Mnyika anaomba Ushirikiano wenu kwenye hili

K-killer

Senior Member
Nov 14, 2011
147
28
Kutoka tweeter;

Kwa wale wanaotaka kushiriki na kuongeza nguvu ktk kampeni zetu za CHADEMA Vijibweni-Kigamboni wasilianeni na:Kilewo 0714225960/0756091748
 
Si upewa telephone number hapo! Kwanini usiwapige na maswali yako ukaelekeza huko? Mbona unapenda kuwa spoon feed kama SIOI SUMARI?

Yaani yeye ndiye anayehitaji msaada halafu mimi ndiyo nimpigie kumuuliza anataka nini? Siwezi nikawa mbuyuyu kiasi hicho.
 
Kutoka tweeter;

Kwa wale wanaotaka kushiriki na kuongeza nguvu ktk kampeni zetu za CHADEMA Vijibweni-Kigamboni wasilianeni na:Kilewo 0714225960/0756091748

Utafiti wa Aweda si ulituhakikishia ushindi wa 70%?
 
Kutoka tweeter;

Kwa wale wanaotaka kushiriki na kuongeza nguvu ktk kampeni zetu za CHADEMA Vijibweni-Kigamboni wasilianeni na:Kilewo 0714225960/0756091748

Chama kimefilisika hiki, mtatuomba mpaka nguo zet a ndani sasa tuuze tuwachangie

[h=2]Kutoka tovuti ya Mh. John Mnyika

Wednesday, March 21, 2012[/h][h=3]Soma, Shiriki na Shirikisha na wengine kuwezesha mabadiliko ya kweli[/h]

Soma, Shiriki na Shirikisha na wengine: Mabadiliko Arumeru Mashariki (Arusha) na Vijibweni (DSM) yatawezeshwa na wewe, mimi na wenzetu.

Kesi ya uchaguzi wa Ubunge Ubungo imenifanya nishindwe kurudi Arumeru Mashariki mapema kwa kuwa nawajibika kuandaa ushahidi na mashahidi. Kiroho nipo pamoja na makamanda wengine katika mapambano kuhakikisha Nassari anaungana nasi kupunguza hodhi ya chama kimoja bungeni. Katika siku hizi ambazo nalazimika kuwepo DSM, kiakili na kimwili pamoja na kesi na majukumu mengine ya kibunge naelekeza nguvu katika uchaguzi wa udiwani kata ya Vijibweni Jimbo la Kigamboni Manispaa ya Temeke.

Marafiki zangu na wote mnaouniunga mkono mlio Arusha naomba muwezeshe uwepo wangu kiroho kwa kushiriki katika harambee ya kuchangia chama itakayofanyika Naura Spring Hotel tarehe 23 Machi 2012 kuanzia saa 1 Usiku. Wasilianeni na Mwigamba 0784815499 au 0713953761 kwa maelezo na maelekezo. Mkishashiriki mnipe mrejesho kuhusu ushiriki wenu kupitia mnyika@chadema.or.tz ili Mungu akipenda nikija Arumeru Mashariki mwishoni mwa kampeni kuongeza nguvu tuweze kuonana. Hakuna Kulala; Mpaka Kieleweke.

Marafiki zangu na wote mnaoniunga mkono katika Jiji la Dar es salaam naomba mshirikiane nami kwa hali na mali kuhakikisha kwamba Manispaa ya Temeke ambayo ndio pekee katika mkoa wa Dar es salaam isiyokuwa na Diwani yoyote wa kata wa CHADEMA inapata walau mwakilishi mmoja kutoka chama mbadala. Wasilianeni na Kilewo 0714225960 au 0756091748 kwa ajili ya maelezo na maelekezo na mnipe mrejesho kupitia mnyika@chadema.or.tz. Kwa kipindi cha mwaka mmoja cha utumishi wa umma nimeshuhidia umuhimu wa kuchanganya vyama katika mabaraza ya madiwani katika kuongeza uwajibikaji kwenye usimamizi wa fedha za umma katika serikali za mtaa ambazo ndio zinashughulikia kwa kiwango kikubwa masuala ya maendeleo katika maeneo yetu. Tuunganishe nguvu ya umma kuwezesha mabadiliko ya kweli. Shiriki sasa na shirikisha na wengine; Maslahi ya Umma Kwanza.

John Mnyika (Mb), Mkurugenzi wa Habari na Uenezi (CHADEMA)-22/03/2012
 
Kutoka tovuti ya Mh. John Mnyika

Wednesday, March 21, 2012

Soma, Shiriki na Shirikisha na wengine kuwezesha mabadiliko ya kweli

Haya Radhia na Ritz mmeelewa?
 
Radhia Sweety anazidi kushow love kwa Mh Mnyika. Uzi wenye neno Mnyika haumpiti kando huyu mtoto. Usifiche ugonjwa bibie mueleze kwa uwazi JJ anaweza kukuconsider. Ulianza na ohhooo amekata kujibu kwa Diva kama hajoa... Huyo sasa kakuibukia hebu mPM
 
Nakumbuka mkuu tena alisema kawahoji wakazi wote wakasema wataichagua Chadema sasa sijui pesa ya nini tena.

Hizo ni mbinu za kujenga chama, kwa taarifa yako baadhi ya wabunge na madiwani wa CDM walishinda uchaguzi uliopita kwa mbinu hiyohiyo ya walalahoi kuchangia na matunda yake wanayaona na hata hawajuti. Mf. Kata ya Vwawa wilayani Mbozi walimchagua diwani kupitia CDM kwa michango ya kuanzia Tsh. 50/= na usafiri wa baiskeli kawaulize leo kama wanajuta, ameweza kushusha mchango wa maendeleo toka Tsh. 15,000/= hadi sh. 5,000 na kazi iliyofanyika ilikuwa ni ileile ambayo makadirio yake yalikuwa Tsh. 15,000/= kwa mtu. Je kama mtu alichangia sh. 200 wakati huo akampata mbunge na leo amesave 10,000 huoni kama kuna hatua hapo? na kumbuka mtu akichangia hizo ndogondogo kwanza ni aina ya kuonyesha commitment hivyo hata kura hawezi kuchakachua. CCM wanatumia mafisadi, CDM inatumia walalahoi wanaotafuta ukombozi. Go on Mnyika, go on CDM mi nitachangia 20,000/= kwa sehemu zote mbili Dar na Arumeru
 
Back
Top Bottom