Mnyika, La hasha rais Kikwete si dhaifu bali.....

May 10, 2012
92
71
Leo kwa mara ya kwanza katika historia ya bunge la Tanzania, Mbunge wa Ubungo kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo John John Mnyika aliamuriwa kutoka bungeni baada ya kukataa kufuta kauli yake tatanishi ya kuwa Rais Jakaya Kikwete ni Dhaifu...Hii ina maana ya kuwa kauli hii ya Myika itabaki katika hansard za bunge la Tanzania milele na milele.

Je, Mnyika kumuita Rais Kikwete Dhaifu ni sawa??

La Hasha Asilani, Mnyika alikosea sana, tena sana, kwani Rais Kikwete ni mtu (individual) na wala si serikali (executive) ama taasisi ya serikali (institution). Sote twajua moja ya majukumu makuu ya Bunge (Parliament) ni Kuisamamia serikali (Executive). Na kama Bunge ambalo Myika naye yumo ndani limeshindwa kuisimamia serikali (Executive) ambayo Myika anadai anayeiongoza ni mtu dhaifu, Je hilo bunge nalo tuliite Bunge Dhaifu?, na kama ni bunge Dhaifu lililoshindwa kusimamia Serikali Dhaifu, Je hii inamaanisha wabunge wa bunge hilo (wawe wa CCM, CDM, CUF, TLP, NCCR, UDP ama Viti Maalum awe Zitto, Mdee, Nchemba, Lembeli, Mbatia, Mwakyembe n.k) nao ni Dhaifu?.

La Hasha Asilani, kwani na aimini ndani ya bunge hilo tuna wabunge ambao si dhaifu asilani, na kuwaita dhaifu ni kumkosea mungu, kwani wanajitahidi sana kuwasilisha kero na matatizo ya wanajamii, lakini mwisho wa siku wanaangushwa na taasisi Bunge, naamini Rais Kiwete si Dhaifu Asilani ila
anaangushwa na taasisi serikali, ambayo ndani yake kuna mawaziri,manaibu waziri,makatibu wakuu, wanasheria wa serikali,wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya,wakurugenzi wa manispaa,makatibu tawala na wafanya kazi wavivu wa taasisi za serikali.


Kama Rais Kikwete angekuwa Dhaifu basi bajeti ya mwaka huu ingesomwa na Mustafa Mkulo.
 
Kijana Msomali habari ya asubuhi? Ukiwa huko huko Mogadishu tafadhari fuatilia na uifahamu kiundani mada unayotaka kuichambua kabla hujaanza kufuka. Samahani kama ntakuwa nimekukwaza kijana wa Sheikh Shariff, napita tu.
 
Kijana Msomali habari ya asubuhi? Ukiwa huko huko Mogadishu tafadhari fuatilia na uifahamu kiundani mada unayotaka kuichambua kabla hujaanza kufuka. Samahani kama ntakuwa nimekukwaza kijana wa Sheikh Shariff, napita tu.

Maneno MbofuMbofu...njoo na hoja ama kale mihogo na ulale...
 
"anaangushwa na taasisi serikali, ambayo ndani yake kuna mawaziri,manaibu waziri,makatibu wakuu, wanasheria wa serikali,wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya,wakurugenzi wa manispaa,makatibu tawala na wafanya kazi wavivu wa taasisi za serikali. "

Hao unaosema ndio wanaoangusha taasisi ya uraisi wanateuliwa na nani?
 
Rais ni dhaifu kwendelea kuwachekea chekea wezi wa mali za umma ni dalili ya udhaifu ameshindwa kuongoza watendaji waliopo chini yake.
 
Sana sana nami nakuunga mkono kuwa siyo dhaifu katika maswala haya. ila kwenye uongozi nabaki na myika kuwa JK ni dhaifu. Tena saaaaaana. most ever.

attachment.php
 
Ni dhaifu kuliko wadhaifu wote niliowahi kuona na kusikia.mkulo kaondoka kwa nguvu ya hoja na wala sio rahisi wako huyo dhaifu,kaambukiza udhaifu kila sehemu,ni hodari wa kuzalisha tu,maana antekeleza mpango wa kuongeza ildadi ya watu flani hivi.
 
mkuu jukumu la bunge ni kusimamia na kushauri serikali but at the end of the day ukishauriwa unaweza ukachukua maamuzi /ushauri au ukaachana nao.ok by the way yameshasemwa mangapi ya richmond hayakufanyika,madini,
 
ni dhaifu ukatae ukubali,ndio ukweli!sababu,coz hao wote waliokoserikalini yy ndo mwenye mamlaka ya kuwateua!ss inapofika majali wameshidwa lutekeleza majukum yao na rais anatambua hilo,y anashindwa kuwachukulia hatua?tunachoshuhudia mafisadi wanazidi kuitafuna nchi yetu!ni dhaifu!
 
ni dhaifu ukatae ukubali,ndio ukweli!sababu,coz hao wote waliokoserikalini yy ndo mwenye mamlaka ya kuwateua!ss inapofika majali wameshidwa lutekeleza majukum yao na rais anatambua hilo,y anashindwa kuwachukulia hatua?tunachoshuhudia mafisadi wanazidi kuitafuna nchi yetu!ni dhaifu!
 
Kumbuka rais wa Tanzania ni Imperial presidency. Watendaji wote wa serikali anawateua yeye.Udhaifu wake unawaambukiza na wengine. So "like father like son"
 
Sioni hoja hapa ya kuijadili. Haihitaji uwe kipanga kujua udhaifu wa Kikwete.
 
Kuendelea kuichekea serikali ya CCM na kiongozi wao dhaifu ni ujinga angalau Mnyika umesema ukweli na utabaki kwenye kumbukumbu kuwa Kikwete ni mdhaifu kashindwa kuiongoza nchi na hii serikali yake legelege...hivi hawa watoto wana matumaini gani?

View attachment 56860
CCM hoyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee​
mtoto.jpg
Dogo wabunge wako wanashinda kutukana chama cha upinzani.
 
Kikwete ni dhaifu kwani alisema anajua orodha ya wauza dawa za kulevya hadi leo kimya,pia ni dhaifu kwani katika wizi kwenye halmashauri zetu hakuna ailiguswa;mkulo,luhanjo,jairo wote wanakashifa na wanakula bata mtaani,baba riz wewe ni dhaifu ni ngumu kumeza ila huo ndio ukweli.
 
Nani asiyejua kuwa kikwete ni dhaifu? Hivi unaposema urais ni tasisi, muundaji wa tasisi hiyo si yeye anayeteua marafiki baadala ya wachapakazi. Watanzania tuache uvivu wa kufikiri. Mawaziri dhaifu nani anayewateua, hao wakuu wa mikoa anateua nani kama si rais huyo aliye dhaifu. Kuwajibisha mawaziri au watendaji hadi ashurutishwe huyo si dhaifu.

Shule hazina vitabu, shule binafsi wanapandisha ada kama hakuna mwenyewe, hali ngumu ya maisha, kugawa vyandalua huku dhahabu yetu ikipotea. Niambie wewe ni sekta gani inayofanya vizuri chini ya kikwete? Fikiri sana unapoposti hapa JF. Inawezekana wewe ni mbumbu au ni kibaraka tu usiyejua unachofanya. kikwete ni dhaifu na ndiyo maana hata watendaji wanafanya madudu wanayofanya.

Nawapa onyo ccm wasijisahau na kufikiri watanzania ni walewale na kufikiri bunge ni lao akina Ndugae, wajue cheo ni dhamana. wapo waliokuwepo hawapo. Hongera Mnyika kwa msimamo wako mhimu tuko nyuma yako na tunaamini kama unavyooamini kuwa tuna rais dhaifu kuliko wote waliomtangulia na pengine haitatokea kuwa na rais dhaifu kama Kikwete
 
Mtoa mada uko mbali sana na ukweli kwani yeye ndiye anayechagua hao mawaziri,wakuu wa mikoa,wilaya na wakurugenzi anauwezo nao sana tu kwani yeye ndiye aliyewachagua. kama wanamuangusha ni udhaifu tena mkubwa kuliko unavyofikiria
 
Back
Top Bottom