Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 879
- 4,125
Mhe. Rais amefanya jambo kubwa sana kufungua milango upya kwa watu kuja Tanzania . Alikuta nchi imefungwa, tulikuwa kisiwani na sasa amekwenda kuwaleta wageni na kutusaidia watanzania tukubalike huko nje.
Watanzania wanaokwenda China, Uturuki, Dubai, Malaysia, Ulaya na America ni wengi kipindi cha mama kuliko kipindi cha JPM. Means exposure inaongezeka. Tunapunguza idadi ya illiterate katika eneo la diplomasia ya kimataifa. Tulizoeshwa kwamba kupanda ndege ni anasa. Leo hii mama ametufungulia njia tunaweza kupanda ndege bila kukutana na vikwazo tuendako. Tunapaswa kumpongeza sana.
Royol tour imewashtua majirani zetu na kuwafanya watamke visa free bila hata kufanya maandalizi , hizi zote ni juhudi za mama. Nitakuwa mnafiki nisipokiri hapa kwamba mama amefanikiwa kuturejeshea uhuru wa kimataifa muda mfupi baada ya sisi kuupoteza.
Aidha, zipo changamoto kubwa zinazokwamisha mama katika kukuza uchumi na mahusiano ya kiuchumi. Nitataja baadhi
1. Wafanyakazi wengi wa wizara ya maliasili na utalii hawamwelewi mkuu wa nchi. Mfano jana tumeona kwenye mitandao wafanyakazi huko Serengeti wanazuia watalii kuendelea na ratiba zao kisa wanataka wakusanye dola hamsini kwa makampuni ya utalii ambayo wanafahamu ofisi zao zilipo na kwamba wakiwapa hills mifumo ya TEHAMA aliyoweka mama itawatambua kama wanadaiwa bila kuathiri utalii. Anatakiwa kwa kitendo kile amfute kazi waziri mwenye dhamana na watendaji wa hifadhi ili next time wajifunze kutoa huduma kwa kuzingatia mazingira kabla ya wageni walioathirika awajaenda kutangaza vibaya huko Duniani.
2. Watendaji katika viwanja vikubwa vya ndege vya Julius Nyerere, KIA na Abeid Aman Karume wamejaa uaskari zaidi kuliko utoaji huduma. Watendaji wasiovaa uniform katika viwanja hivi na wasiokuwa na nametag ni mzigo kwa Taifa. Wanavyotoa huduma ni kama wao ndio wamiliki wa nchi na kwamba wao wasiposema uingie au utoke hautatoka. Viwanja bmvikubwa vyote ikiwemo hata Ethiopia hakuna huu ujinga wakujaza unskilled labour uwanjani. Hakuna ujinga wakuruhusu afisa asiye na uniform Wala name tag kusumbua wageni. Waondoleeni haya mamlaka hawa viumbe wageni wawe na amani kuja tena
3. Mhe. Rais anatafuta wawekezaji lakini mawaziri na watendaji wanaosimamia uwekezaji wamekaa kijeshi zaidi. Hawana moyo wakupunguza usumbufu wa huduma kwa sababu ya rushwa. Kila mtu ni bosi kwenye ofisi yake na hakuna uniformity wala ufuatiliaji wa muda wa utoaji huduma.
4. Mawaziri wa kisekta ni mzigo kwenye eneo la kusisimua uwekezaji. By nature mawaziri wa Tanzania siyo watu wakukaa ofisini lakini pia kila siku wanabadilishwa . Pamoja na hayo mamlaka walizojiwekea mawaziri wamekuwa miungu watu kwenye wizara. Mfano waziri wa uwekezaji asipoamua kupitisha vibali au waziri mwenye dhamana na ajira asiporuhusu appeal za ajira kwa wageni zisikilizwe na atoe maamuzi mtakesha. Mhe. Rais rejesha mamlaka za utoaji huduma kwa Makatibu wakuu. Mawaziri wabaki kufuatilia utekelezaji na kama standards zinafuatwa.
All In all nimpongeze mama kwakuifungua nchi sasa hivi Tanzania siyo kisiwa tena