Mnyika kinara bungeni

Mkuu upo? Nakusubiri na wewe uingie Bungeni uwe Kinara kama Mnyika. Zamani Zitto ndio alikuwa Kinara lakini sasa naona Mnyika ndio Kinara.

Nipo mkuu wangu.

Niombee Mungu tu kaka.Kuingia Bungeni ni kuwakilisha kwa weledi.Ukinara unakuja kama matokeo tu.

Ni vyema tukawa sasa na vigezo vya kupima performance kitaalamu kwa kuangalia idadi ya michango na impact ya michango yako katika kubadili,sheria,kanunni au policy mbaya na kuleta zilizo bora.Hicho kitakuwa kigezo bora zaidi,na kama nitakuwa mbunge ningependa ubora/ukinara wangu upimwe kwa vigezo hivi.

While some politicians were great for a season because they defended the interests of the ordinary Tanzanians when those interests converged with their personal pecuniary or political interests, 'Mbunge yeyote ili awe kinara' should side with the people every time and on every issue. No one can dispute this.
 
Mnyika kinara wa Mwongozo spika, mpaka spika anamwambia kaa chini...Mnyika onyesha ukinara wako kwa kuleta maji Ubungo, Kimara njia mbovu njia azipitiki Kimara Bonyokwa, Kimara Temboni.

umerusha thread sasa hivi inayosema wananchi wa ubungo wampongeza kikwete kwa kuwajengea barabara, umezitaja zoootee!!

Sasa hapa unasema nini tena?
Unaona akili mchuzi inavyofanya kazi hapo?
 
MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tunapokea
taarifa hii, sasa napenda kuwatangaza ambao
wataanza kuchangia, kama tulivyotangaziwa tutaanza
na Mheshimiwa Joseph Mbilinyi na atafuatiwa na
Mheshimiwa Ali Abdallah na Mheshimiwa Kombo 215
Khamis Kombo ajiandae, pia Mheshimiwa Henry Daffa
Shekifu ajiandae, Mheshimiwa Mbilinyi!


MHE. JOSEPH O. MBILINYI: Mheshimiwa
Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi.
Napenda kuanza kwa kumshukuru Mungu kwa kila
jambo, wakati huo huo nawashukuru wana Mbeya
kwa support wanayonipa, wananitia nguvu ya kufanya
kile ninachofanya na napenda nitumie fursa hii
kuwaahidi kwamba tutakavyoanza ndivyo
tutakavyomaliza kwa stahili ya nguvu ya umma.
(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo nitachangia zaidi
kwenye masuala ya utawala bora ambao ndiyo msingi
wa amani na utulivu na kwa kuanza kwa maslahi ya
Taifa naomba nitoe rai kwa Wabunge wa Chama cha
Mapinduzi hasa vijana, mnapopata nafasi ya kukaa na
wazee wenu naomba tafadhali mtumie muda huo
vizuri kuwaambia ukweli wazee kuhusu ni nini hasa
kinachoendelea mtaani, kwamba mtaani watu
hawana furaha na maisha. Acheni upambe wa
kisiasa na fikra za kuwaza Uwaziri, ujumbe wa Bodi na
kadhalika, wazee wenu wako detached ndugu zangu,
ni jukumu lenu kuwaweka sawa na kuwasaidia kama
tunavyofanya sisi bila kuangalia itikadi za Chama kila
tunapopata muda wa kukaa nao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, huwa nashangaa sana
humu ndani vijana Wabunge wa CCM wanasimama
wanampongeza Rais kwa kuteua Wakuu wa Wilaya,
are we serious? Unampongeza Rais kwa kufanya
majukumu yake, kesho utampongeza kwa kunywa 216
maji. Sasa basi si haki kumpongeza Rais kwa kutekeleza
majukumu yake na hakika siamini kwamba huwa
anapokea pongezi zenu, kabisa siamini kama huwa
anapokea pongezi zenu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo
naomba niendelee sasa kwenye masuala ya utawala
bora ambao ndiyo msingi wa amani na utulivu. Leo
nitazungumzia suala ambalo halipo Mahakamani,
suala la kutekwa kwa ndugu yangu Daktari Stephen
Ulimboka. Hili suala halipo Mahakamani na najua
kwamba kesi ya Madaktari ipo Mahakamani, lakini
suala la kutekwa Daktari Ulimboka halipo Mahakamani
unless kutekwa huko ni sehemu ya mgogoro wa
Madaktari na Serikali ya Chama cha Mapinduzi.
Sasa basi…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mbilinyi naomba
nikukumbushe kwamba uongee kwa uhakika kwani
utakuja utakiwe kuthibitisha mambo haya. Ahsante.
Endelea!

MHE. JOSEPH O. MBILINYI: Yaliyomkuta Daktari
Ulimboka kutekwa ni mtiririko wa waliyoyakuta
Wabunge wa CHADEMA akina Machemli kukatwa
mapanga na huo unaonekana ni utamaduni mpya
sasa wa kuendesha mambo katika Taifa letu. Leo hii
nchi hii tunang'oa watu meno, tunang'oa kucha watu
kwa koleo kwa kuwa tu wana msimamo tofauti na
wanadai kitu ambacho wanaamini ni haki yao. Hii siyo
sawa kwani binadamu anapigwa mpaka figo
zinaacha kufanya kazi. Hili halikubaliki kwa sababu 217
tukilikalia kimya na inaonekana ni utamaduni mpya,
basi kesho watamteka Sugu kwa kusema ukweli.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu Ofisi ya Rais
ndiyo kila kitu na ndiyo jungu kuu, hapa ndiyo sehemu
yake ya kulisemea na kulikemea. Hicho mnachofanya
na yeyote anayefanya katika Mahakama ya Kimataifa
ICC yaani International Criminal Court kinaitwa torture
na adhabu yake ipo. Rais Bashir wa Sudan hakutumia
Jeshi wala Polisi kwa yale anayotuhumiwa bali alitumia
janjaweed, sasa inaonekana kama hapa kwetu sasa
pia halitumiki tena Jeshi wala Polisi wa Taifa bali kuna
element za janjaweed zinaanza kuteka watu ambao
wanaongea ukweli katika Taifa hili, hilo halitakubalika
na tutalikemea kwa maslahi ya Taifa na kwa maslahi
ya amani …..

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mbilinyi naomba ukae.

Mheshimiwa Daktari Mary Nagu!

KUHUSU UTARATIBU

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU,
UWEKEZAJI NA UWEZESHAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti,
Kanuni namba 68 inasema kwamba, Mbunge yeyote
ndani ya Bunge hawezi kuongelea jambo ambalo
hana uhakika kama ulivyosema wewe.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile kama Waziri na
kama Mbunge nasikitika sana Daktari Ulimboka
kukutwa na matatizo yale, lakini vile vile kwa Kanuni ya
64 kwamba, kila Mbunge humu ndani ataongelea
ukweli na jambo ambalo ana uhakika nalo. Naomba 218
Mheshimiwa Mbunge aliyekuwa anazungumza sasa
hivi aongelee mambo ambayo ana uhakika na
mambo ambayo hapotoshi Taifa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Mbunge
adhihirishe kauli yake.


MWENYEKITI: Nakushukuru Mheshimiwa Waziri,
kama nilivyoanza kuzungumza mwanzo kwamba
Kanuni ya 64 (1)(a) naisoma: "Mbunge hatatoa ndani
ya Bunge taarifa ambazo hazina ukweli." Sasa kwa
sababu Mheshimiwa Mbilinyi nilikutahadharisha
mwanzo, lakini ukaona uendelee kujenga hoja yako.
Nakuomba uthibitishe yale ambayo unayazungumza
sasa hivi yaani unaliarifu Bunge, hiki ni chombo kikubwa
sana na kama huna taarifa nacho, basi naomba ufute
kauli yako.


MHE. JOSEPH O. MBILINYI: Kwamba Daktari
Ulimboka alitekwa na kuteswa, nina uhakika nalo na
Tanzania nzima inalijua hilo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, bila kupoteza muda
wangu naomba unipe fursa sasa niendelee.
MWENYEKITI: Hapana, naomba uketi chini.
Umesema ametekwa na janjaweed, naomba uwataje
hao janjaweed kwa manufaa yetu ili Taifa hili, naomba
mnyamaze. Kanuni ya 72 inawazuia kuongea bila
ruhusa ya Kiti.
Ututajie Janjaweed ili Serikali ichukue hatua kwani
Serikali nzima ipo hapa, iwashughulikie kwa suala hili la 219
aibu kwa Taifa letu kumteka na kumdhuru mtu ambaye
ni raia wa Tanzania. Tanzania katika Katiba yake
inasema kwamba, kila mmoja ana haki ya kulindwa
maisha yake. Sasa naomba uwataje janjaweed ili
washughulikiwe kwa taratibu za kisheria. Tafadhali
naomba uthibitishe ama ufute kauli yako.

MWONGOZO WA SPIKA

MHE. TUNDU A.M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti,
Mwongozo!
MWENYEKITI: Naomba ukae chini!
WABUNGE FULANI: Kaa chini!
MHE. TUNDU A.M. LISSU: Kwani mnajua nataka
kuzungumza nini?
MWENYEKITI: Nimetaka maelezo ya Mheshimiwa…
MHE. TUNDU A.M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti,
kwani unajua nataka kuzungumza nini?
MWENYEKITI: Tusibishane, kaa chini!
MHE. TUNDU A.M. LISSU: Kwani unajua nataka
kuzungumza nini? Mwenyekiti naomba Mwongozo.
MWENYEKITI: Kwanza nimetaka maelezo kutoka
kwa Mheshimiwa Mbilinyi, kwanza kaa chini!
MHE. TUNDU A.M. LISSU: Naomba mwongozo! 220
WABUNGE FULANI: Atoke nje!

MWENYEKITI: Mheshimiwa usije kuni-provoke
maana yake nimewasikia, jana kwenye semina
naweza kumtaja mtu hapa, anasema mnapotutoa nje
tunapata umaarufu, sasa suala hili si zuri, tafadhali!
Mheshimiwa Susan Kiwanga nilimwambia alikiuka
kubishana na Kiti juzi akasema, naomba nielezee
halafu kwanza usibishane na mimi tafadhali.
Akasema mnapotutoa nje tunapata credit, sasa
hii tea politics Watanzania hawahitaji, Watanzania
wanataka tuwasemee kero ambazo zinawasumbua ili
tupate usuluhisho. Sasa haturuhusiwi kuropoka. Kanuni
ya 64(1)(a) inasema usilete taarifa ambazo huna ukweli
nazo na kama una ukweli uthibitishe, nimetaka nipate
uthibitisho janjaweed ni nani, tafadhali. (Makofi)

MHE. TUNDU A.M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti...
MWENYEKITI: Tafadhali usibishane na mimi.
MHE. TUNDU A.M. LISSU: Nimeomba Mwongozo.
MWENYEKITI: Naweza kutoa Kambi yote ya
Upinzani kama mnakiuka mamlaka yangu, naomba
mtii Kiti.
Mheshimiwa Mbilinyi tafadhali thibitisha na kama
huna uhakika basi futa kauli yako.

MHE. JOSEPH O. MBILINYI: Mheshimiwa
Mwenyekiti, naona umetoka nje ya track, Hansard zipo.
Sikusema kama kuna janjaweed bali nimetoa mfano
wa Rais Albashir wa Sudan ambavyo hakutumia
majeshi rasmi ya Taifa lake akatumia janjaweed
kwenda kushambulia Darfur na nikatoa mfano
kwamba watu waliomshambulia Daktari. Ulimboka
tumesikia wamekuja na silaha sasa kama wana silaha
na siyo majeshi ya Ulinzi na Usalama, hao ni nani kama
siyo janjaweed? Kwa hiyo, nilichofanya ni kutoa mfano
na nimesema kwamba...

MWENYEKITI: Naomba ukae chini. Nadhani
Mheshimiwa unatumia vibaya uhuru wa kujieleza humu
ndani. Wewe mwenyewe unasema kwamba umesikia
kwani maneno ya kusikia ni ya nini hapa? Tunataka
utoe taarifa za uhakika, huwezi kuiambia Serikali
unasikia, mambo ya mabarazani usilete humu ndani
kwani hii ni sehemu moja kubwa sana ya nchi yetu.
Naomba mheshimu Bunge tafadhali, kama huna
uhakika tafadhali usiongee kuhusu kusikia watu wenye
silaha, huna uhakika tafadhali.

TAARIFA

MHE. TUNDU A.M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti,
taarifa!
MWENYEKITI: Kaa chini, Mheshimiwa Mbilinyi
naomba uendelee kuchangia.

MHE. JOSEPH O. MBILINYI: Mheshimiwa
Mwenyekiti, ahsante kwa kuniruhusu niendelee, lakini
natumaini uta-save muda wangu ambao umepotea.
Mimi ninachosema ni kwamba, yeyote aliyehusika
na suala la Daktari Ulimboka aache ku-terrorise this
nation huku tukiendelea kuimba wimbo wa amani na
utulivu na iundwe Tume ya Bunge kama Tume ya
Daktari Mwakyembe ya Richmond, iundwe Tume huru
ya Bunge ikiwezekana ili ichunguze suala hili kwa
sababu Serikali haiaminiki katika hili, kwani kuna
complications.

MWENYEKITI: Naomba ukae chini! Suala la
Ulimboka kama huna uhakika nalo tafadhali zungumza
hoja nyingine, lakini suala la Ulimboka usiendelee nalo
kama huna uhakika nalo …..

Mheshimiwa Tundu Lissu, usibishane kwani hapa
siyo sokoni, tafadhali kaa kimya. Mheshimiwa Mbilinyi
kama huna uhakika tafadhali naomba ufute kauli yako
ama ongelea suala lingine uendelee na mchango
wako, otherwise naita mchangiaji mwingine aendelee
kama huna hoja nyingine.

MHE. JOSEPH O. MBILINYI: Nina uhakika kwamba
nahitaji Tume huru kwa ajili ya kuchunguza suala la
Daktari Ulimboka, hilo nina uhakika nalo na katika hili
Serikali haitaaminika, hivi ndivyo nilivyotumwa na wana
Mbeya niseme.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia kwa faida ya
amani na utulivu, sasa nahama nakwenda kwenye 223
Tume ya Maadili. Naunga mkono hotuba ya Upinzani
kwamba Tume ya Maadili sasa iwe wazi zaidi pale
inapotuchunguza viongozi. Wakija kutuchunguza
wawe na mfumo wa kuhakikisha kwamba taarifa
zinawafikia wananchi juu ya nani anamiliki nini na
chanzo cha fedha ni nini kwa sababu sasa hivi
kumekuwa na too much myths mtaani, kuna
minong'ono mingi mitaani na rumours, ni chanzo cha
kuvuruga amani hasa pale ambapo wananchi
wanakosa kupata maelezo ya kutosha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, limetokea suala la
nyumba ya Maige hapa ya dola 400,000 wakati mimi
nakwenda Dar es Salaam nimesimamishwa na vijana
pale Chalinze, wamenizunguka, wanasema
Mheshimiwa nini nyumba ya Maige dola 400,000,
twende tukupeleke Msoga ukaone Ikulu binafsi ya
Mkuu, wengine wanasema sijui kuna airport binafsi,
wengine wanasema kuna mitaa na kadhalika. Sasa
hizo zote ni myths ambazo kama hatutazi-control kama
Taifa zitatuyumbisha, Usalama wa Taifa, TAKUKURU,
Tume ya Maadili na kadhalika wafanye kazi yao ili
wananchi wawe wanapata taarifa za kutosha kuhusu
viongozi wao kuondoa manung'uniko ambayo
yanavuruga amani na kuondoa morale ya wananchi
katika Taifa hili.
Sasa basi, sitaki kuamini hayo mambo kwani hayo
mambo tulikuwa tunasikia zamani wakati wa akina
Mobutu sijui kajenga kasri la vyumba 100 kijijini kwao
Gbadolite na kadhalika, ndiyo hizo stori tulikuwa
tunazisikia. Perception ya watu iko hivi, Nyerere
katawala hii nchi miaka 24, kaondoka hana kitu mpaka 224
kajengewa nyumba na Jeshi, wanashangaa
wanapoona vitu vya ajabu. Mimi sijaviona, lakini
mamlaka zinazohusika sasa ni jukumu lao kuondoa hizi
myths ambazo zipo mitaani kwa watu kwa faida ya
amani na utulivu. Serikali iweke wazi mishahara, mafao
na kila kitu cha viongozi wote akiwemo Rais na ijulikane
wazi ili kutoa fursa kwa wananchi kuoanisha kipato
halisi cha viongozi pamoja na mali halisi wanazomiliki
na hii ni kwa faida ya amani na utulivu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, siungi
mkono hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Nakushukuru, naomba kumwita sasa
Mheshimiwa Rashid Ali Abdallah na Mheshimiwa
Kombo Khamis Kombo ajiandae.

MHE. TUNDU A.M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti,
mimi ni Chief Whip, kama unamruhusu Chief Whip wa
Serikali surely in a Multiparty Parliament, you can not
ignore the existence of the Opposition Chief Whip.

MWENYEKITI: Aliyeku–allow kuzungumza kabla ya
kuruhusu mimi ni nani? Naomba ukae chini!

MHE. TUNDU A.M. LISSU: Nimeomba Mwongozo!

MWENYEKITI: Nakushukuru Mheshimiwa. Kabla ya
kumwita mchangiaji anayefuata, naomba nimuite
Mheshimiwa Tundu Lissu, tafadhali!

MHE. TUNDU A.M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti,
nakushukuru sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla sijaomba
Mwongozo niliokuwa nataka kuutoa, naomba niweke
masikitiko yangu katika Kumbukumbu Rasmi za Bunge
kwa jinsi ambavyo mimi kama Mnadhimu Mkuu wa
Kambi ya Upinzani nafikiri hatutendewi haki humu
ndani. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mnadhimu wa Kambi
Rasmi ya Upinzani nina cheo sawa na Mnadhimu Mkuu
wa Kambi ya Serikali.

MWENYEKITI: Mheshimiwa eleza hoja ambayo
unayo, sasa hotuba ya nini? Elezea issue.

MHE. TUNDU A.M. LISSU: Nilisema niweke haya
malalamiko kwenye record kwa sababu
ninaposimama hapa nina hoja naomba nisikilizwe,
halafu hoja yangu ikataliwe.
Mheshimiwa Mwenyekiti, any way naomba
niombe Mwongozo wako kuhusu maelekezo ambayo
umempa Mheshimiwa Joseph Mbilinyi kwamba, 229
athibitishe kauli yake kuhusiana na kutekwa nyara na
kuteswa kwa Daktari Ulimboka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Kanuni ambayo
umeisema wewe mwenyewe na Kanuni aliyoisema
Mnadhimu wa Kambi ya Serikali ni Kanuni ya 64 (1) (a)
ya Kanuni zetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Kanuni inayohusika na
inayokipa Kiti chako mamlaka ya kumwelekeza
Mbunge athibitishe kauli yake ni Kanuni ya 63 fasili ya
(6)...

MWENYEKITI: Mheshimiwa Lissu isome Kanuni ya
64(1) (a), hebu isome inasemaje.

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti,
nashukuru. Inasema hivi: "Bila ya kuathiri masharti ya
Ibara ya 100 ya Katiba yanayolinda na kuhifadhi uhuru
wa mawazo na majadiliano katika Bunge, Mbunge
hatatoa ndani ya Bunge taarifa ambazo hazina
ukweli".
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niendelee. Sasa
kunapokuwa na hoja kwamba, Mbunge amesema
uongo kinachotakiwa cha kwanza kabla hajaambiwa
athibitishe kauli yake sijui kama nasikika maana yake
Mheshimiwa na wewe umewasha microphone yako!

MWENYEKITI: Unasikika, endelea.

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Kinachotakiwa kabla
Mbunge anayetuhumiwa kusema uongo hajaambiwa 230
au aifute kauli yake ni yale yaliyoko katika Kanuni 63(4)
inayosema kwamba: "Mbunge anayetoa madai kwa
mujibu wa fasili ya (3) ya Kanuni atakuwa na wajibu wa
kutoa na kuthibitisha ukweli kuhusu jambo au suala hilo
kwa kiwango cha kuliridhisha Bunge".
Kwa hiyo, yule aliyetoa hoja kwamba,
Mheshimiwa Mbilinyi ametoa kauli ya uongo, kabla ya
Mheshimiwa Mbilinyi hajatakiwa kuthibitisha kauli yake
au kuifuta, huyo alitakiwa atoe huo uthibitisho chini ya
Kanuni ya 63 (4), ili akiishatoa uthibitisho huo, huo mpira
wa kuthibitisha ukweli unamrudia sasa mzungumzaji wa
kwanza Mheshimiwa Mbilinyi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa naomba utupe
Mwongozo kama hayo maelekezo yako kwa
Mheshimiwa Mbilinyi ya kuthibitisha kauli yake juu ya
kutekwa nyara kwa Daktari Ulimboka ni sahihi wakati
huyo aliyedai ni uongo hajathibitisha uongo huo kwa
mujibu wa Kanuni ya 63 (4).
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Tundu Lissu Kanuni hii
tuliyoisoma ya 64(1)(a) ambayo inazuia kuzungumza
kitu ambacho huna ukweli, unajaribu kuipinga kwa
maslahi yako kwa kweli unapotosha Watanzania,
usitake umaarufu hapa.

MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA: Mheshimiwa
Mwenyekiti, kwanza, nakushukuru kwa kunipa hii nafasi
ili nami niweze kuchangia Hotuba za Bajeti hizi mbili,
lakini pia niweze tu kusema kwamba naunga mkono
hoja zote zilizotolewa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla sijaanza
kuchangia, niseme kwamba, nitachangia zaidi katika
eneo la Utawala Bora na kwa bahati nzuri kama
ulivyotoa ufafanuzi asubuhi alisema kwamba sisi
hatuulizi maswali tuko upande wa Serikali. Kwa hiyo, leo
nitachangia zaidi eneo la Serikali, kwa sababu nina
dhamira ya dhati ya kumwunga mkono Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete katika Hotuba yake aliyoitoa
jana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maneno
nitakayoyazungumza yawezekana wengine
hayatawafurahisha, sitapenda yawafurahishe kwa
sababu napenda ukweli usikike, Watanzania wasikie na
wale wenye kupenda ukweli watafurahi. Mama Teresa
alisema: "Yawezekana usiwe na uwezo wa kumpa mtu
kila anachotaka lakini angalau umpe hata furaha."
Umwoneshe angalau ume-smile ili na yeye iweze
kumwongezea maisha. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukweli ni kwamba,
mgonjwa anapokuwa Hospitali pale anapoambiwa
kwamba hakuna atakayekutibu, anakuwa
amenyimwa hata matumaini; ni hali ya kutisha na
inakatisha tama. Mimi kama Msomi wa Tanzania
nasema; suala hilo linaturudisha nyuma wasomi.
Pamoja na kwamba, suala hili lilifikishwa Mahakamani
lakini kwa kuwa upande wa pili wamependa
kuchangia, siyo vibaya na sisi tukachangia. Kuna suala
la mtu kukuomba moyo wako anasema nipe moyo
wako usiponipa nitakuua. Kwa hiyo, lugha nyepesi
amekuchagulia kifo. Haya ndiyo yanayofanyika kwa
wenzetu Madaktari. Nawashukuru sana Madaktari
wangu wa Mkoa wa Rukwa, kwa sababu
hawajagoma mpaka leo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu kinachohuzunisha na
kushangaza, wanaoongoza migomo hii, wanaohitaji
migomo hii kwa dhati yote ni wale ambao wako katika
Miji Mikubwa, ambao wana fursa ya kwenda kutibu
katika hospitali mbalimbali katika hiyo Miji. Kwa mfano,
Dar es Salaam wanakwenda Tumaini, wanakwenda
Agha Khan, wanakwenda TMJ na kote huko 260
wanapata hela. Hali kadhalika, wana hospitali zao
binafsi na wagonjwa wanaambiwa kwa tatizo hili njoo
Muhimbili nitakushughulikia wakati na pesa
ameshachukua, lakini haya yote hawayaoni.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nashangaa;
kwanza, nasema Mwenyezi Mungu ampe afya njema
ndugu yetu Dkt. Ulimboka. Nasema kwamba, kutokana
na Maandiko, Mungu amemwepusha kuendelea
kuongoza mgomo uliokuwa unaondoa uhai wa watu.
Mungu amemwepusha kuwa Hitler wa Tanzania.
Mungu amemwonea huruma atoke kwenye dhambi
hiyo kubwa. Wanaomsaidia kusemasema hapa;
tumeshasema mara nyingi, likitokea jambo kabla
halijatokea wenzetu wanaanza wanasemasema siku
mbili linatokea. Mimi nilishtuka pia hata Mheshimiwa
Martha aliposema siku ile, nikasema nadhani kuna
ukweli ndani yake. Kuna ile tabia ya mtu kujipiga kofi
shavu la kushoto halafu kujidai kulia mkono wa kulia.
CHADEMA mna la kujibu, kwa sababu mnasaidia
mgomo huu uendelee. Mnalo la kujibu.

KUHUSU UTARATIBU

MHE. JOHN J. MNYIKA: Kuhusu Utaratibu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Kanuni ya 64(1)(a):
"Mbunge hatatoa ndani ya Bunge taarifa ambazo
hazina ukweli."
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi ni mmoja wa
Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) na mchangiaji aliyezungumza ... 261
MWENYEKITI: Samahani, naomba ukae chini.
Nimesimama hapa si kukuvunja moyo wala kukatisha
maelezo yako. Kwa vile una uhakika wa kile ambacho
Mheshimiwa atakuwa amekisema, maana Kanuni hii
tukienda ile ya 63 atakuwa amekiuka. Sasa wewe utoe
uhakika ambao unaujua kwamba yule anasema sivyo.
Ahsante.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,
nilianza kutoa uhakika kwa kusema kwamba, mimi ni
Kiongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA). Mimi ni Mbunge na kwa nafasi yangu ya
Ubunge naingia kwenye Vikao vya Chama, lakini ni
Mkurugenzi wa Chama wa Habari na Uenezi, Mjumbe
wa Kamati Kuu ya Chama na Mjumbe wa Vikao vyote
vya Maamuzi vya Chama. Naomba kulihakikishia
Bunge lako kwamba, madai yaliyotolewa na
mchangiaji kwamba CHADEMA inahusika kwenye
migomo inayoendelea siyo ya kweli.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hili jambo kwa kuwa
limekwishaingia ndani ya Bunge lako, ili ukweli ujulikane
hapa wa chanzo cha hii migomo, tuletewe hapa
Bungeni Taarifa ya Kamati ya Bunge ya Huduma za
Jamii, ambayo ilikutana na pande zote; Serikali na
Madaktari, itabainika wazi kwamba maelezo
tunayopewa humu Bungeni na Serikali ni ya uongo.
Kwa kuwa Mheshimiwa Mbunge mchangiaji ni Mkuu
wa Mkoa, anatoa maelezo ya uongo Bungeni,
kuendeleza propaganda za Serikali dhidi ya raia
ambao tunawawakilisha, ili ukweli ujulikane taarifa hizi
ziletwe hapa Bungeni na Bunge lizijadili.

T A A R I F A

MHE. MWIGULU LAMECK NCHEMBA MADELU:
Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Acha Mheshimiwa Mnyika amalizie.

MHE. MWIGULU LAMECK NCHEMBA MADELU:
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna taarifa kwa huyu
aliyekuwa anasema.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mnyika umemaliza?
Mheshimiwa Mwigulu naomba ukae chini.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,
ninaomba aliyetoa kauli ya kukituhumu Chama cha
CHADEMA athibitishe. Naomba vilevile ili Bunge lako
Tukufu lipewe nafasi kwa mujibu wa Katiba, Ibara ya
63(2), kuisimamia Serikali kuhusu migomo
inayoendelea, tuletewe Taarifa iliyotumia fedha za
walipa kodi za miezi miwili ikakutana na Madaktari na
Serikali ikaahidi Taarifa hiyo italetwa Bungeni humu na
haijaletwa Bungeni na Serikali inafanya propaganda
mtaani kwa kutumia taarifa za upande mmoja.
Tuletewe hapa tuweze kuisimamia Serikali.

T A A R I F A

MHE. MWIGULU LAMECK NCHEMBA MADELU:
Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Taarifa.

MHE. MWIGULU LAMECK NCHEMBA MADELU:
Mheshimiwa Mwenyekiti, nampa taarifa aliyetoka
kusema. Kwa ajili ya muda, naomba niseme kupitia
Kanuni ya 68(8).

MWENYEKITI: Naomba uisome.

MHE. MWIGULU LAMECK NCHEMBA MADELU:
Mheshimiwa Mwenyekiti, inasema: "Vilevile Mbunge
yeyote anaweza kusimama mahali pake na kusema
taarifa na kwa ruhusa ya Spika atatoa taarifa au
ufafanuzi kwa Mbunge anayesema, ambapo
atamtamka Mbunge aliyekuwa anasema aketi
kusikiliza taarifa hiyo."
Mheshimiwa Eng. Manyanya, alipokuwa
anaongelea kuhusu uchochezi ule na kuhusu kuhusika
kwa Chama hiki, Kiongozi mmojawapo wa Chama
ametokea kukanusha. Mimi siendi mbali, nataka
kulithibitishia Bunge na Watanzania jinsi ambavyo
hawa wenzetu wameshiriki. Katika taarifa yao ya leo ya
Msemaji wa Kambi ya Upinzani, kuanzia ukurasa wa 26
pale lakini imetokea ukurasa wa 21, kuhusu migogoro
baina ya Serikali na Watumishi wake wameongelea.

MWENYEKITI: Samahani, hebu niongoze; sehemu
gani?

MHE. MWIGULU LAMECK NCHEMBA MADELU:
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuanzia ukurasa wa 21,
inaongelea migogoro baina ya Serikali na Watumishi
wake. Wameelezea migogoro yote ikiwemo na hii ya
Madaktari na mwisho pale kwenye ukurasa wa 26 wao 264
wenyewe kwa kutambua migogoro iliyokuwa
inaendelea na njia iliyokuwa inatumika kudai hiyo haki
kwamba ilikuwa ni migomo, wao wamesema ukurasa
wa 26: "Rai yetu kwa Watumishi wote wa Umma
waendelee kupigania haki zao na sisi tutaendelea
kuwaunga mkono." Wanaunga mkono mgomo hawa
halafu wanasema hawahusiki.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hili la ndugu yetu
Ulimboka, hawa CHADEMA kuna Mbunge wao wa
Rombo alipata ajali mbaya karibu na kifo, hawajawahi
hata kwenda kumsalimia wala kumpigia simu. Leo hii
kwa Ulimboka kwa sababu kuna kazi walimtuma
wanalialia kimbelembele. Hivi kweli leo hii amekuwa
ndugu yenu kule yule wa Rombo?

WABUNGE FULANI: Boya, boya!

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,
taarifa ina haki ya kujibiwa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Manyanya, endelea.
Nadhani taarifa hizi zimefika kwa wahusika. Sasa
naomba tuendelee; Mheshimiwa Eng. Stella
Manyanya.

MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA: Mheshimiwa
Mwenyekiti, ahsante sana. Ninaomba kwa wale
wenye taarifa basi waniache nimalizie ili waweze kutoa
taarifa nyingi zaidi kwa sababu bado naendelea.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kudhihirisha hayo pia
katika misemo inayozungumzwa inasema kwamba, 265
waliokuwa wamemchukua huyo bwana walikuwa sijui
na mavazi; lakini ukiangalia mavazi kama ni ya askari
yanafanana sana na Magwanda ya CHADEMA.
(Kicheko)

KUHUSU UTARATIBU

MHE. JOHN J. MNYIKA: Kuhusu Utaratibu.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mnyika, kaa chini.

Tafadhali endelea.
MHE. JOHN J. MNYIKA: Kuhusu Utaratibu.

MWENYEKITI: Sikuruhusu.

MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA: Kwa hali hiyo
basi.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti!

MWENYEKITI: Mheshimiwa Manyanya, kaa chini.
MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,
nashukuru sana. Mzungumzaji aliyezungumza na ni
Kanuni ya 61(1)(a) inasema kwamba, hatatoa ndani
ya Bunge taarifa ambazo hazina ukweli na hatatumia
lugha inayodhalilisha watu wengine. Mzungumzaji
aliyezungumza kwanza ametoa taarifa zisizokuwa za
ukweli kwamba waliomteka nyara Dkt. Ulimboka na
kumjeruhi ni watu waliokuwa wamevaa magwanda na
kwamba ni watu wanaofanana na CHADEMA na ni
udhalilishaji kwa wengine sisi wa CHADEMA. 266
Niseme kwamba, mzungumzaji anapaswa
kufahamu kwamba, kwenye Vyombo vya Habari na
Kanuni zetu za Bunge zinasema; Mbunge hatahesabika
kuwa anasema jambo la uongo kama atanukuu
taarifa za vyombo vya habari.
Kwenye vyombo vya habari, Dkt. Ulimboka bahati
nzuri yuko hai, amenukuliwa mwenyewe akisema
kwamba, waliomteka nyara ni Askari Polisi na wengine
amewataja kwa majina. Sasa kama Askari wa Polisi ni
CHADEMA, Mkuu wa Mkoa ambaye ni sehemu ya
Serikali, atueleze hapa kwamba Askari wale ni wa
CHADEMA? (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Mimi nadhani Mheshimiwa
Mnyika, ilikuwa kwanza ukanushe Taarifa ya Msemaji
Mkuu wa Kambi ya Upinzani hapa ili tuanzie pale, kwa
sababu... kaa chini.
Kwa kuwa umeshindwa kujibu hoja ambayo
Mheshimiwa Mwigulu alitoa taarifa kutokana ... kaa
chini basi, mbona unawashwawashwa! Umeshindwa
kuheshimu taarifa ambayo umepewa na Mheshimiwa
Mwigulu. Mimi ningependa kuona umahiri wako kama
Mkurugenzi wa Habari wa CHADEMA, ukanushe taarifa
hii ya Msemaji wa Kambi ya Upinzani hapa kwanza
tuendelee, lakini badala ya kujibu hoja hii umerukia
nyingine. Mtayumbisha Kiti, tungeenda taratibu hoja
kwa hoja then tunakwenda mbele, lakini umeshindwa
kujibu hili. Kwa kuwa ulishindwa kujibu hoja hii na kwa
kuwa muda hauruhusu, naomba nimwachie
Mheshimiwa Eng. Stella Manyanya aendelee.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,
naomba nafasi ya kujibu hilo.

MWENYEKITI: Kaa chini. Mheshimiwa Moses
Machali, kaa chini. Mheshimiwa Machali, una tatizo
moja; kudandia hoja za watu. Usitake umaarufu hapa
kaa chini. Sergeant-At-Arms mtoe nje Mheshimiwa
Moses Machali. Naomba atoke nje ya gate arudi kesho
asubuhi. (Makofi)
(Hapa Mhe. Moses Machali Alitolewa Ukumbini)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Manyanya, endelea.

MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA: Mheshimiwa
Mwenyekiti, nakushukuru kwa busara zako, lakini
niseme tu kwamba ni maana ya rai ya Mheshimiwa
Rais; ndiyo maana Mheshimiwa Rais amelihutubia Taifa
na akasisitiza kuwa, anataka kuhakikisha kwamba
Vyombo vyake vya Ulinzi na Usalama vihakikishe
vinafuatilia kwa umakini na kuweza kubaini nani
amehusika na vitendo hivyo. Hii yote ni kwa sababu ya
kutuondoa sisi kwenye nafasi hii ya kutupiana
madongo humu ndani. Kama ni suala la kutupa
madongo, kila mtu anao uwezo wa kutupa dongo. Je,
tutakuwa tumefikia usuluhishi; na hapo ndiyo maana
nasema mjifunze kwamba hata sisi huku tunayo ya
kuwaambieni ninyi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nazidi kusisitiza kwamba,
kila mtu anamtegemea mwenzake, Polisi kama
utakumbuka ... 268
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa
mzungumzaji)

MWENYEKITI: Mheshimiwa muda umekwisha,
nakushukuru.

MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA: Mheshimiwa
Mwenyekiti, muda wangu ulichukuliwa.

MWENYEKITI: Naomba uendelee.

MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA: Mheshimiwa
Mwenyekiti, kama utakumbuka, najaribu kuangalia
yale ambayo yalijitokeza moja kwa moja. Baada ya
kutokea lile tatizo tayari Dkt. Mkopi aliomba Vyombo
vya Usalama vifanye kazi, kwa maana hiyo
tunategemeana. Kuonesha kwamba, mwananchi au
huyu ambaye anakuwa ameenda hospitali kakosa
matibabu anapata tabu kiasi gani? Madaktari waone
jinsi ambavyo walimhudumia mwenzao.
Kwa hali hiyo basi inaonekana kwamba, hata
kama wanasema kuna mgomo wenzetu bado
wanatoa huduma kwa ndugu zao, lakini wanaokufa ni
wale wasio na ndugu. Sasa niungane na alivyosema
Mheshimiwa Kasikila, kuna wagonjwa wanaotoka
Sumbawanga wanafuata huduma Dar es Salaam,
kuna wengine wanafuata huduma Mbeya au KCMC,
wanafika pale wanakuta kuna mgomo; na ukiangalia
hata katika distribution ya watumishi, unakuta kuna
baadhi ya maeneo hayana watumishi wenye asilia na
huko pengine nao wangepata uchungu wa 269
kuwasaidia ndugu zao. Kwa hiyo, ombi langu ni
kwamba, hizi rasilimali za Taifa, hizi ajira za Taifa,
zisambazwe kwa kadiri ya mtazamo wa nchi nzima ili
kila mtu anapokuwa kwenye utumishi, aweze
kukumbuka umuhimu wa kusaidia ndugu zake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya hayo,
naungana na maneno yote aliyoyazungumza
Mheshimiwa Rais wetu jana na ninaunga mkono hoja
kwa asilimia mia moja. Ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Ninakushukuru sana. Waheshimiwa
Wabunge, naomba niwakumbushe Kanuni zetu; haya
maneno ya sijui nini, hayatusaidii. Naomba tutunze
nidhamu, tuongozwe na hizi Kanuni, lakini kwa sababu
tunafanya ushabiki Watanzania wanashindwa
kutuelewa kama kweli tunastahiki sisi kuwa Wawakilishi
wao. Tunazungumza masuala ya msingi hapa,
naomba tuzingaite, tunafahamu Kanuni zinazuia
kuongea bila ruhusu ya Kiti lakini mmefanya Bunge
kama klabu. Bunge siyo klabu ni Chombo cha juu sana,
wenyewe mmesema Bunge lina jukumu la kuisimamia
Serikali; hivi kweli tunasimamia Serikali?
Mnapofanya hivi, mnazomea, makofi yasiyokuwa
na msingi, nadhani tunataka kupoteza heshima yetu.
Nawakumbusha kulinda heshima yetu kama
Wawakilishi wa Wananchi. Hapa hatujibishani kama
tupo sokoni, tunajibishana kwa hoja. Hoja ikitolewa
tuijibu kwa ustaarabu. Sasa kama hoja inatolewa
hujibu kwa ustaarabu, siyo jambo jema. Naomba
tunapoendelea tuendelee kujadili katika hali ya
umakini. Tuisaidie Serikali, pale ambapo tunahisi 270
inahitaji kukumbushwa basi ni wajibu wa Bunge kama
Wawakilishi wa Wananchi kufanya hivyo.
Baada ya kusema hayo, kwa vile muda
hauruhusu, naomba niwataje watakaonza kuchangia
saa tatu baada ya maswali na majibu; Mheshimiwa
Selemani Jafo, Mheshimiwa Mussa Haji Kombo,
Mheshimiwa Amina Abdallah Amour na wengine
wataendelea. Nawashukuru, jioni njema. Naomba
kuahirisha Shughuli za Bunge.
 
huyu mwenyekiti wa Bunge kweli ni bogus la kufa mtu, pili nimeamini ukitaka kujua rangi halisi ya mtu mpe madaraka, huyu STELA MANYANYA namkumbuka vema kwenye Bunge la spika sitta alivyokuwa anajidai jemedari wa kupambana na ufisadi leo kapewa ukuu wa Mkoa na VX kawa mjinga kabisa anaudhi kama nini mama huyu.
 
Anaonewa vipi wakati yeye kinara? Hivi vijisababu eti Keenja kakaa miaka mingapi ni vya kisengelema. Siku tukiwapa nchi CDM watakuja na majibu hayo hayo CCM imekaa miaka 50. Wakati anaomba kura Mnyika alisema ataondoa hizi kero na akirudi atapimwa kwa hilo sio idadi ya miongozo ya spika.

Hiviwtu kutoka sengelema wanaitwaje? au ndio *******-lema?
 
Mkuu wewe siku zote hakuna jema analofanya Mnyika...Mimi ni mkazi wa Ubungo na huyu ndiye mbunge bora ukilinganisha na wabunge wengine kwa kipindi cha miaka 20

Molemo Kimbunga ameonyesha sababu na ushahidi wa maeneo yanayomfanya aone kuwa Mnyika hajafanya kazi kama alivyowaahidi wapiga kura wake. Je unaweza kutupa sababu na ushahidi uliosababisha umtangaze Mnyika kuwa mbunge bora kuliko wote waliotangulia kwa kipindi cha miaka 20 iliyopita?
 
sasa kumbe watu mnapenda kuongopewa eeh! manake mimi ni miongoni mwa watu ambao niliwah kusema mnyika anataka kudumaa kisaisa kwa hli jimbo. na wakati nasema nilionekana niviroba lkn wachambuzi wa siasa walisema ni kweli.hatuwez kumtegemea amalize haya yote kwa mara mja ila kule alikofanya apewe hongera zake na siyo kuonekana kana kwamba hajatend kabisa.

Sina uhakika kuwa inahitaji muda mrefu sana kutatua tatizo linalojulikana na hasa kwa kuwa alishasema analiweza. Kinachotakiwa ni kuanza kulitatua na kupima hatua kwa hatua ufanisi wake. La sivyo, itapita miaka 20 akiwa mbunge na asiwe amefanya lolote kuhakikisha matatizo yanayoahirishwa yametatuliwa.

Lakini ni vyema pia akasema wazi kuwa matatizo fulani fulani ameyashindwa. Ili asije akalaumiwa kwa kutoyamaliza.
 
Hili halinamtu wa kupinga.
Mnyika nikati ya wabunge nchini tanzania ambao ni dhaifu.
1. Mnyika kazi yake kupiga kelele tu bila kutekeleza ahadi za jimbo lake.
2. Huyu mnyika hataki hatakukutana na wananchi wake.
3. Hajawahi hata sikumoja bungeni kusemea kero za jimbo lake.
4. Mnyika ni dhaifu sana kero za maji za kimara hazisemei yuko kimya tu haji kutuona huku kimara.
kazi yake kuhamasisha maandamano watu waandamane ili walete fujo.
5. Mnyika alikuja analia lia ubungo akiomba msaada watu wamchangie wakati wa kampeni (Mnyika unakumbuka pale shekilango ulivyokuwa unalia wakati wa kampeni kuwa hujiwezi na watu wakakuchangia?) sasa mnyika kafanya nini shekilango.

Mnyika alikuwa akizunguka kweli na kuonakana kama mtu mzalendo kumbe anataka kula tu.

Mnyika ni dhaifu.
 
Hili halinamtu wa kupinga. Mnyika ni dhaifu.

Mimi napinga. Ila wewe ni kama mtoto anayejifunza kusema, huigiza misemo ya alionao. Msamiati wa neno Dhaifu lililetwa na Mnyika; sasa inakuwaje wewekuigiza maneno ya mtu unayemwita dhaiu?

WEWE NI DHAIFU A DHALILI
 
Waziri wa mambo ya maji unamfahamu boss Annael?DAWASCO/DAWASA unawafahamu?Mnyika alishasema kiongozi wa udhaifu hapa nchini ni nani na hilo lipo kwenye hansard.Wewe ni dhaifu pia,umeifanyia nini Kimara?,walau kuokota taka za rambo hatua chache kutoka kibandani mwako?WALAU KUACHA KUTUPA TAKA OVYO?
 
wewe una matatizo au ya kiakili au una bifu binafsi na Mnyika! huyu ni mbunge ambaye muda mrefu sana anakuwa jimboni na wananchi na amekuwa bega kwa bega na wananchi kutatua matatizo ya wanancchi na kikubwa zaidi huwa anatoa feed back ya kazi zake, nenda ubungo shina ya maji inatatuka, barabara zinanyooshwa,ulinzi upo imara huyu mnyika ni hazina kubwa ya taifa letu! ila wewe mleta mada huwa ni kawaida yako kutopoka ila signature yako inakuhusu wewe mwenyewe, isome halafu ujipime nayo!!tembelea blog ya mnyika uone kazi zake umchallenge kutokea hapo!!
 
Waziri wa mambo ya maji unamfahamu boss Annael?DAWASCO/DAWASA unawafahamu?Mnyika alishasema kiongozi wa udhaifu hapa nchini ni nani na hilo lipo kwenye hansard.Wewe ni dhaifu pia,umeifanyia nini Kimara?,walau kuokota taka za rambo hatua chache kutoka kibandani mwako?WALAU KUACHA KUTUPA TAKA OVYO?

Kwani mnyika sio dhaifu kwi kwi kwi kwi!
 
Vipi mambo ya makundi CCM yanaendeleaje pamoja na zile harakati za KUCHAKACHUANA kimakundi???????
 
Back
Top Bottom