Uchaguzi ndiyo kipimo cha juu cha ukomavu wa Wanasiasa/ Viongozi wetu

El Roi

JF-Expert Member
May 29, 2020
263
502
Jambo ambalo sijalifahamu kwa kiwango kikubwa huwa ni kwanini suala la uongozi ukitaka " madaraka" huwa ni suala la kufa na kupona kwa nchi nyingi za kiafrika.

Mtu mmoja aliwahi kuniambia kwamba siasa za kiafrika za kimadaraka huwa haziendi zaidi ya matumbo yetu, akiwa anamaanisha kwamba " siasa za kiongozi afrika, ni Ili mtu ale na kupata faida zake.

Pamoja na wasiwasi wote ambao nimesikia watu wakichambua siasa katika Africa, kwa utu uzima wangu, nimegundua kwamba siasa za kiafrika ni kukaa madarakani tu na si zaidi.

Nimeangalia kwa makini kinachoendelea hapa nchini kwa kile kinachoitwa urejeshaji wa demokrasia na haki za watu.

Hakika " siasa za kiafrika huwa haziendi zaidi ya matumbo, na mbwembwe nyingine zote za haki na demokrasia huja kabla ya uchaguzi tu.

Sasa naamini kwamba viongozi wetu huongea haki na demokrasia kama suala la kutuliza watu na joto tu la siasa, Ili mtawala/ watawala wapate muda wa utulivu kufanya mambo yao.

Kizungumkuti kinachoendelea Sasa kwenye maboresho ya sheria na yote yanayoitwa maridhiano ni kiashiria tosha Cha kipimo kwamba " demokrasia na haki za watu huwa ni kabla ya uchaguzi tu katika Africa.


Kwa kuwa homa ya uchaguzi imeanza nchini, inachekesha kuona miswaada inayokwenda bungeni ambayo inatafuta democratic space.!!

Kila kilichotengenezwa ni kusaidia watawala kubaki madarakani.

1) Hivi kweli Rais mgombea anateuwa bado mwenyekiti na makamu wa tume ya uchaguzi na bado eti watu wanaona wako sawa?

2) wakurugenzi wa halmashauri bado wanapigiwa chepuo na marekebisho Ili wawe wasimamizi wa uchaguzi. Kweli?

3) Nchi yenye miaka 60 na zaidi ya uhuru bado ina sheria inayoruhusu Kutopinga matokeo ya urais mahakamani ? What primitivity is this? Nakadhalika na kadhalika.

Kuna wakati niliwahi kutoa maoni hapa juu ya CCM vs Mhe. Rais. Na maoni yangu yalikuwa kutilia shaka kama kweli kile Rais anachoita 4R kingefanikiwa. Nilijua kwa hakika kwamba CCM ni chama ambacho kimeshalewa madaraka na wimbo wanaoujua ni kutawala tu. Nje ya madaraka hawajui maisha mengine. Nilijipa moyo kwa Rais na hayo mabadiliko aliyotaka ku introduce , lakini nilijua ni mtu mwenye ujasili tu kama wa Magufuli ndiye angeweza kuwafanya CCM wakubali mabadiliko chanya ya ujenzi wa demokrasia na maendeleo ya watu.

Nilionyesha mashaka kama Rais angeweza kubadilisha fikra za waccm, wajali haki za kimokrasia za watu wengine, na wasahau madaraka kweli?

Hiyo Sasa imedhihiri, mbwembwe za haki, demokrasia kwa watu wote kwa usawa, huwa ni mbwembwe kabla ya uchaguzi tu.

Viongozi wa kiafrika katika yote wao hujua madaraka tu. Wanapenda kuongoza wao pekee, wanajimilikisha hati ya kutawala wenzao daima kana kwamba waliteuliwa na Mungu kufanya hivyo.

Tuache kujisifu kwa lolote, Afrika ni madaraka na madaraka ndo ulevi wa waafrika.

Mungu atuinulie kama Hilo linawezekana kwake " viongozi walio juu ya matumbo yao" . Wanaoweza kufikiri haki za watu objectively na wako tayari kupoteza hata hayo madaraka in right course".

Nimesikitishwa na ngonjera na michezo ya chama tawala hapa kwetu. Any way labda inafanyika hivyo Ili kunithibitishia kwamba " uchaguzi ktk Africa ndo kipimo Cha juu Cha kujua wale wanaojiita waleta haki, warudisha demokrasia, wajenga maelewano Tena na waleta uvumilivu.

I am completely disappointed.
 
Kaka Afrika hii hakuna mtu anaqualify kwenda kwenye nyumba ya ibada.tunachokifanya ni ujinga mala 10000
 
Back
Top Bottom