ya hapo, hutaona tena mambo machafu ya PPF kwenye Raia Mwema.

PPF walikuwa wanamkodia ndege kumsafirisha kwa shughuri za kibunge. Mfano alikodiwa ndege kwenda Kagera Sugar.

Nadhani sasa hivi wamekorofishana na DG ERIO ndio maana kakumbushia maovu ya 2008 ili waendelee kumuenzi.

Sishangai kama Mbunge wa Ubungo naye katekwa kupokea vijisenti, labda kafundishwa na Zitto.

Hii ni AIBU. Wana JF tuwe more positive kwa chama chochote sio kuchagua.

Nachukia UFISADI, ufanywe na CCM CDM CUF.....ni UFISADI tu.

Mleta hoja hakuandika kama ni tetesi, na tetesi si tuhuma za kuchafua watu. Tunachotaka humu ni ushahidi au facts zinazoweza kutusaidia kupata ukweli. Kipindi cha daladala huwezo kukifuatilia kupata ukweli. labda kama wale wanaozungumza wanafahamika, wanahojiwa kwa undani ili kuthibitisha madai yao, pia akili ya mwandishi mwenyewe kutambua uwezekano wa tuhuma yenyewe. Hata awe Makamba, januari, ngeleja, tutadai hayo ili kila mtu apate haki yake
 
Juzi nikiwa natizama kipindi cha daladala kinachorushwa na itv kila siku saa moja jioni.kuna tetesi mh. J.mnyika umechukua ela kutoka kwa magari ya maji taka ili yaendelee kumwaga maji taka hayo katika mabwawa ya kiwanda cha urafiki yaliyopo mabibo.je tuhuma hizi zina ukweli?tujulishe wapiga kura wako wa mabibo.

Tatizo lenu mnafanya kazi kwa tetesi badala ya fact,,, comes with fact after doing research... bahati mbaya humu hamna jukwaaa la tetesi wala umbea!
 
Juzi nikiwa natizama kipindi cha daladala kinachorushwa na itv kila siku saa moja jioni.kuna tetesi mh. J.mnyika umechukua ela kutoka kwa magari ya maji taka ili yaendelee kumwaga maji taka hayo katika mabwawa ya kiwanda cha urafiki yaliyopo mabibo.je tuhuma hizi zina ukweli?tujulishe wapiga kura wako wa mabibo.

mnyika na mabwawa ya kumwaga taka wapi na wapi? hizo ni shughuli za jiji!! muwe mnatumia hata chembe ya akili zenu kufikiria kabla ya kupost upuuzi kama huu
 
Mleta hoja hakuandika kama ni tetesi, na tetesi si tuhuma za kuchafua watu. Tunachotaka humu ni ushahidi au facts zinazoweza kutusaidia kupata ukweli. Kipindi cha daladala huwezo kukifuatilia kupata ukweli. labda kama wale wanaozungumza wanafahamika, wanahojiwa kwa undani ili kuthibitisha madai yao, pia akili ya mwandishi mwenyewe kutambua uwezekano wa tuhuma yenyewe. Hata awe Makamba, januari, ngeleja, tutadai hayo ili kila mtu apate haki yake
Aliyewasilisha mada kasema mnyika kala pesa za magari ya maji taka yaani yale magari yanayopakua mavi katika vyoo vilivyojaa, sasa hakuna muda wa kupoteza kumtafuta aliyeongea nadhani madereva wa magari hayo ni wahusika wakuu sasa kamuulizeni. na hii itakuwa na maana hata mavi yanayopakuliwa huku ilala na buguruni yake watakuwa wanakuja kumwaga huko kwa Mnyika?!!! kweli dogo siasa na utajiri kashindwa kuvitofautisha mapema. wanaubungo mtegemee harufuuuuuuuuuuuuu mbaya
 
unachosea hakina makosa lakini kamuulize kama kapewa mkopo na benki gani kati hizo.bado naamini mpaka jamaa ameandika kuna milioni 280 kwenye akaunti ya Mnyika atakuwa huyu bwana ni mtu wa benki, na kama ni kweli ni mtu wa benki ni kwamba pesa iliyoingizwa kama mkopo huwa wanaona kwamba imeingizwa na nani kwa sababu gani. pesa nyingi kama hizo haziwezi ingizwa kienyeji enyeji na benki kubwa kama hizo

Ni kweli kabisa sasa hajatuambia kuwa hela hizo zimeingizwa na nani,
Aje atuambie hela kaingiza nani.
Ila kaa ukujua wabunge WOTE wamekula 200+ kutoka CRDB/NMB.
 
Hizi ni habari za ndani kabisa na za uhakika, na tena huyu dogo kwenye akaunti yake ameingiziwa Tshs 280m kwenye benki fulani, muulizeni amepewa na nani ? asije kuwa anatumiwa na mapacha 3
MODs please delete hii thread, imekaa kizushi sana, no proof, no mashiko, nothing, ngoja ni-Report abuse
 
MODs please delete hii thread, imekaa kizushi sana, no proof, no mashiko, nothing, ngoja ni-Report abuse

Sasa unataka tuanze kuamini JF ni ya Chadema. Hii thread haina matatizo yoyote na kama MODs wataifuta tutajiuliza maswali mengi. Mbona tumejadili habari nyingi sana zenye mwelekeo huu kwa viongozi wengine hasa wa CCM?

Kumbukeni JF ni jukwaa la watu wenye maoni na milengo tofauti. Mnyika mwenyewe hajakanusha iweje wengine mumsemehe?

Sasa naanza kuelewa kwanini watawala huwa wanaangamiza vyombo vya habari vinavyowapinga, hata wewe ungekuwa mtawala si ajabu ungefanya hivyo hivyo!

Jamani wana JF!
Ndio maana JF inaonekana ni CDM kwa kupinga kila kinachoibuliwa against CDM na kuunga mkono kila kinachohusu ccm, mngeambiwa J. Makamba kapewa hela na makampuni ya madini kusafirisha udongo wenye dhahabu nje ya nchi naamini mngeendelea kudodosa na kusaka ukweli na sio kumjibia kuwa hiyo ina mhusu waziri wa madini kama mnavyomjibia Mnyika sasahivi. Ingawa habari hiyo ni tetesi lakini source imetajwa kipindi cha daldala ingawa ushahidi zaidi katika hilo unahitajika na pia sio lazima kila tuhuma ijibiwe lakini ukimya pia unaleta hisia za kuwepo kwa viji chembechembe vya ukweli lakini pia watu huchokoza ili wapate kitu flani ndani yake. Tuvumiliane jamani tunapotofautiana.

Tunachosema ni kwamba mtu akileta tuhuma aweke ushahidi eg angeweza kuleta makabrasha yanayoonyesha kwamba mnyika kapokea hela tajwa kwenye benki fulani tatehe fulani na kwa malipo ya kazi fulani,kwa nini tuvumilie tetesi katika mambo nyeti?
 
Hizi ni habari za ndani kabisa na za uhakika, na tena huyu dogo kwenye akaunti yake ameingiziwa Tshs 280m kwenye benki fulani, muulizeni amepewa na nani ? asije kuwa anatumiwa na mapacha 3

Me nadhani hapa tusiangalie pesa walizo pewa bali tutizame yale wanayo wajibika nayo kwa Jamii zetu je wanatekeleza walio haidi au? Uchaguzi ujao ndipo pa kuwahukumia hapo bila kuwapa nafasi ya kujieleza na waombe tu KATIBA isije nzuri wawe wanaponea hapo ila nauhakika KATIBA ikija mpya mchezo wao wa siasa chafu ndipo utakuwa mwisho wa viongozi wote ndania nchi hii maana walisha tuona sie madunga embeee kabisa ati

MODs please delete hii thread, imekaa kizushi sana, no proof, no mashiko, nothing, ngoja ni-Report abuse

hii sentensi huwa siipendi ya kumuamrisha MODs a delete post ya mtu. Ivi uhuru wa mawazo uko wapi? ivi kweli media ziko huru au bado hazijaapata uhuru? kwanini uifute? siku zote usidhani watanzania wote waatakuwa na mawazo kama ya kwako, jifunze kubadirika, achana na ubeberu huo. wewe changia mawazo yako kama hauna basi kaushia watu wachangie ima kumuelimisha aliyewasilisha mada au kuwaelimisha wasomaji wengine. please dont rpt this
 
Sasa unataka tuanze kuamini JF ni ya Chadema. Hii thread haina matatizo yoyote na kama MODs wataifuta tutajiuliza maswali mengi. Mbona tumejadili habari nyingi sana zenye mwelekeo huu kwa viongozi wengine hasa wa CCM?

Kumbukeni JF ni jukwaa la watu wenye maoni na milengo tofauti. Mnyika mwenyewe hajakanusha iweje wengine mumsemehe?

Sasa naanza kuelewa kwanini watawala huwa wanaangamiza vyombo vya habari vinavyowapinga, hata wewe ungekuwa mtawala si ajabu ungefanya hivyo hivyo!

thanks kayumba 4ur comments. Maana mimi siku nyingi huwa naona MODs wanaamrishwa kudelete post na wao wanafanya hivo najiuliza maswali mengi mengi na bado sijapata majibu ya uhakika,sasa hivi wanasema kuna uhuru wa vyombo vya habari lakini mie naona uhuru huo haupo ila ni kiini macho, kwani media nyingi huandika habari yenye maslahi na wao hii hali nayo inabidi ipaganiwe ni aina fulani ya ufisadi wa fikira za watu. Ama kweli nyani halioni kund..e wewe USWE kila siku mada zinazowahusu viongozi wa ccm husemi zitoeni ila kwa vile unaona Mnyika kavurunda mapema na niwachadema unakimbilia kuwa itolewe, ngoja tumonite hii post tuone kama itatolewa, kama itatolewa JF nayo ivue gamba maana itakuwa ni .........
 
Mleta hoja hakuandika kama ni tetesi, na tetesi si tuhuma za kuchafua watu. Tunachotaka humu ni ushahidi au facts zinazoweza kutusaidia kupata ukweli. Kipindi cha daladala huwezo kukifuatilia kupata ukweli. labda kama wale wanaozungumza wanafahamika, wanahojiwa kwa undani ili kuthibitisha madai yao, pia akili ya mwandishi mwenyewe kutambua uwezekano wa tuhuma yenyewe. Hata awe Makamba, januari, ngeleja, tutadai hayo ili kila mtu apate haki yake

Nawasiwasi sana na hili,yawezekana kipindi cha daladala wametumia lugha iliyojificha kufikisha ujumbe na asiyeweze kudadabuwa lugha hiyo akabaki kiza pasipo kuelewa nini kinaendelea,ni vyema tukawa makini na kuchunguza undani wa swala zima,tusitoe majibu rahisi kwa upenzi na unazi hehehehehe
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom