Mmiliki wa website ya unitedrepublicoftanzania anapotosha kuhusu Kabila la Wabena au jamii ya wabena?? Tutake radhi

Mgosi Mbena

JF-Expert Member
Nov 28, 2023
308
428
Wabena ni kabila la watu wenye akili sana wanaopatikana tanzania mkoani njombe.
Idadi yao ni takribani milion 1 na kitu…..(makadirio) pia kabila hili linapatikana mikoa jirani kama morogoro ,Iringa ,Ruvuma.

LAKINI PIA AFRICA NCHINI ETHIOPIA
Kuna kabila linajiita Bena (Bannaa) wanaishi katika Bonde la Omo valley.Sijui historia vizuri kama haya makabila mawili yana uhusiano lakini najua ni makabila yanayopatikana nchi mbili tofauti tena ambazo hazina ukaribu na mipaka.

NARUDI KWA HII website ya unitedrepublicoftanzania.com Katika hali ya kushangaza au kustajabisha website hii imejikuta ikitumia picha za Ethiopia au wabena wa Ethiopia kuelezea kabila hili la wabena wa tanzania.


NAJUA HII NI WEBSITE KUBWA ningependa kupata maelezo yaliyonyooka nini kinaendelea?? Wanatumia au wametumia kima kosa?? au mm ndio sielewi?? Na kama wako sahihi wanaweza kuelezea hiyo picha ambayo ndo wameweka ikiwakilisha wabena waliipiga wap ?? mwaka gani?? sehemu gan ? Je kuna mbena wa hivo??

NB: Yawezekana ni mkanganyiko wa mitandao lakini pia nina imani kubwa picha ni ya Ethiopia,,,Kama siko sahihi nirekebishwe nami nitaomba msamaha.
 

Attachments

  • 5ED6E52C-AAE6-49F8-AF4C-AC4F38B57FEB.jpeg
    5ED6E52C-AAE6-49F8-AF4C-AC4F38B57FEB.jpeg
    1.4 MB · Views: 2
  • 08B705B3-A7F5-4577-AA43-97D840D03EFC.jpeg
    08B705B3-A7F5-4577-AA43-97D840D03EFC.jpeg
    627.6 KB · Views: 2
  • 8F4D6BAE-4B0F-4D77-94BD-E0EA9841ADB5.jpeg
    8F4D6BAE-4B0F-4D77-94BD-E0EA9841ADB5.jpeg
    1 MB · Views: 2
Back
Top Bottom