Mliofiwa na wazazi (mama), mliwezaje kuvuka kipindi hiki?

Wandugu habari, mama alikuwa mgonjwa na akaanza matibabu ila akiwa hospital akafariki. Hapa naenda msibani, ila siwezi kuvumilia kulia mara kwa mara licha ya kujikaza.

Kwa mliopata hii changamoto, mliwezaje kumove on? Nikifikiria ameenda bado mdogo hata 50 hajafika, ni mengi nawaza yananiumiza ila sometimes inabidi nifanye ujinga tuu ili kupoteza mawazo.
Usifanye ujinga ndugu,ila pole sana kwa msiba mkuu
 
Ni ngumu sana hii hali. Ni mwaka sasa umepita tangu mama yangu mpenzi alipoitwa mbele za haki. Ni kama imetokea jana tu. Nikienda nyumbani simkuti sebuleni najua labda yuko uani napitiliza nako hayupo. Ukiwa mkubwa mama ametuachia hasa baba ambaye ni mtu mzima. Ila Kazi ya Mungu haina makosa maana ni kwake tulitoka na kwake ni lazima tutarejea. Pole sana mtoa mada. Mungu akutie nguvu
Pole sana mkuu
 
  • Thanks
Reactions: Ok9
Wandugu habari, mama alikuwa mgonjwa na akaanza matibabu ila akiwa hospital akafariki. Hapa naenda msibani, ila siwezi kuvumilia kulia mara kwa mara licha ya kujikaza.

Kwa mliopata hii changamoto, mliwezaje kumove on? Nikifikiria ameenda bado mdogo hata 50 hajafika, ni mengi nawaza yananiumiza ila sometimes inabidi nifanye ujinga tuu ili kupoteza mawazo.
Nilimpoteza mama nikiwa na umri wa miaka 22, wakati anafariki alikuwa na miaka 41,Mimi ni mtoto wa kwanza kuzaliwa, na yeye ndiye alikuwa nguzo yangu ;kwa hakika nilipitia magumu mengi sana Ila Mungu kanivusha salama;Muombe Mungu na atakuvusha salama
 
Nimebakia na mama tu mzee alishafariki, kuna muda nakwazana nae lkn nikiwaza upendo wake juu yangu , presence yake ni kila kitu maishani mwangu huwa namshukuru Muumba kwa zawadi hii. Nipo hivi nilivyo leo kwa sababu yake, nazidi kumuombea maisha marefu na yenye baraka tele. Poleni sana mlioondokewa na mzazi mmoja ama wote. Wazazi ni lulu maishani tuwaombee.
 
Maumivu yake utakapokumbuka wakati wowote yanakuwa mabichi kabisa. Mimi baba alifariki mwaka 1995 wakati huo sijaingia hata shule. Yale mazingira kuanzia anaumwa, tulivyokuwa tunaongea binafsi mimi na yeye au tukiwa wote yaani naona kama ni mwaka jana tu.
Pia nakumbuka jinsi nilivyosikia taarifa ya msiba (maana nilikuwa nacheza na wenzangu pembeni kidogo na sikujua kama ile homa ingemwondoa)
Kwa ujinga wa wakati ule wa utoto nikawa namwuliza mama kuwa baba atarudi lini.

Hakika inaumaga sana, kuna siku likikutokea jambo baya utahisi labda angekuwepo mzazi lisingetokea.
 
Nimebakia na mama tu mzee alishafariki, kuna muda nakwazana nae lkn nikiwaza upendo wake juu yangu , presence yake ni kila kitu maishani mwangu huwa namshukuru Muumba kwa zawadi hii. Nipo hivi nilivyo leo kwa sababu yake, nazidi kumuombea maisha marefu na yenye baraka tele. Poleni sana mlioondokewa na mzazi mmoja ama wote. Wazazi ni lulu maishani tuwaombee.
Pole sana dear,ishi kwa upendo na mama mkwe.Usivutane naye.
 
  • Thanks
Reactions: Ok9
Yule mzee ananiuma mpka kesho Rip mzee wangu sjawah kuizoea hyo hal et unaenda nyumban unakuta kaburi lina zege ndan kuna mtu aliekua akikupokea mnacheka anakupa na hela japo unakaz hata kama n elfu kumi mzaz ananafas yake special kwenye mioyo yetu pumzka kwa aman Baba
 
Mama angu mlezi alifariki May 10 2019, toka kipindi hicho hua namuota sana. Mara nyingi nilikua namuota tupo kwenye nyumba niliyokulia namuona anapika. Mwezi uliopita nilimuota kafariki wakamleta kanisani akiwa kavishwa sanda. Niliokopa sana.

She was muislim, nimeulizia kwa wenye uelewa wa dini hii wananishauri nikamfamyie kisomo hiyo hali inaweza kuisha. Naplan kufanya hivyo siku moja, Hopefully Mungu ataniwezesha

Kuna muda hali ilikua mbaya hadi nikaleta uzi
 
Poleni sana ndugu kwa Msiba. Simama na Mungu kwa Imani yako.
 
  • Thanks
Reactions: Ok9
Back
Top Bottom