Mnyika ahamasisha wananchi wadai maji

Serayamajimbo

Senior Member
Apr 15, 2009
191
38
MBUNGE wa Ubungo John Mnyika (Chadema), amewataka wakazi wote wa jimboni kwake kuifanya Wiki ya maadhimisho ya Maji kuwa ya madai ya maji huku akitoa mawasiliano ya Bodi ya mamlaka inayohusika, kwa ajili ya kuwafikishia ujumbe wa suala hilo.

Mnyika ametoa kauli hiyo juzi kupitia ujumbe aliouandika katika mtandao wake wa kijamii wa mnyika.blogspot.com kwa kumtaka kila mwananchi wa jimbo hilo kushiriki kwa njia mbalimbali katika kudai maji, ikiwamo njia ya kutuma ujumbe wa barua pepe.

Alisema wakati huu ambapo Taifa linaadhimisha sherehe ya Wiki ya Maji, wananchi wa Ubungo wanapaswa kuitumia wiki hiyo kwa kuwataka wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) kuyafanyia kazi madai yao katika maeneo yao.

“Kwa nafasi hiyo natoa mwito kwa wananchi wa Ubungo na wa Jiji la Dar es Salaam kwa ujumla kwamba badala ya kuadhimisha sherehe za maji bila ya maji, kila mmoja ashiriki kwa namna mbalimbali katika Wiki ya Madai ya Maji” alisema Mnyika katika taarifa yake.

Huku akiandika anuani ya wajumbe wote wa Bodi ya Dawasa kupitia mtandao huo, Mnyika amewataka wananchi hao kushiriki katika hilo kwa lengo la kuwasukuma viongozi hao kufanya kazi ya kuharakisha upatikanaji wa maji kwa mujibu wa sheria, kanuni, mipango na mikataba.

Maadhimisho ya Wiki ya Maji yaliyoanza Machi 16 Mwaka huu, yanatarajiwa kufikia kilele chake keshokutwa huku yakiwa na ujumbe unaosema “Maji kwa Usalama wa Chakula”.

Mbunge huyo alitaka maelezo ya matokeo ya ujumbe wa mwaka uliopita uliosema “Maji kwa ajili ya Miji: Kukabiliana na changamoto mbalimbali mijini”.

Aidha pamoja na wito huo, Mnyika pia aliwataka wananchi hao kuungana kwa pamoja kuitaka Serikali Kuu na Serikali za Mitaa, kuitumia wiki hiyo kutoa maelezo kwa umma kuhusu hatua iliyofikiwa katika kutekeleza miradi ya maji na pia kuharakisha uzinduzi wa miradi iliyocheleweshwa.

Nimeitoa: HabariLeo | Mnyika ahamasisha wananchi wadai maji
 
Hali si nzuri hata kidogo UBUNGO, mbunge wangu Mh. Mnyika keshapoteza dira ingawa siipendi CDM ila nilimchangua yeye na anabakia kuwa muwakilishi wa jimbo langu, Hatumtaki hata kumsikia huku jimboni kwa sasa na ninakuhakikishia asijaribu kugombea 2015, ameimarisha chama akabomoa jimbo lake. Ngoja nikajiandae nitawaletea uozo wa mweshimiwa huyu tokea apewe jimbo hili.
 
Lazima atakuwa na shida ndio maana ana "utambulisho wa PILI" Magamba Bwana taabu kweli kweli
 
Hali si nzuri hata kidogo UBUNGO, mbunge wangu Mh. Mnyika keshapoteza dira ingawa siipendi CDM ila nilimchangua yeye na anabakia kuwa muwakilishi wa jimbo langu, Hatumtaki hata kumsikia huku jimboni kwa sasa na ninakuhakikishia asijaribu kugombea 2015, ameimarisha chama akabomoa jimbo lake. Ngoja nikajiandae nitawaletea uozo wa mweshimiwa huyu tokea apewe jimbo hili.

Huna jipya. Ukajiandae unafikiri hapa harusini
 
Magamba na chama chao bwana. wanafanya kila waliwezalo kumkwamisha kijana wa watu aonekane kama hafai.Mnyika kijana mwenzitu ALUTA CONTINUE!Uhuru wa kweli uko jirani.
 
Back
Top Bottom