Mambo ya kuzingatia kwa mnaofanya safari za masafa marefu mwezi huu wa Desemba

Antennah

JF-Expert Member
Oct 14, 2015
6,651
8,512
Kwa mnaosafiri kwa ajili ya mapumziko ya mwisho wa mwaka, ni jambo jema, uwe peke yako au na familia yako jiandae kisaikolojia;

1. Hakikisha gari iko vizuri
2. Safiri mchana tu
3. Waza kufika salama na si saa ngapi
4. Epuka mafuta ya vichochoroni
5. Kama kwenu mbali yaani km 700 na zaidi basi safari yako unaweza kuikata vipande viwili
6. Ukiwa na wasi wasi na uwezo wako tafuta mtu ukifika mpe posho kidogo na nauli arudi
7. Kuwa makini sana unapoanza safari na unapokaribia kufika
8. Usipende kusimama porini usipopajua bila sababu au kuchimba dawa
9. Usiku ukipishana na gari punguza mwendo huku ukiibia kushoto kwako kidogo
10. Epuka kushindana na gari/mtu ambaye hata hujui anatoka na anakwenda wapi hata kama gari lake ni sawa na la kwako
11. Kama vipi andaa chakula toka kwako anayeendesha atumie vyakula vyepesi bites zaidi nyama kavu za kutafuna
12. Akili yako muda wote iwe barabarani na sio unakokwenda au unakotoka
13. Jitahidi njiani si kila mtu ajue unaenda wapi
14. Hakikisha upepo uko sahihi wakati wote
15. Hizi mvua kuwa makini ukiona inazidi tafuta mahali salama paki subiri ipungue kisha uendelee
16. Hakikisha hakuna gari lolote nyuma linakufuata kwa muda mrefu bila sababu, chukua namba kisha mpishe aende

Asante kwa kusoma ujumbe na kuuelewa.

Uwe na siku njema

Credit to "SnrDirector" from X
 
Ushauri mzuri sana. Kwa kuongezea tu; hakikisha umepumzika vya kutosha kabla ya safari. Sio unaondoka kesho saa 12 asbh, saa 7 usiku bado una pilika.
 
Wenye dhamana ya usalama baranami walipaswa kila mara kusema na wananchi , madereva na wadau wengine wa barabarani.
Kisheria, hilo ni jukumu la mbunge kwa wana nchi wake. Kuwaelewesha faida, madhara, sababu ya kulitungia sheria na hukumu yake kwa atakaye fanya tofauti.
Kwa upande wa Polisi, sio jukumu lao bali wanatusaidia tu kutujuza ila sio jukumu lao. Jukumu la Polisi ni kuchukua hatua stahiki kwa atakae kengeuka sheria iliyotungwa na mbunge.
 
Back
Top Bottom