Mlipuko wa masalia ya mabomu Mbagal: Je, Dr. Mwinyi ajiuzulu?

Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,947
4,445
Mabaki ya mabomu 2 yalipuka na kuua watoto wawili walio kuwa wakicheza kwenye migomba na kuwaacha 4 wakiwa wamejeruhiwa vibaya.

More news stay tuned.

Watoto hawa wamenusurika kupata mauti wakiwa na mama

Last edited by a moderator:
Mabaki ya mabomu 2 yalipuka na kuua watoto wawili walio kuwa wakicheza kwenye migomba na kuwaacha 4 wakiwa wamejeruhiwa vibaya.
More news stay tuned.

That is bad jamani.

Hivi ile report mbona haijatolewa wazi?
 
Ndo hivyo watoto wawili wamesha poteza maisha na wengine wanne taabani.
Si walisema wataleta vifaa vya kusasa kuja kufukua na kusaka vipande vilivyo salia?
Ok nimegundua kwa vile kule wanaishi walalahoi haya mabomu yangelipuka kwa matajiri Mbezi beach huko najua serikali ingeleta wamerekani kuja kusaka vipande.
 
Serikali yetu hushughulikia jambo pale linapokuwa linagusa maslahi yao, kwa hao watoto kufa kwao wala si tatizo kwa sababu haiwagusi sana, lakini angekufa mtoto wa mmoja wa viongozi ungeona shughuli pevu pale Mbagala, Mungu azilaze pema peponi roho za wanyonge.

DUNIA YETU INA SHERIA TU, HAKI IPO MBELE YA MUNGU!

JWTZ Oyeeeee!
 
Jamani hivi hii serikali yetu inatupeleka wapi? We Mrisho una tupeleka wapi watanzania wako? Yao wapi maisha bora kw akila mtanzania? mbona tunashuhudia vifo vya kizembe namna hii nawe umekaa kimya tu? Au kwa vile Ikulu haiko Mbagala? Kumbuka wananchi hao hao wa Mbagala ndio walokupa wewe kura za kukuwezesha kula.

Uliruhusuje wananchi wa Mbagala kuruhusiwa kurudi majumbani mwao (Mbagala) tena na fidia zikatolewa wakati wewe na serikali yako hamkuwa na uhakika kuwa mahali pale ni salama? Hebu jeshi liwajibike katika vifo hivi ni aje wawe hawakumaliza mabomu yote? Hivi ni lini tutafikia mahali pa kuwawajibisha wewe na serikali yako kwa uzembe huu wa serikali yako?

Nasikitika sana kuwa hamu na uaminifu wangu kwako na serikali yako imefikia tamati sina uhakika kama mwakani nitakupa kura yangu tena.

Aksante.
Poleni wafiwa na majeruhi MUNGU awape nafuu
 
dah wakazi wa huko wameona hiyo sehemu kuwa ni hatari kuishi ni sawa unitoe bongo unipeleke afghanistan, jamani kimbie hukooooooooo
 
Natamani watanzania wangelink haya matukio na 2010 elections. If the current regime can not protect its citizens, lets give a try to an alternative party!!

Damn the current regime!!!
 
ina sikitisha sana ila hakuna jinsi, nchi yetu haina utaratibu wa watu kuwajibika kwa vitu kama hivyo, poleni sana wafiwa na mungu awasaidie majeruhi wapate nafuu haraka
 
According to Michuzi blog, bomu limelipuka mbagala kizuiani karibu na kambi ya jeshi na kuua watoto wawili na wengine kujeruhiwa. ni mabaki ya yale ya zamani. Sasa hawa watu wa mbagala wataishi kwa hofu hivi hadi lini, halafu wanasema ni bahati mbaya. Tutafika hivi kweli na watoto wenyewe very innocent 6 years.
 
Masikini,Muumba awalaze mahala pema peponi,amini.Tatizo lenu nyie mnatatka kuleta siasa katika kila jambo.Sasa sijui watasema nini tena.
 
Mungu awarehemu watoto hao.
Wakazi wa e na serikali wanapaswa kukubaliana kuwa eneo si salama na halifai kwa makazi ya binadamu kwa wakati huu na ifanyike mipang madhubuti ya kuwahamisha watu kutoka hapo, la sivyo tutashuhudia maafa mengine
 
Habari zilizopatikana hivi punde inaeleza watoto wawili wamekufa kwa mabomu huko mbagala karibu na kambi ya jeshi wilaya ya Temeke
Watoto waliokufa ni Reginald Shawala (6) Rajabu Said (6) Aidha katika mlipuko huo pia kulikuwa na majeruhi ambao ni mtoto Said Seleman (2) ,Asha Seleman (5) pamoja na Stela christia Chawala ambaye amejeruhiwa vibaya na kukimbizwa hospitaly ya muhimbili kitengo cha wagonjwa mahututi,
Chanzo cha mlipuko huo umesababishwa na baadhi ya mabomu yaliyokuwa yamebaki ,hivyo familia hiyo ilipokuwa inafanya usafi katika nyumba yao na kuchoma taka baadhi ya takataka ukapelekea mabaki hayo kulipuka
Mkuu wa mkoa wa Dar Lukuvi pamoja na kamanda wa polisi kanda maalum ya dar Suleiman kova wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo
 
Jamani! nimesikia wanatangaza sasa hivi redioni! lakini nchi hii kwanini hatujifunzi na kutatua haya matatizo? hivi kweli tutaendelea kuumia mpaka lini? Mbagala, North Mara, Barabarani?

Kuunda tume kila mara mpaka lini?
 
Kuna dalili zote Mbagala hakufai kuishi watu kwa sasa. Maana kama moto unaweza kuleta milipuko, ni dhahiri maisha yatawawia vigumu wakazi wa Mbagala. Nadhani ni wakati wa kuwapatia maeneo mengine salama na kuwashauri ili wahame
RIP
 
Jamani hivi hii serikali yetu inatupeleka wapi? We Mrisho una tupeleka wapi watanzania wako? Yao wapi maisha bora kw akila mtanzania? mbona tunashuhudia vifo vya kizembe namna hii nawe umekaa kimya tu? Au kwa vile Ikulu haiko Mbagala? Kumbuka wananchi hao hao wa Mbagala ndio walokupa wewe kura za kukuwezesha kula.

Uliruhusuje wananchi wa Mbagala kuruhusiwa kurudi majumbani mwao (Mbagala) tena na fidia zikatolewa wakati wewe na serikali yako hamkuwa na uhakika kuwa mahali pale ni salama? Hebu jeshi liwajibike katika vifo hivi ni aje wawe hawakumaliza mabomu yote? Hivi ni lini tutafikia mahali pa kuwawajibisha wewe na serikali yako kwa uzembe huu wa serikali yako?

Nasikitika sana kuwa hamu na uaminifu wangu kwako na serikali yako imefikia tamati sina uhakika kama mwakani nitakupa kura yangu tena.

Aksante.
Poleni wafiwa na majeruhi MUNGU awape nafuu

Hivi wa kulaumiwa hapo ni Serikali au JWTZ?......... Oooh! Sorry, nlishasahau kuwa JK ndio Amiri Jeshi mkuu! Bania kura yako mama, una haki hiyo.
 
Back
Top Bottom