Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,900
- 944
ALEXANDER MNYETI ATAKA TANGA CEMENT IRUDI KUWA MALI YA SERIKALINI
Mbunge wa Jimbo la Misungwi Mhe. Alexander Pastory Mnyeti tarehe 04 Mei, 2023 alipata nafasi ya kuchangia suala la Tanga Cement na Twiga Cement wakati wa kuwasilishw akwa hoja ya bajeti ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara iliyosomwa na Waziri mwenye dhamana Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji
"Ukiunganisha kiwanda cha Twiga Cement na Tanga Cement ushindani hautakuwepo, bei atakuwa anajipangia. Leo kule Mwanza tunanunua saruji hadi shilingi 25,000 kwa mfuko, sasa Twiga Cement akiununua Tanga Cement na kuamka asubuhi aseme leo mfuko sh. 40,000 na hakuna wakushindana, sisi walaji tutafanyaje. Naomba serikali muangalie namna ya kuokoa changamoto hii ili watumiaji wa mwisho wa saruji waweze kuipata kwa gharama nafuu" Alexander Mnyeti, mbunge wa jimbo la Misungwi
"Kwanini tunashindwa kuweka wazi, kiwanda hiki kilikuwa ni miongoni mwa vilivyokuwa viwanda vya serikali. Kule Tanga kuna viwanda viwili vya chuma ambavyo wawekezaji walishindwa kuviendeleza na serikali imevichukua, najiuliza swali dogo sana kwanini hiki kiwanda (Tanga Cement) kwa masharti hayo hayo kisirudi serikalini?" Alexander Mnyeti, mbunge wa jimbo la Misungwi