Mmh Nape anazidi kumbomoa Lowassa

Indume Yene

Platinum Member
Mar 17, 2008
2,950
711
Sina comment kuhusu aliyoongea Nape, sikiliza.

[video=vimeo;31668596]http://vimeo.com/31668596[/video]
 
The link you have provided does not respond. Unaweza turekebishie tuskie?
 
Sina comment kuhusu aliyoongea Nape, sikiliza.

[video=vimeo;31668596]http://vimeo.com/31668596[/video]

Wewe, kama great thinker, dadavua alichoongea Nape ili watu wachangie. Unaposema huna comment unatarajia nani atakuwa na comment sasa?
 
Anambomoa kivipi, kwani Lowassa ni kibanda? Kwanini aende kuongelea vichochoroni kama kweli amedhamiria anachokiongea. Kuna runinga ya TBC 1 na redio ya TBC Taifa zinasikika nchi nzima hakuziona hadi aende kujifungia maliwatoni na kuongea? Kama amekutuma mwambie aache unafiki.
 
Mbona hajavaa manguo yale ya kijani, au kwakuwa yale Manguo ni ishara ya ufisadi anaogopa FBI wakimuona na yale manguo watamdaka? Hana lolote zaidi ya kujiongezea kipato kwa kukamata Per Diems ndefu za ughaibuni...
 
Wewe, kama great thinker, dadavua alichoongea Nape ili watu wachangie. Unaposema huna comment unatarajia nani atakuwa na comment sasa?

Si lazima nitoe comments kwa muda wako unaoutaka wewe. You need to cool yourself off.
 
Hizi interview za kufanyia sebuleni kwa watu ni kujitia aibu kama katibu mwenezi wa chama kinachopoteza umaarufu kwa kasi kuliko vyote duniani.
 
Eti anadai mimba ya kumzaa yeye Nape ilitungwa wakati CCM inaanzishwa...

Eti atasema ukweli daima FITINA KWAKE MWIKO...

Ina maana siku ile mlipotuhonga hela kuhudhuria mkutano wenu wa Mwanza sio fitina? Kusema utashikisha watu ukuta sio fitna hiyo?
 
Eti wameinua kioo watu wajiangalie na kulala mbele wenyewe...

Kamnyima kazi mzee wa propaganda kwa kukifuta kitengo cha propaganda. Huyo jamaa ana roho mbaya sana, sasa Tambwe Hizza atakula wapi?
Mkianzisha vyuo vidogo vya chama wilayani, nani atahudhuria hivyo vyuo na kuvaa yale manguo ya kijani?
 
Vita vya Magamba.......,furaha kwa CHADEMA.Viva CHADEMA!
 
Wewe, kama great thinker, dadavua alichoongea Nape ili watu wachangie. Unaposema huna comment unatarajia nani atakuwa na comment sasa?
Kuiweka humu pekee ni mchango tosha. Halafu hili neno jamani naliona sio kabisa.
 
Yote anayoyaongelea ni kama hayatekelezeki na alivyo kichekesho anashindwa kuwataja watu majina kwa hiyo mleta mada nawe umetumia vibaya jina la Lowassa kwa vile Nape ameogopa kutaja hilo jina kuwa linatakiwa kujivua gamba
 
Nani anahusika na Rada watu watataja jina, Richmond ni ya nani watu watataja jina... Sasa wewe Nape mbona hautaji?? Mfitini mkubwa, kama uko serious na kujivua gamba taja kabisa sema Lowassa jivue gamba, Chenge jivue gamba. Sio kusema kwa mafumbo. Anaongelea usaliti wa chama wakati naye alianzisha CCJ...
 
Sijasikia hiyo interview, lakini basing on the headline, naomba Nape afahamu kuwa Lowassa ni mmoja wa watu wenye nguvu kubwa ndani ya CCM. Kwa hakika, hata Kikwete hana nguvu ndani ya CCM kulinganisha na Lowassa. kwa hiyo, jitihada zozote za kutaka kumbomoa Lowassa ndani ya CCM, ni kuibomoa CCM yenyewe
 
Wewe, kama great thinker, dadavua alichoongea Nape ili watu wachangie. Unaposema huna comment unatarajia nani atakuwa na comment sasa?
Tuondelee viji amri amri vyako vya kikurya hapa
 
Back
Top Bottom