Mmepoteza Ubunge kwanini bado ninyi mawaziri?

Mbona we mwenyewe hukuchagua maneno kwa uangalifu? Utasemaje mwanamke tumchukulie taratibu kwa vile ana udhaifu ulioonyeshwa kisayansi? Huo kwanza ni uongo mkubwa, ni mchemko mkubwa, na huwezi kuthibitisha tafiti uliyofanya ukang'amua kwamba mwanamke kaumbwa dhaifu.

Tumsifu na kumkosoa Mtema bila kujali jinsia yake.

Tindikali;

sio lzm utumie maneno ya hovyohovyo kama ulivyoandika hapo juu ndipo uwasilishe ujumbe wako;kwangu mimi mtu unaeleweka vyema zaidi kama utatumia lugha ya kiungwana!Ungeniuliza kwanza niwasilishe wapi nimeyapata haya maneno kabla ya kunihukumu kama mie ni muongo mkubwa!

Unaweza ukaenda kusoma kuhusu "automatic and effortful encoding"inayoeleza wazi kabisa utofauti wa mwanamke na mwanamme kukabiliana na "emotions".Kwa mfano mimi binafsi nimeweza kukabIliana na lugha yako ya hovyohovyo na naongea na wewe hapa bila jazba;kwa mwanamke "inawezekana" wakashindwa kukabiliana na maandiko kama haya yako kwa sababu ya nature ya 'limbic size' yao na uwezo wao wa kushindwa kuidhibiti 'amygadala'

Tindikali;kama nimekosea kuhusu andiko la Regina nisamehe!
 
Gaijin;

Hakuna sehemu kwenye andiko langu nimesema akina mama wasikosolewe;kwenye andiko langu nimesemea umuhimu wa kuchagua maneno kwa uangalifu unapoandika au kuongea chochote kuhusu mwanamke,nikaongelea hata kuhusu Obama vs Clinton kama mfano hai!

Gaijin;

Pole sana kama andiko langu lilikukwaza lkn sikuwa na maana hiyo ndugu yangu!

umesema yachaguliwe maneno ya kuambiwa kwa kuwa wanawake wana inferiority complex.....................sasa hapa mkuu mwanamke mwenye 'kuweza' unataka alichukuliaje hili?

tunapotaka kukosoa viongozi wetu hasa watarajiwa lazima tusahau jinsia zao................kama maneno makali mno yasitumike ni kwa jinsia zote sio tutoe upendeleo maalum kwa wanawake...............kuzaliwa mwanamke hakutakiwi kumpe mtu easy ride. Mwanamke asiyeweza kushindana kwenye ulingo usio tambua jinsia ya mtu na agombee nafasi za viti maalum vya wanawake.
 
Kiranga,Mwanakijiji na wengineo Male-oriented society;

Tuwe kama tu Rais Obama ambaye hata siku moja hakumshambulia jukwaani Mama Clinton kwenye kampeni zake ingawaje mama huyu aliongea sana negative kuhusu yeye hata akaileta hadi ad ikiita "3 am in the morning"ikimuonyesha eti Obama atakuwa legelege kama akija kuwa Rais.

Tuwe tu kama Rais Obama ambaye hadi leo hasemi chochote negative kuhusu mashambulizi ya kila siku yanayoletwa kwake na mwana mama Sarah Palin;tumuige hata Makamu wa Rais Biden ambaye kwenye mdahalo wake na Mama Palin alijizuia kabisa kumjibu vibaya Mama mbwatukaji Sarah!

Kiranga ndugu yangu,akina mama wana udhaifu wao hasa wa inferior-complex na study nyingi za physiology zimeonyesha hivyo,cha kufanya ni kupunguza makali ya maneno dhidi ya mgombea Regina hata kama kaandika kinyume na mategemeo yetu;kwa hili namsifu sana Mwanakijiji kwa kukabiliana nalo hasa kwa kukaa kimywa hadi sasa kufuatia andiko la dada Regina lililomdhihaki waziwazi kabisa!

Dada Regina endelea kupambana na kampeni zako,nina uhakika unaweza kushinda na kubadili mamabo mengi sana Bungeni;mm binafsi nipo tayari kwenye upande wa strategies nikitakiwa kufanya hivyo!

Asanteni sana bandugu na bajamaa!

Asante sana Malafyale,nimekupata.
Kuhusu Mwanakijiji naomba nieleweke sikumaanisha ambavyo imeeleweka na wengi humu.Namheshimu Mwanakijiji kuliko mtu mwingine yeyote ndani ya JF,natambua mchango wake katika taifa hili hata kwangu pia as an individual,namuomba radhi kama nayeye atakuwa amenielewa vibaya.Hata Ilani yangu ya Jimboni imekuwa polished na yeye.

Mwanakijiji kama na wewe umenielewa vibaya na kukwazika kwa hili ninaomba unisamehe sana.

Naanza kuona machungu ya kutumia jina halisi wakati huo ukiwa na maadui ambao siwafahamu wala sijui niliwatengenezaje.Nachelea kutolitumia tena jina hili na hii itakuwa ni post yangu ya mwisho kwani kama mwanadamu mwenye moyo,mwili na nafsi nakwazika ninaposhambuliwa bila sababu za msingi na hasa watu wenyewe siwajui ni kina nani.
Kila pande inamwona mwenzake ana makosa hivyo sio rahisi kufikia muafaka.Niko kwenye kipindi kinachohitaji uvumilivu wa hali ya juu lakini kama mwanadamu nashindwa.

Kwaheri friends.
Kwa heri Kiranga na timu yako Tindikali na Gaijin napenda kuwaambia kuwa Jimbo ninashinda na mjengoni nitakwenda,hii ni ndoto yangu na lazima itimie.

Malafyale nitakutafuta.

Aluta Continua

Regia Mtema
Mgombea Ubunge-Kilombero(CHADEMA)
 
Wewe mtu anakutukana wewe pamoja na jinsia yako yote kwamba "akina mama wana udhaifu wao hasa wa inferior-complex" na wewe sio tu unakubali, bali pia unamshukuru !

Huyu mtu ana akili kweli huyu ? Huyu si anaaibisha wanawake tu, kwamba wanawake hawawezi kupigania haki na ni watu inferior wanaohitaji kuwa patronized na wanaume.

Ndivyo unavyoamini hivyo? Kwamba wanawake ni inferior ?

Na bungeni nako unataka kwenda kukubali motions bila kuzichunguza hivi hivi ? Hivi huu ndio umakini tunaotaka bungeni huu ?

Wewe bungeni utaota ndoto tu, uende kwa uwezo gani ulio nao ? Umesema vizuri kwamba unaota, utabaki unaota tu, kwa mtaji huu hata rafiki zako una wa alienate, utaenda bungeni bila kujua ku form simple alliances ?

Utaenda bungeni kwa spirit hii ya kukatishwa tamaa na kukimbia kila unaporushiwa makombora? Si utaenda kujiuzulu hata huko bungeni kama Sarah Palin wewe? Waandishi wa habari, ambao washaanza kunusa harufu ya kwamba wewe ni mtupu na huna kitu, wakitaka kukuandama zaidi ya Kiranga, utaweza kuendelea na kazi waliyokutuma wananchi wewe ?
 
Kiranga,Mwanakijiji na wengineo Male-oriented society;

Tuwe kama tu Rais Obama ambaye hata siku moja hakumshambulia jukwaani Mama Clinton kwenye kampeni zake ingawaje mama huyu aliongea sana negative kuhusu yeye hata akaileta hadi ad ikiita "3 am in the morning"ikimuonyesha eti Obama atakuwa legelege kama akija kuwa Rais.

Tuwe tu kama Rais Obama ambaye hadi leo hasemi chochote negative kuhusu mashambulizi ya kila siku yanayoletwa kwake na mwana mama Sarah Palin;tumuige hata Makamu wa Rais Biden ambaye kwenye mdahalo wake na Mama Palin alijizuia kabisa kumjibu vibaya Mama mbwatukaji Sarah!

Kiranga ndugu yangu,akina mama wana udhaifu wao hasa wa inferior-complex na study nyingi za physiology zimeonyesha hivyo,cha kufanya ni kupunguza makali ya maneno dhidi ya mgombea Regina hata kama kaandika kinyume na mategemeo yetu;kwa hili namsifu sana Mwanakijiji kwa kukabiliana nalo hasa kwa kukaa kimywa hadi sasa kufuatia andiko la dada Regina lililomdhihaki waziwazi kabisa!

Dada Regina endelea kupambana na kampeni zako,nina uhakika unaweza kushinda na kubadili mamabo mengi sana Bungeni;mm binafsi nipo tayari kwenye upande wa strategies nikitakiwa kufanya hivyo!

Asanteni sana bandugu na bajamaa!

Male oriented society inajionyesha kwa nani hapa?

Ni mimi ambaye nawaona wanawake ni sawa na wanaume na wanahitaji kupewa challenge sawa bila kuangalia kwamba wao ni wanawake au wewe unayesema wanawake ni viumbe dhaifu wanaohitaji kuonewa huruma na wanaume ?

Nani mwenye mfumodume hapa ?
 
Huyu dada kaanza kutangaza anagombea ubunge bila kutaja jimbo wala jina lake, akawa anataka kuleta biashara za kutuuzia mbuzi aliye katika gunia, watu makini tukakataa na kumweleza kwamba ukishasema unagombea ubunge huna budi kutangaza jina lako na jimbo, kama hutaki kutangaza, usiseme chochote.

Akabisha kama mtu ambaye haelewi the very basic principles of public service, kwamba ukishataka kazi ya kuwahudumia watu katika siasa, huna privilege ya kutaka kutojulikana, ukitaka kufanya hivyo wengine tutafikiri una jambo unaficha au hujiamini, au vyote.

Nikashikia bango hili, mpaka akakubali kujitaja. Alivyojitaja akawa anataka kuchukua credit kwamba kajitaja, kama vile kajitaja kwa kutaka mwenyewe na si kwa preessure ya watu. Nikamwambia ukishalazimishwa kufanya kitu huwezi kuchukua credit, umelazimishwa. Akatuonyesha tena asivyo organized, akasema kaamua kutaja jina lake mwenyewe bila kulazimishwa, na alijitaja siyo kwa pressure yangu, bali kwa kuambiwa na watu fulani waliomshawishi (contradicting her first position). Hata hivyo akaendeleza usiri wake na kukataa waliomshawishi katika PM hapa JF ni kina nani, na hivyo kutufanya wengine tuhisi hakuna mshawishi kwenye PM wala nini, ni utunzi wa hadithi za ku "save face" tu. Usiri siri unatupa watu sababu ku suspect uongo ongo.

Alipojitaja akajionyesha kwamba hata anapoamua kufanya jambo zuri, hawezi kulifanya vizuri - hata mazuri nayo yanaweza kufanywa vizuri au vibaya- akaenda kututajia historia ya maisha yake yote mpaka vitu ambavyo havina relevancy katika uchaguzi huu, ikawa anajitaja kama anatafuta mtu wa kumuoa wazae watoto. Akajionyesha hana kiasi na hajui proportion, wala hana priority, anapokuwa msiri anaficha kila kitu hata jina humjui, anapoamua kujitaja anakutajia mpaka vitu vya ndani kabisa ambavyo hatuhitaji kuvijua, too much informatiopn. Anajionyesha asivyokuwa na exposure.

Listi inaweza kuwa ndefu, lakini kama unaona namuonea na chochote atakachofanya nitaona makosa, hili linatokana na ukweli kwamba chochote atakachofanya anafanya kwa makosa. Juzi kaja hapa kajionyesha tena kwamba hana tact, akitaka kujionyesha muwazi katoa mambo yao ya ndani kabisa chamani, na kuanzisha confrontation na mwanachama mwenzake Kitila Mkumbo basically akimuita Kitila muongo anayepotosha mambo hapa JF, bila ya kuwa na sababu ya msingi ya kusababisha confrontation hii. Bahati nzuri Kitila kauchuna, maana angeamua kujibizana na huyu wangewapa faida watu. Regia akajidai uwazi hapa na kusema huo ndio msimamo wake, baadaye akafuta maneno yake na kujionyesha hana msimamo. Flip flopping, tena hata bila kueleza kwamba kabadili mawazo.

Kwa kifupi ndiye mtu wa aina hii, incoherent, msiri msiri, mnyemela nyemela etc. Wanasema King Midas kila alichogusa kiligeuka dhahabu, huyu dada kila anachoguza kinageuka kinyesi.

Ndiye mbunge mtarajiwa huyu ? Hata watu kama kina Tundu Lissu na Mnyika washaanza kumshtukia na kum diss by her own admission aliyopost hapa JF.

Naona nyie mmetoka mbali.
 
Tindikali;kama nimekosea kuhusu andiko la Regina nisamehe!
"Kama nimekukosea..." Kama hujui kama umekosea huhitaji kuomba msamaha.

Unaweza ukaenda kusoma kuhusu "automatic and effortful encoding"inayoeleza

Niende kusoma wapi? Itabidi utueleze kinaga ubaga leo hizo tafiti za "automatic and effortful encoding" zimesema wapi kwamba mwanamke kiasili ni dhaifu. Lete chanzo, nukuu rejesho tuisome.

nature ya 'limbic size' ... ....kuidhibiti 'amygadala'... "automatic and effortful encoding" zimesema ... "emotions".Kwa mfano
Unachomeka vijineno vya kibaiolojia kana kwamba una sayansi fulani nyuma yako kumbe unazuga tu. Tupe rejesho hapa kuonyesha hujaongopa ulipodai wazi wazi kuwa Mtema na Wanawake kiujumla ni dhaifu maana bongo zao ("amygadala...nature ya limbic size") ni ndogo.

Tangu wiki iliyopita mwishoni na hata leo nimeendelea kusikia ati "Waziri" fulani kafanya jambo hili au lile. Hivi Mwanasheria Mkuu hawezi hata kutoa maelekezo kuwa sasa hivi nchi haina mawaziri au waziri mkuu? Baada ya Bunge kuvunjwa rasmi kwa kuanza kampeni ya uchaguzi Augusti 20 wabunge wote walipoteza ubunge wao na hivyo waliokuwa mawaziri nao wamepoteza uwaziri wao. Haijalishi kama baadhi yao wamepita bila "kupingwa" lakini siyo wabunge hadi siku watakapoapishwa.

Hivyo, aidha Rais Kikwete awateua baadhi yao na kuwaapisha kuwa mawaziri sasa kwa mujibu wa katiba (japo sioni haja ya kufanya hivyo) ama wale wote wanajiona ni bado "mawaziri" wapigwe makonzi na kuambiwa waondokane na fikra hizo kwani wao siyo mawaziri na uhondo wote na madaraka yao ya uwaziri hayapo sasa na wizara zao ziko chini ya Makatibu Wakuu.

So.. sitaki kusikia chombo cha habari kinatuambia ati "Waziri wa Ulinzi na JKT Dr. Hussen Mwinyi" amefanya hili au lile au "Waziri wa Nishati Bw. William Ngeleja amefungua". Hawa watu SIYO MAWAZIRI!!!!!!!!!!!!!!!

Mwanasheria alishaitolewa ufafanuzi mzuri tu kulingana na katiba ya nchi na michuziblog aliiweka mwanzoni mwa mwezi huu au mwishoni mwa mwezi uliopita. Bahati mbaya speed ya internet hapa kwangu iko doro, ikikaa sawa sawa nitatafuta na kuiweka hapa.
 
Asante sana Malafyale,nimekupata.
Kuhusu Mwanakijiji naomba nieleweke sikumaanisha ambavyo imeeleweka na wengi humu.Namheshimu Mwanakijiji kuliko mtu mwingine yeyote ndani ya JF,natambua mchango wake katika taifa hili hata kwangu pia as an individual,namuomba radhi kama nayeye atakuwa amenielewa vibaya.Hata Ilani yangu ya Jimboni imekuwa polished na yeye.

Mwanakijiji kama na wewe umenielewa vibaya na kukwazika kwa hili ninaomba unisamehe sana.

Naanza kuona machungu ya kutumia jina halisi wakati huo ukiwa na maadui ambao siwafahamu wala sijui niliwatengenezaje.Nachelea kutolitumia tena jina hili na hii itakuwa ni post yangu ya mwisho kwani kama mwanadamu mwenye moyo,mwili na nafsi nakwazika ninaposhambuliwa bila sababu za msingi na hasa watu wenyewe siwajui ni kina nani.
Kila pande inamwona mwenzake ana makosa hivyo sio rahisi kufikia muafaka.Niko kwenye kipindi kinachohitaji uvumilivu wa hali ya juu lakini kama mwanadamu nashindwa.

Kwaheri friends.
Kwa heri Kiranga na timu yako Tindikali na Gaijin napenda kuwaambia kuwa Jimbo ninashinda na mjengoni nitakwenda,hii ni ndoto yangu na lazima itimie.

Malafyale nitakutafuta.

Aluta Continua

Regia Mtema
Mgombea Ubunge-Kilombero(CHADEMA)

Umesema vema kote huko dada yangu Regia, ila hapo tu kwenye Bold ndipo unapowapa kina "kiranga and co" nafasi ya "kukushambulia" the way unavyoona.

yaani mfano hapo kwenye red, ingekuwa mimi hayo maneno nisingeyaandika kabisa....

(halafu unahitaji kupumzika jamani usiku huu na kesho kampeni ama bado hujaanza? I wish you all the best Regia)
 
Sasa kama "technically speaking hajastaafu" ujaji, this reinforces and reintroduces my original objection.

Kama Jaji technically bado hajastaafu, na jaji ni mtu wa Judiciary, anafanya nini katika kazi ya u A.G ? Ikija showdown kati ya judiciary na executive technically speaking hapa si kutakuwa na a technical conflict of interest ?

Ni hapo itakapotokea then itapatikana "test case"
 
"Kama nimekukosea..." Kama hujui kama umekosea huhitaji kuomba msamaha.

Niende kusoma wapi? Itabidi utueleze kinaga ubaga leo hizo tafiti za "automatic and effortful encoding" zimesema wapi kwamba mwanamke kiasili ni dhaifu. Lete chanzo, nukuu rejesho tuisome.

Unachomeka vijineno vya kibaiolojia kana kwamba una sayansi fulani nyuma yako kumbe unazuga tu. Tupe rejesho hapa kuonyesha hujaongopa ulipodai wazi wazi kuwa Mtema na Wanawake kiujumla ni dhaifu maana bongo zao ("amygadala...nature ya limbic size") ni ndogo.

Mazee kaongopa, kabanwa, hana cha kusema kujitetea hapa.
 
Ni hapo itakapotokea then itapatikana "test case"

Haya ndiyo matatizo yetu, mtu anakwambia hii hapa ni live wire, haitakiwi kuwa open, inatakiwa kufunikwa, ni fire hazard, inaweza kulipuka au kumnasa mtu saa yoyote.

Watu wanakwambia "Ni hapo itakapotokea then itapatikana "test case" ".
 
Hapo kwenye bold ni ideal situation na haihitaji kuvaa miwani kuona! Ni vingapi tunaviona na kujua suluhisho na hata kutoa mapendekezo ya nini cha kufanya na hakifanyiki? Unadhani watu hawayaoni au hawajui solutions?
 
Ile comment ya "hapo itakapotokea tutapata test case" inakuja across kama vile "whatever will be will be, no need to address preventative measures even as a mere position".

Ni kama mtu anasema "ukiwa na sexual contacts bila protection kuna uwezekano mkubwa ukaikanyaga miwaya, kwa hiyo ni muhimu kuacha hizi contacts au at least kuwa na protection"

Halafu jibu unalopewa ni "hapo itakapotokea tutapata test case".

Totally irresponsible. Unasubiri tatizo litokee uone wakati mtu anakwambia jinsi ya kuondokana na possibility ya kupata tatizo kabisa.

Not proactive at all. Hata kwenye attitude tu !
 
Mtazamaji thank you for the comment.Mimi wala sikati sikatishwi tamaa na huyu jamaa.nafahamu kwamba namzidi kiuwezo kwa mbali sana,yeye kazi yake ni kubishana na watu tu kila siku na hasa watu tuliomzidi akili.Nimekuwa nikijuliza kwanini ananifuata kiasi hiki lakini sijapata bado jibu.Kutofahamu kipengele kimoja cha katiba haimaniishi kuwa huijui katiba.Maendeleo hayaletwi na kuijua Katiba yote,ingekuwa hivyo basi kina Mwanakijiji wangebadilisha hii nchi,kila siku wanasoma na kuandika lakini bado tuko pale pale.Maendeleo yanaletwa kwa vitendo sio kukaaa kwenye kompyuta masaa 24 na kubishana na watu.Ninafuraha kwamba mimi ni sehemu ya mabadiliko katika nyanja zote,ya kuandika na kufanya kwa vitendo.Wengine watabaki kuwa waongeaji tu.

Haya dada
Hope pia unawatu wa kupreview na kuproof read hotuba au point zako utakazoongea za kwenye kampeni. Watakusadia maana unaweza kuwa na ujumbe mzuri lakini utakavyouwakilisha ukaeleweka tofauti. Maana naona kwa Thread hii tu kuna tatizo la commucation. what, who , How and when to and not to communicate ni mambo ya msingi kujiuliza.

Otherwise Good luck
 
Naanza kuona machungu ya kutumia jina halisi wakati huo ukiwa na maadui ambao siwafahamu wala sijui niliwatengenezaje.Nachelea kutolitumia tena jina hili na hii itakuwa ni post yangu ya mwisho kwani kama mwanadamu mwenye moyo,mwili na nafsi nakwazika ninaposhambuliwa bila sababu za msingi na hasa watu wenyewe siwajui ni kina nani...

Mwanakijiji kama na wewe umenielewa vibaya na kukwazika kwa hili ninaomba unisamehe sana....Hata Ilani yangu ya Jimboni imekuwa polished na yeye.

Niko kwenye kipindi kinachohitaji uvumilivu wa hali ya juu lakini kama mwanadamu nashindwa.

Kwaheri friends.
Kwa heri Kiranga na timu yako Tindikali na Gaijin

Duu, unarusha taulo!

Umeambiwa unachemka Regia, umekewa jina la ukweli halafu hauko makini unachoongea, nadhani hata ndugu zako wanaobeba jina la Mtema wanaona unachoreka mitandaoni tu, mara unatafuta wanaume ambao hawakutaki, mara unawawakia CHADEMA wenzio kina Mnyika, mara unammaliza Mwanakijiji anaekuandikia maneno ya kusema Kilombero, mara inabidi uombe misamaha.

Sasa unadai unamheshimu Mwanakijiji kuliko mtu yeyote, ina maana unawatenga ambao wamekuchangia hali na mali au wanafikiria kufanya hivyo, wanaona kumbe unamthamini mmoja tu, ungesema "Mwanakijiji ni moja kati ya watu ninaowaheshimu kupita wote," ndio umakini wa kuongea. Wenzio wa kina Mnyika wanakashifiwa kulia na kushoto humu sijui kafeli kidato cha sita, sijui Regia Mtema kamwambia sijui nini, ushaona anajibu mashambulizi? Heshima mwanzo mwisho, yuko kwenye umma kwa ubini wake wa kweli, wengine majinamizi tu humu, we unataka kushindana nao? Na watetezi wako nao uzalendo unawashinda.

Heri umejitoa. Lakini wewe sidhani kama hutarudi kuchemka tena na jina hilo.

Ile comment ya "hapo itakapotokea tutapata test case" inakuja across kama vile "whatever will be will be, no need to address preventative measures even as a mere position".

Ni kama mtu anasema "ukiwa na sexual contacts bila protection kuna uwezekano mkubwa ukaikanyaga miwaya, kwa hiyo ni muhimu kuacha hizi contacts au at least kuwa na protection"

Halafu jibu unalopewa ni "hapo itakapotokea tutapata test case".

Totally irresponsible. Unasubiri tatizo litokee uone wakati mtu anakwambia jinsi ya kuondokana na possibility ya kupata tatizo kabisa.

Not proactive at all. Hata kwenye attitude tu !

Ningetamani sana Kuona pro-activeness ikionyeshwa kwa mifano zaidi badala ya maneno yenye kurushia lawama wengine wakati wote!
 
Haya dada
Hope pia unawatu wa kupreview na kuproof read hotuba au point zako utakazoongea za kwenye kampeni. Watakusadia maana unaweza kuwa na ujumbe mzuri lakini utakavyouwakilisha ukaeleweka tofauti. Maana naona kwa Thread hii tu kuna tatizo la commucation. what, who , How and when to and not to communicate ni mambo ya msingi kujiuliza.

Otherwise Good luck

Mimi nilishayaona haya matatizo ya communication, pamoja na mengine mengi ya attitude na exposure, kitambo tu hapa.

Watu wakaniona nataka kumzibia, sasa naona baadhi ya watu wanaelewa ninachosema.
 
Back
Top Bottom