Mnaona Akili za Wabunge Wetu?

Mrimi

JF-Expert Member
Jul 18, 2011
1,691
635
Niliposoma habari hii nimesononeshwa sana. Siamini kama sheria ya mabadiliko ya katiba kiini chake sio maslahi kwa wananchi bali ni maslahi kwa chama tawala. Kwamba sheria hii ni kukiwezesha chama tawala kubaki madarakani na kuzuia uwezekano wa vyama vingine kushika madaraka. These people can't be serious. Mimi naona hapa tunachezewa akili zetu.
 
Mkuu , umenena vyema sana......

Ila jaribu kufikiria kitu gani kimefikisha hapo....nyie endeleeni kuwaita magamba watu wenye akili timamu

wanachofanya ni vita na kuua tu, hakuna maslahi kwa taifa, walikuwa hivyo....., wako hivyo...na watakuwa hivyo......

kiburi cha binadamu kinazidi nguvu ya mauti, CCM wako hivyo....kuwarudisha kwenye ubinadamu kuna hitaji NGUVU au BUSARA!

which one are we capable to do??
 
KAMA KWENYE HOTIBA MUHIMU HUSIKII NENO "Kwa ajri yetu na Kwa ajiri ya vizazi vijajavyo " Unatgemea nini. !!!
 
Siamini watu wazima zaidi ya 200 amekosekana hata mmoja kuona umuhimu wa kujali maslahi ya umma. Lkn kitu kingine, kwani hao wapinzani nao, si ni wantanzania. Tena kuna kundi kubwa tu la wananchi linaolowaamini, kwanini wanyimwe haki yao. Binafsi sioni tatizo la upinzani kuongoza, maana hata wao wakikiuka makubaliano yetu, katiba itatumika kuwawajibisha. Hawa jamaa wasitake kutuaminisha kwamba katiba mpya itawanufaisha wapinzani, maana hata wao ipo siku wanaweza kuwa wapinzani, so sioni sababu ya wao kuweka mikingamo ktk jambo hili ambalo kimsingi lina maslahi kwa watanzania wote.
 
Toka lini CCM wakajua BUSARA? Bila kuwatoa NDUKI hawatoki na ndio maana Kipanya anasema "Watanzania hata ukiwaingilia wake zao hawatatoka kuja mtaani"!!Tulirogwa na sheikh Yahya na alisahau kumuachia mwanae dawa ya kutuzindua.......na hivyo tumeliwa!!
 
Nimewai kusema hapa JF kuwa CCM.Bunge,CUF,NCCR ni majanga ya kitaifa....
 
Mswaada unakwamishwa eti kwa sababu Kikwete kakubaliana na matakwa ya chadema, makubwa, kumbe humo bungeni wao ccm huwa wanatetea maslahi ya nani??????????? Tumuulize Bana
 
Siamini watu wazima zaidi ya 200 amekosekana hata mmoja kuona umuhimu wa kujali maslahi ya umma. Lkn kitu kingine, kwani hao wapinzani nao, si ni wantanzania. Tena kuna kundi kubwa tu la wananchi linaolowaamini, kwanini wanyimwe haki yao. Binafsi sioni tatizo la upinzani kuongoza, maana hata wao wakikiuka makubaliano yetu, katiba itatumika kuwawajibisha. Hawa jamaa wasitake kutuaminisha kwamba katiba mpya itawanufaisha wapinzani, maana hata wao ipo siku wanaweza kuwa wapinzani, so sioni sababu ya wao kuweka mikingamo ktk jambo hili ambalo kimsingi lina maslahi kwa watanzania wote.

Namuona Ndungulile,kigwangala wasiemtaka na makamba kwambaali mzee wa kimasai sendeka waliobaki vilaza na maslahi.
 
naona sasa viongozi wetu wa chama cha mama wanavyozidi kuwa machizi na kuwa na upungufu wa akili,,, nafikiri iko siku watajutia haya wanayoyafanya... kiuhalisia wanataka kuendelea kujinenepesha katika nafasi zao na familia zao wakati watanzania walio wengi wanaendelea kuteseka katika lindi la umaskini,,, kiufupi wamepotoka ijapo wana akili zao ambazo ukimchukua daktari wa mirembe atasema kuwa wako normal........ kwa kweli ndoto za tanzania niliyokuwa naiwaza na kusema kuwa nitakupenda kwa moyo wangu wote sasa inapotea....
 
JK ajitokeze hadharani aseme kuwa hayo marekebisho ni ya msingi kwa manufaa ya taifakisha awaambie wanaccm wenzake kupitisha au kutopitisha ni juu yao na hata wakitaka wampigie kura ya kutokuwa na imani naye..yeye anawe mikono. Huo ndio ushauri wangu kwa mh. Raisi. Mungu ampe hekima kuu majira haya.
 
watanzania walio wengi ni wagumu kuelewa na wepesi kusahau. 2015 wasirudi hao magamba.
 
Back
Top Bottom