Mnyika, La hasha rais Kikwete si dhaifu bali.....

Ni dhaifu tena hilo neno bado ni jepesi. Ameshindwa na anawalea hao watu wake. Haoni sudani juzi watu wamewajibika wakaachia ngazi? Zaidi ya viongozi 50! Aondoke watu wenye nia na upendo wa nchi waongoze. Avunje bunge lote.
 
Jamani Presidaa ni dhaifu tena sana halafu mbaya zaidi amemteua PM ambaye ni dhaifu zaid yake. Angekuwa strong wa kukemea na kuchukua hatua wote aliowateua wangejua hivyo na wangechapa kazi ipasavyo.

Jikumbushe enzi za Edo Moringe alikuwa akitema cheche wahujumu uchumi wate wanajikojolea na wanarudisha vitu walivyopora wenyewe. leo hii anahitajika presidaa anaye tema cheche mara 10 zaid ya Sokoine kwa sababu viongozi wa leo nao wamepinda.
 
Hata wewe ulieanzisha hii thread pia ni dhaifu sana. kama hao wanaTaasisi ambao wote wameteuliwa na Dr JK ni dhaifu wanawezaje kumwangusha asiekua dhaifu kuliko wao? since 2010 mnasema tu wanaomwangusha Rais ni watendaji wake. Ina maana anapowateua huwa hajui kama ni dhaifu?

Kubali kataa Mnyika yuko sawa kabisa kuwa mkuu wa Nchi ni dhaifu thats it. Mara ngapi hapa JF hii kitu inasemwa? au kwa vile imesemwa bungeni na mbunge wangu Mnyika?

Kiongozi anaekubali madhaifu yake na kubadilika huyo ndio kiongozi sio anaekaa kusubiria watu kama wewe wamtetee kwa kusulubisha wengine kuwa eti ndio wanamwangusha. Kama ni dhaifu basi ni dhaifu. the only way is to change sio kubishana.
 
Nani asiyejua kuwa kikwete ni dhaifu? Hivi unaposema urais ni tasisi, muundaji wa tasisi hiyo si yeye anayeteua marafiki baadala ya wachapakazi. Watanzania tuache uvivu wa kufikiri. Mawaziri dhaifu nani anayewateua, hao wakuu wa mikoa anateua nani kama si rais huyo aliye dhaifu. Kuwajibisha mawaziri au watendaji hadi ashurutishwe huyo si dhaifu. Shule hazina vitabu, shule binafsi wanapandisha ada kama hakuna mwenyewe, hali ngumu ya maisha, kugawa vyandalua huku dhahabu yetu ikipotea. Niambie wewe ni sekta gani inayofanya vizuri chini ya kikwete? Fikiri sana unapoposti hapa JF. Inawezekana wewe ni mbumbu au ni kibaraka tu usiyejua unachofanya. kikwete ni dhaifu na ndiyo maana hata watendaji wanafanya madudu wanayofanya.

Nawapa onyo ccm wasijisahau na kufikiri watanzania ni walewale na kufikiri bunge ni lao akina Ndugae, wajue cheo ni dhamana. wapo waliokuwepo hawapo. Hongera Mnyika kwa msimamo wako mhimu tuko nyuma yako na tunaamini kama unavyooamini kuwa tuna rais dhaifu kuliko wote waliomtangulia na pengine haitatokea kuwa na rais dhaifu kama Kikwete

Heee! unanirushia mate!! hivi hakuna mwamvuli??
 
Tuanujua kusikia hujuhi, hata kuona hukuona,
Je hata kusoma?
soma tena!

Nitatoa tamko la kina baadae kuhusu kilichotokea lakini kwa ufupi ubovu wa bajeti hii ni matokeo ya udhaifu wa Rais Kikwete, yeye ndiye aliyesaini Mpango wa Taifa wa miaka mitano kama Kiongozi Mkuu wa Nchi tena kwa wino mwekundu kama Amiri Jeshi Mkuu.

Na yeye ndiye Mwenyekiti wa baraza la mawaziri, bajeti hii iliyoacha kuzingatia mpango wa Taifa imepita kwenye baraza alilloliongoza, pia kushindwa kutekelezwa kwa bajeti iliyopita ni matokeo pia ya udhaifu wa taasisi ya Urais.

Pia kwa mujibu wa Katiba Rais ndiye ambaye anapeleka bajeti bungeni, Waziri mwenye dhamana anapeleka tu kwa niaba.

Rais amepewa mamlaka makubwa juu ya bajeti ibara ya 99 imeweka mipaka kuhusu mambo ambayo bunge lina mamlaka nayo huku ibara ya 90 inasema bunge likikataa bajeti rais ana mamlaka ya kuvunja bunge.

Hivyo Rais Kikwete anapaswa kuagiza Waziri wa Fedha bajeti iondolewe irudi kwenye baraza la mawaziri ikafanyiwe marekebisho!

John Mnyika
19 Juni 2012
 
Kama jk ni dhaifu ilikuaje wakaenda ikulu kunywa juisi na kiongozi dhaifu?. Nilidhani bunge litakuwa na busara baada ya Lema kuondolewa.
 
anaangushwa na taasisi serikali, ambayo ndani yake kuna mawaziri,manaibu waziri,makatibu wakuu, wanasheria wa serikali,wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya,wakurugenzi wa manispaa,makatibu tawala na wafanya kazi wavivu wa taasisi za serikali.
Tusijaribu kuficha uchungu wa klorokwini kwa kuipaka sukari juu. Hao wote uliowataja na wengine uliowaacha (Mwanasheria Mkuu, Majaji, wakuu wa Bodi......) huwa wanachaguliwa na yeye. Ng'ombe anapoharibu vipando vya mtu hushitakiwa mchunga wake na Raisi wala asingeguswa kama angekuwa anawachunga kondoo wake.
 
mkuu jukumu la bunge ni kusimamia na kushauri serikali but at the end of the day ukishauriwa unaweza ukachukua maamuzi /ushauri au ukaachana nao.ok by the way yameshasemwa mangapi ya richmond hayakufanyika,madini,

I agree 100%
 
Kuendelea kuichekea serikali ya CCM na kiongozi wao dhaifu ni ujinga angalau Mnyika umesema ukweli na utabaki kwenye kumbukumbu kuwa Kikwete ni mdhaifu kashindwa kuiongoza nchi na hii serikali yake legelege...hivi hawa watoto wana matumaini gani?

View attachment 56860


Wa pili kutoka kushoto ni yule mbunge wetu mropokaji aka KIBAJAJI
 

anaangushwa na taasisi serikali, ambayo ndani yake kuna mawaziri,manaibu waziri,makatibu wakuu, wanasheria wa serikali,wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya,wakurugenzi wa manispaa,makatibu tawala na wafanya kazi wavivu wa taasisi za serikali.

Mkuu,

Nimependa hayo maneno yako ya mwisho, kwani ndio msingi mkuu wa hoja. Woote hao uliowataja ni wateule wa rais in personal, na wanakula kiapo cha utii kwa rais na si kwa taasisi ya urais (rejea kiapo cha katibu tawala wa mkoa wa Ruvuma juzi tu). Mwenye mamlaka ya kuwawajibisha ni rais mwenyewe na wala si kwa kushirikiana na mtu yoyote (Rejea wakuu wa wilaya na mawaziri umemtaja Mkulo).

So kama mambo yanaenda mrama, mfano ubadhilifu kwenye halmashauri mbali mbali, matumizi holela ya pesa, misamaha ya kodi iliyokidhiri, ukwepaji wa kodi mkubwa, na matatizo chungu tele mwenye kauli ya mwisho kukemea na kumaliza uozo huu ni rais na si what you call taasisi ya urais. He has all the powers za kuhire na kufire mtu yoyote asiyetimiza wajibu wake, kuanzia waziri mkuu, mkuu wa majeshi, makatibu wakuu, wakurugenzi na makamishna woooooote nchi hii wanawajibika kwake. Leo kila sehemu inanuka rushwa na ufisaji, executive president anajiweka pembeni, na nyie watetezi wake mnauita huo ni udhaifu wa taasisi ya urais. President himself is weak, hata Hosea alisema hivyo.

Bunge is weak, kwa sababu majority ya wabunge ni kutoka chama weak wanopigania chama hicho kisife.

Bravo John John, the truth shall always stand still.
 
kama hangetumia neno Rais,basi angekuwa amemshambulia kikwete binafsi.hivyo kutumia neno Rais nikwamba anamsema yeye na serikali yake.
 
hata wewe ulieanzisha hii thread pia ni dhaifu sana. Kama hao wanataasisi ambao wote wameteuliwa na dr jk ni dhaifu wanawezaje kumwangusha asiekua dhaifu kuliko wao? Since 2010 mnasema tu wanaomwangusha rais ni watendaji wake. Ina maana anapowateua huwa hajui kama ni dhaifu?

Kubali kataa mnyika yuko sawa kabisa kuwa mkuu wa nchi ni dhaifu thats it. Mara ngapi hapa jf hii kitu inasemwa? Au kwa vile imesemwa bungeni na mbunge wangu mnyika?

Kiongozi anaekubali madhaifu yake na kubadilika huyo ndio kiongozi sio anaekaa kusubiria watu kama wewe wamtetee kwa kusulubisha wengine kuwa eti ndio wanamwangusha. Kama ni dhaifu basi ni dhaifu. The only way is to change sio kubishana.


tena kwa heshima na taadhima nisema hapa mhe. Mnyika ametumia lugha ya ustaraabu sana ----- mimi nasema rais kikwete na watu wake wote ni wapombavu kabisa na sasa tutaenda mtaani bali usikubali lazima kieleweke
 
Ukisema Rais Kikwete ni taasisi hapo tayari sasa Serikali nzima so Dunia Nzima inajua Serikali ya Tanzania wasiwasi..kutwa kuomba hela kwa Wazungu tuna Kila kitu hapa Kodi Haikusanywi,Nchi isiyokusanya Kodi ni Corrupt...leo hii GGM,Vodacom,tiGO hazipo kwenye walipaji Kodi wakubwa wanashindwa hata na Serengeti Bia..sasa uchumi wa Tz tutegemee Kwenye Vileo...Je watanzania wakiokoka ??

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Kama baba ni kichwa cha nyumba lazima uonyeshe maana ya kuwa kichwa siyo unafanana na mkia alaa!! Tuache unazi Msumari wa Mh Mnyika Umegonga mahala pake mtake msitake msg sent ccm mjitafakari yapo mengi yanakuja
 
Kama jk ni dhaifu ilikuaje wakaenda ikulu kunywa juisi na kiongozi dhaifu?. Nilidhani bunge litakuwa na busara baada ya Lema kuondolewa.

Wow! I'm blown away by your ability to think and your reasoning capacity.:wink2:
 
Inabidi uonyeshe Rais kuwa si dhaifu!!!!!!!! ona uchumi wa nchi unavyo yumba wakati yeye kila siku anasafiri kwenda nje, bei za bidhaa unaona zinavyo ongezeka kila kukicha, umesikia bajet iliyo somwa ingiongezwa asilimia ya vinywaji, wakati tax bases zipo nyingi!

Huwezi kuonyesha Rais wa nchi anauwezo wakati sisi tunaona hamna kitu. Amebadili mawaziri kwa kushinikizwa angekuwa strong angefukuza hao kabla ya kutishika bungeni.

INABIDI UWE NA ROHO NGUMU KUMTETEA. WALIO WENGI WANA MRARAMIKIA WE MBONA NAWEWE NI KAMA YEYE?
 
Kuendelea kuichekea serikali ya CCM na kiongozi wao dhaifu ni ujinga angalau Mnyika umesema ukweli na utabaki kwenye kumbukumbu kuwa Kikwete ni mdhaifu kashindwa kuiongoza nchi na hii serikali yake legelege...hivi hawa watoto wana matumaini gani?

View attachment 56860
CCM hoyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee​
View attachment 56861
Dogo wabunge wako wanashinda kutukana chama cha upinzani.


Kwa rasilimali tulizojaliwa na Mola kwa kweli ni kufuru kubwa kuendelea kuona watoto walio katika hali hii huku tukijivunia miaka 50 ya Uhuru! Tena tukaiadhimisha kwa mbwembwe na gharama ya kutisha!!
 
Back
Top Bottom