Mnawakumbuka watuma salamu maarufu redioni wa enzi hizo? Tujikumbushe kwa kuwataja...

DSC01245.JPG


Huyu ndiye Mzee Zakaria Ndemfoo wa Babati.

Wow nimefurahi sana kumon aliuwamaaufu saana. TBC wangewaalika kweny unction maalum!
 
Jamani sijaona Isomba Samaki akitajwa humu, kadi ya huyu nguli kwa siku isiposomwa zaidi ya mara 10 bado haijawa siku. Bila kumsahau Manase Mhaha (Ng'ambako) pande za Buguruni Rozana ni shughuli kubwa...
 
mazungumzo baada ya habari =Paulo Sozigwa. Alikuwepo Sango Tuwa baadae akaitwa Sango Kipozi. Mtuma salamu Thobias R. Mnyani wa Uhuru na Msimbazi
 
Last edited by a moderator:
21. Ongeza..... Sura Mbili ( nimesahau jina la kwanza maana hii ni AKA - Huyo alikuwa akituma zile salam za kuunganisha anataja watu kama 10 kama salamu za kwanza, za pili watu kama 30..nk.. alikuwa ana kipaji cha kuongea kama cherehani!

Alikuwa anaitwa TX Exaud Anaeli Nnko au Sura mbili akiwa Usariver Meru
 
Wee ndio angalau umewataja wa enzi hizo. Enzi za mawimbi ya MW na SW. mf Chivalavala wa Chivalavala wa Mahuta,Newala, Zakaria Ndemfoo wa Babat-Arusha.

Zama hizo unasikia matangazo kama vile
" Philips ndiyo yenyewe,,...sauti safi, sauti kubwa, ndiyo yenyewe." Hawa wengine wanawataja wa zama za FM. Hizi niza kuanzia 1996.
Nyuzi za JF huwa hazifi kumbe bado hii inaendelea mwaka huu tena, kulikuwa na Mnyonge Kwavira kama sikosei na Bongo Experience
 
Habari wana Jamvi.

Wale watuma salamu maharufu redioni wapo wapi mbona hawasikiki tena miaka ya hivi karibuni.

Wapo wapi Manyota top Manyota, John Msalaba a.k.a Mtumishi wa Mungu, Dogo Beka Dogo Beka na Makamanda wal Chabela Camp pale Dodoma.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom