Mmh !! Nimemaliza mtihani wa kwanza ila huu sasa !!

Hujasema kisa ni nini?

Ushauri tu, ukishaoa, main woman anapaswa kuwa mkeo. Mama yako ana mume wake, amuache mkwe wake na mume wake
 
Kwann wagombane? Maana yake umewaweka karibu katika mambo fulanifulani yanayofanya wakutane mara kwa mara hatimaye ugomvi... nyie ni watoto, kaa na mkeo apunguze namna zote za kukutana na mama mkwe wakwe isipokuwa kwa sababu kubwa zisizokwepeka na hata ikiwa hivyo ajitahidi kutokuwa nae ana kwa ana yaani salamu tu baada ya salamu ajichanganye kivyake na wengine. Kama kuna biashara wapo pamoja basi mwondoe mmoja ashikirie mmoja. Haya majibizano yataisha na yatapungua,
Asante cna, sehemu anapkaa Mama Yangu unapanda dala dala kufka Huko na mimi Ndio Niko karibu na Mama yangu Ndugu zangu wengine wapo nje Ya mkoa huu. Hivyo mara nyingi mimi Ndio Nategemewa kwenda kumsabahi mara moja moja ukizingatia ni mjane
 
Kila mmoja na nafasi yake. Kuwa na msimamo. Tambua kuwa mama ndie mlango wako wa kuingia peponi, ila kuwa muadilifu kama anamuonea mke simama kidete na umtetee mke na hali kadhalika kama mke ni mkosa mwambie. Na uwe mvumilivu na jitahidi kutumia lugha nzuri na adabu ya hali ya juu mwisho wa siku watakuelewa tu.
Habarini !! Tayari nilifanikiwa kupata mke miaka miwili sasa na mtoto juu, ila Mke na Mama yangu hawaelewani kila cku maneno mke hamsikilizi mama kwa chochote ukifka kwa mama naye malalamiko, nilishawahi kumkanya Kidogo mke kuwa mvumilivu na Mama yangu lakini imeonekana kuwa ngumu, ingawa hatukai karibu na Mama yangu ila mkoa ni mmoja bado inakuwa issue, Embu nishaurini wale walio kwenye ndoa huu Mgogoro utaisha kweli !? Maana mke namtaka Mama namtaka
 
Hamuishi pamoja lakini migogoro haiishi. Uende kumtembelea mama yako pekee yako na mara chache sana unakwenda na familia hata mama yako apunguze kufika kwako yote hayo kupunguza ugomvi. Wanawake wakiwa pamoja hawaachi kugombana
Asante, sana kwa ushauri Nitajitahidi
 
kwa hiyo ndo maisha hayo, maana kipindi cha nyuma kuna Mzee mmoja aliwahi kuniambia hao kuna kitu wanagombania sasa cjui Nini mpaka leo Cjajua
Wanagombania upendo wako

Bila kujua, kwa mmoja utabaki kuwa mtoto wake na kwa mwingine utabaki kuwa mme
 
Hongera kwa kuwa mchawi mkuu
Ukishindwa kutatua mgogoro wa mke wako na mamako bado wewe mvulana !!!karibu chama chetu Cha ubachelor.mama ako umekanae muda mrefu ukishindwa kujua tabia yake ili uoe mwanamke anayeweza kuendana na tabia yake .mfano mimi familia yetu ni wachawi lazima nioe mchawi ili tuoane kivyote ,Mambo popompo Kama haya ndio badae yanaleta mchwererere kwenye familia.
 
Suluhu ya tatizo ni kukaa nao wote wawili kwa pamoja na uanze kuhoji kila mmoja ana tatizo gani. (Mwanaume aliyekamilika tu ndo ataweza kuendesha hichi kikao) usikilize kila upande na ufanye mamuzi bila kuegemea upande wowote...

Likishindikana hilo basi hamieni mkoa mwingine kabisa, muwe mnaonana mara moja kwa mwaka hakutakuwa na ugomvi
 
Ukiwaweka chini wote kwa pamoja hlf mama akaonekana na makosa hatapenda ukimwambia ukweli. Cha kufanya Ni mke wako amuelewe mama mkwe wake. Binafsi Sina story Wala mazoea na mama mkwe maana namfahamu vzr, ninachofanya ni kukaa nae mbali, naongea nae ikibidi, natekeleza majukumu yangu napita hivi ..
 
Hapo mmoja ajishushe tu Hamna namna..la sivyo ugomvi hautaisha milele

Na wakujishusha ni mkeo..
 
Hujasema kisa ni nini?

Ushauri tu, ukishaoa, main woman anapaswa kuwa mkeo. Mama yako ana mume wake, amuache mkwe wake na mume wake
Ukweli mama yangu ni muongeaji cna na ni mtu wa fact yaani yeye hapindishi ukweli ni ukweli na sisi tumelelewa hivyo nakumbuka kipindi cha uchumba kuna kipindi Wife alipitiwa kidogo mama alimuita na kumkanya waziwazi basi toka kipindi hicho mke hamkubali kabsa nilishawahi kumwambia toka cjamuoa kuwa mama yangu yuko Hivi Akasema Sawa nitaweza kukaa nae maana yeye hakopeshi na tena nilishawahi kumkanya na kumwambia mama yangu Huyu ni Mjane na mimi Ndio Niko karibu nae mkoa huu kumuangalia naomba umvumilie naona mziki ni ule ule tu tena ukimwambia Ndio anakumbushia yale ya nyuma
 
Acha mke brother!!! Yalinikuta kama yakwako,ukiona mwanamke anashindana na mama mkwe wake jua si mke ni ibilisi,achana nae kaka,utakuja nikumbuka,yalinikuta hayo,msikilize sana mama yako,Hakuna mzazi asiyependa mwanae awe na furaha,ukiona anaongea jua kuna tatizo hapo
Pole sana Chifu, yalikukuta yapi Kaka?
7bu ukitudokeza tutajifunza nasi namna ya kukabiliana na majanga kama hayo Kaka.
 
Ukishindwa kutatua mgogoro wa mke wako na mamako bado wewe mvulana !!!karibu chama chetu Cha ubachelor.mama ako umekanae muda mrefu ukishindwa kujua tabia yake ili uoe mwanamke anayeweza kuendana na tabia yake .mfano mimi familia yetu ni wachawi lazima nioe mchawi ili tuoane kivyote ,Mambo popompo Kama haya ndio badae yanaleta mchwererere kwenye familia.
😂😂😂😂😂 Mkuu umenifanya nicheke, nimesoma na jina lako umenifanya nihisi unaweza kuwa Mchawi kweli aiseee.
 
Pole sana Chifu, yalikukuta yapi Kaka?
7bu ukitudokeza tutajifunza nasi namna ya kukabiliana na majanga kama hayo Kaka.
Elewa tu kaka,mwanamke yoyote anayeshindana na mzaziwako huyo hana adabu,Hata kama mama atakuwa na makoso,japo naamini siokweli,mana mama anajua furaha ya mwanae ni mke mwema kwahiyo kama mkeo angekuwa mwema mama asinge thubutu kukuharibia furaha yako.Hapo mwanamke huna,kama anauwezo wakukingiana kifua na mama yako,vipi kwa upande wako wewe mwenyewe?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom