Mnawakumbuka watuma salamu maarufu redioni wa enzi hizo? Tujikumbushe kwa kuwataja...

Habari zenu wanabodi.

Nina kitambo sana tokea niache kusikiliza redio kutokana na shughuli za hapa na pale.Bila shaka kwa wale wapenda kusikiliza redio mtakua mnawafahamu hawa watu. Nilikuwa nikipenda sana utaratibu wao wa kukumbukana kwa kupitia redio, wengine walifahamiana kwa njia hii hii ya kutumiana salamu maredioni.

Watu kama Tumbuiza Tweve aliekua akijiita Kamanda la wakinga, Lawena msonda a.k.a baba mzazi, Fikiri Dario, Top Manyota, Edward Kabamba, Zakary Ndemfoo, Mama Africa nakati Manyara, Masanja wa Kuyanja, Filbert Kiyauki, Chadela camp na wengineo wengi. Baadhi hata wamekuwa maarufu kwa kupitia njia hii.

Nilikua napenda kujua kwa wale ambao bado ni wasikilizaji hawa watu bado wanaendelea na utaratibu huo au kukua kwa utandawazi iliopelekea matumizi makubwa ya smartphone nchini imeua kabisa haka kautaratibu.
 
Mhhhhh! sikuwahi tuma salamu redioni hata kwa babu yangu, wapenzi wanakuja jibu - ila mkuu mi sijackia hii kitu mda mrefu sana
 
Thomas Mushi Kimboka
Issa Hasan Majeshi aka kamanda wa salamu
Kangomba H Kangomba.
.
.
.

Wee ndio angalau umewataja wa enzi hizo. Enzi za mawimbi ya MW na SW. mf Chivalavala wa Chivalavala wa Mahuta,Newala, Zakaria Ndemfoo wa Babat-Arusha.

Zama hizo unasikia matangazo kama vile
" Philips ndiyo yenyewe,,...sauti safi, sauti kubwa, ndiyo yenyewe." Hawa wengine wanawataja wa zama za FM. Hizi niza kuanzia 1996.
 
Zakaria Ndemfoo wa Babati

DSC01245.JPG


Huyu ndiye Mzee Zakaria Ndemfoo wa Babati.
 
wapi Sita wa Sita, Mohamedi Kiyaiyai, Kung'ombe Chacha Morema Sokare Mohiri Obare (ukipenda Mohiri Obare bwaaana!), Chesco Mzee wa Mtanda, Mzee Lawena Nsonda (ee babaaaaa!), Dismas Chabela, etc.?

Wapi Top manyota kutoka makongorosi chunya mbeya
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom