Mkuu wa wilaya Hai-Novatus Makunga kafanya alichoshindwa M/kit wa CCM Hai

Inapendeza kuona mkuu wa wilaya ''has guts'' kupita huku bila kujificha na kufafanua mambo.

Kusema kweli Mkuu wa Wilaya Ndugu nova makunga ni wa kuigwa kwa jinsi alivyotoa ufafanuzi. Iwe ufafanuzi umekubalika ama la lakini ni muhimu kutoa ulichonacho without fear or favour.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Diga Diga wewe ni yule mcheza disco wa enzi zileee au!? Hivi mtu akiteuliwa ndiye anakuwa ametoa vigezo vya yeye kuteuliwa au mteuzi ndio anakuwa vigezo? Hilo tu mkuu.
 
Last edited by a moderator:
heshima mbele mh nova

hongera sana kwa kujitokeza hapa JF na kujibu hoja, hata kama mleta hoja ametumia lugha ambayo pengine haijaeleweka kwa wengi na/au hata lugha isiyo ya kistaarabu, busara na hekima pamoja ukomavu wa uongozi huja na kuonekana unapojibu hoja husika kwa uwazi na utulivu. Usikubali uongozwe na hisia na hasira kwenye kujibu hoja zako na zaidi kwenye utendaji wako wa kazi. JF ni pa moto lakini taratibu utajenjwa hapa, utakomazwa, utafundishwa na mwisho wa siku utakuwa imara, hodari na mwenyewe elimu.
Nashukuru ndugu yangu nipo humu JF tangu inaanzishwa mwaka kwa jina lingine hivyo nafahamu vizuri.

Nikirudi katika hoja yako, tatizo la pale ni kubwa sana kiasi cha wananchi walifikia kufunga ofisi ya kijiji,kwa taratibu zilivyo nisingeweza kuwafanya wampigie kura ya kuwa na imani naye ama laa katika ule mkutano wa hadhara kwani kwa vyovyote vile angekataa rufaa angeshinda.

Nina mifano mmoja nilishuhudia nikiwa mwanahabari mwenyewe kabla ya kuja huku, huko mkoa wa manyara, mwenyekiti naelezwa amerudi madarakani na kijiji ni vurugu tupu, katika mkutano wangu wa kwasadala ambapo bahati nzuri ulihudhuriwa na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya hai na mheshimiwa diwani, niliwaomba wananchi waliohudhuria mkutano ule mwenyekiti akae pembeni kwa siku saba, nifuate taratibu na mbele yao nikamtaka mkurugenzi kutoa notisi ya mkutano mkuu maalumu wa kijiji licha ya taratibu kutokuwa wazi ni nani mwenye mamlaka ya kuitisha lakini unataka taarifa ya kuitishwa kutolewa ndani ya siku saba lakini pia kumpa mtuhumiwa tuhuma zake kimaandishi.

Kwa upande wa timu yangu ya wataalamu ambayo itaanza kazi jumatatu itanisaidia kuandika tuhuma kwa uzuri zaidi ndugu yangu, hivyo kwa ufupi ndugu yangu maamuzi yangu yamelenga zaidi katika kufuata sheria na kuhakikisha amani havurugiki pale kijijini, wananchi ndiyo watakaoamua na siyo DC wala DED wala mwenyekiti wa halmashauri kwa upande wa wananchi waliohudhuria hakuna anayeweza kulalamika mkutano ulikuwa mzuri sana na kile kijiji hakijakuwa na mikutano ya kijiji muda mrefu ambapo taratibu zinataka kila baada ya miezi mitatu.

Samahani huwa sipendi kuandika text ndefu kwani mara nyingi inawachosha wasomaji
 
  • Thanks
Reactions: Paw
Mkuu Diga Diga wewe ni yule mcheza disco wa enzi zileee au!? Hivi mtu akiteuliwa ndiye anakuwa ametoa vigezo vya yeye kuteuliwa au mteuzi ndio anakuwa vigezo? Hilo tu mkuu.
Hivi wewe unapopata kazi kupitia interview ya uwazi unakuwa hujui vigezo vilivyokufanya upate hiyo kazi? Au ni interviewers pekee ndio wanaokuwa wanajua? Au na wewe ni wale wale?! Rubbish!
 
Hongera Mkuu Nova,

umekuwa chachu ya kutupasha hapa Jf bila woga na umekubali kushambuliwa na unajibu kwa hoja.

wewe ni mfano kwa wakuu wa wilaya wengine nao wajitokeze, Utafika mbali zaidi ya hapo kwa uwazi wako.

Mimi sijui power zenu kama wakuu wa wilaya inawezekana mamlaka hayo unayo sioni shida

Usingemsimamisha wananchi wangesema unamwogopa, sasa umemsimamisha umeambiwa huna mamlaka, ndio Tanzania yetu hiyo chapa kazi bila kupendelea chama wala itikadi, big up
 
Mkuu wangu wa wilaya hongera sana kaka,pale kijiji cha shari panakaribia jangwa watu wanakata miti ovyo embu fuatilia ,pia jf ndio darasa usiogope kutujibu wala usiwe na hasira viongozi wengi wa ccm hawapendi kukosolewa!
 
Baada ya jaribio la kufa na kupona la mwenyekiti wa CCM kutaka mto amwenyekiti wa Kijiji Kwasadala hatimaye Novatus Makunga kalifanya.Mwenyekiti wa CCM ambaye anasemakana kuwa obsessed sana na hali ya raia kuipiga chini CCM alimfukuza kazi mwenyekiti wa kijiji ila mwenyekiti .Watu wakamuuliza mamlaka kapata wapi?Mwenyekiti aliyechoka akajaribu tumia msaada wa polisi ila nao wakionekana kuichoka CCM wakampa swali kama hilo.Leo Taarifa ya habari ya ITV inamwonyesha akiwamfukuza mwenyekiti huyo huku akiwa na watu walioandaliwa kuonyesha kuwa wamepangwa waongee nini.Kama inavyofahamika huyu mkuu wa wilaya kilaza aliwahi fanya kazi ITV na atakuwa mwepesi sana kuwaita kwa mambo yamhusuyo na kujijenga kisiasa.


Cha kujiuliza ni kwamba kama mwenyekiti kashindwa kazi kwanini asitolewe kwa kura za wanakijiji kama walivyomchagua?kwani yeye si wa kuteuliwa na serikali.

Taarifa iliyopo ni kwamba hata polisi wamemchoka huyu m/kiti wa CCM wilaya ya Hai.Amekuwa akiwahemea wamsaidie kuzui nguvu ya CDM bila jijua kuwa yupo katik nyumba ya CDM.Novatus nae akiwa kama watupu wengine wa CCM anatafuta sana nji ya kujijenga kwa nguvu nyingi,mojawapondio hii ya kufanya kazi ya CCM.

Mbona hueleweki, ww ni Dhaifu, jipange upya unapoandika hbr. kalale ukiamka andika tena.
 
Hapa nadhani kikubwa ni kumpa ndugu yeu makunga nafasi afanye kazi,sidhani kama amekurupuka,namfahamu sana huyu bwana yuko makini,kingine jamani mnatakiwa kuelewa kwamba DC ni rais wa wilaya
 
ndugu zangu nashukuru wote wakiwemo waliochangia kwa hoja na pia waliokejeli,natoka sitarudi katika uzi huu tena,nilichojifunza wengi wetu humo wanatufahamu kwa muda mfupi tu,mtu anakujaji kwa kuwa alikusikia katika kampeni za uchaguzi mdogo wa arumeru mashariki basi lakini hajui kuwa ulikuwa mwajiriwa uliyetumwa kufanya kazi katika eneo fulani mjadala ni mpana hasa kwa sekta ya habari nitauleta baadaye.

Kwa bahati mbaya mtoa uzi huu hakurudi tena naamini hakuwepo katika mkutano ule wa kwasadala na wala siyo mkazi wa kwasadala kwani baadaye alisema yeye anatoka rongoi,leo nimeshinda pale kijijini.

kila la heri wana jf
 
i
Hivi wewe unapopata kazi kupitia interview ya uwazi unakuwa hujui vigezo vilivyokufanya upate hiyo kazi? Au ni interviewers pekee ndio wanaokuwa wanajua? Au na wewe ni wale wale?! Rubbish!

Mkuu kumbe ukuu wa Wilaya unapatikana kwa interview ya wazi? Unaijua katiba mkuu? Kumbe hata hujui ukuu wa wilaya unapatikanaje! Naona wewe unajua rabbish tu. Jishughulishe basi hata kidogo ili ujue ukuu huo unapatikanaje kisha uende kwenye tume ya katiba ili utusaidie kutoa mawazo ili tuje kupata wakuu wa wilaya kwa vigezo na interview za wazi!
 
Mkuu wangu wa wilaya hongera sana kaka,pale kijiji cha shari panakaribia jangwa watu wanakata miti ovyo embu fuatilia ,pia jf ndio darasa usiogope kutujibu wala usiwe na hasira viongozi wengi wa ccm hawapendi kukosolewa!

marie naomba tuwasiliane maana masuala ya mazingira ni vita kwetu hai tusaidiane kupambana
 
Mbona hueleweki, ww ni Dhaifu, jipange upya unapoandika hbr. kalale ukiamka andika tena.
-Kwani wewe ni mahakama sasa?kama kala pembejeo si angafunguliwa kesi?

-Au ndio umefuta sera za ccm kuhamisha mhalifu badala ya kuburuzwa mahakamani?

-Ulimchagua wewe?kwani usiwasaidie kuitisha kura?

-kuna ubishi ulikuwepo kuhusu mtoa kauli upande wa pili ishara yake nini?

-umetumia kifungu number ngapi cha sheria?na sheria ipi?tekeleza ilani ya ccm kanjanja wewe.kwani nani hakujui enzi zile ulikuwa ukivizia offer za ccm katik mikutano na kampeni ndio wakakupa hizo nafasi za kike?
 
Hi ndio nyumbani paa m4c ngoja tuone wageni wakigomban mda simrefu
tutawafukuza wote.mi niteremka kimashuku kwanza nikirudi lazima kieleweke
 
Hapa nadhani kikubwa ni kumpa ndugu yeu makunga nafasi afanye kazi,sidhani kama amekurupuka,namfahamu sana huyu bwana yuko makini,kingine jamani mnatakiwa kuelewa kwamba DC ni rais wa wilaya
kama ni rais wa wilaya kwanini alingeitwa kumchagua?ugumu wangu kuandika haimanish nova alitumia akili kujibana katika sheria.utashi wa ccm ulimzidi kwani hii ndio kazi waliyoamriwa kama wale wa mwangoka walivyofanya.

ushenzi ulikuwepo na unaendelea kuwepo lakini kwa nini hakuenda kwanza mpaka mwenyekiti wa ccm alivyobounce?

kiongozi makini haongozwi na na kelele hata za mke wake mwenyewe.kwani alishindwa saidia wanakijiji kulianzisha na kupitisha kura ya maoni wafanye nini kama hatua ya mwanzo ya uchunguzi,halafu baada ya hapo watu wajadiliane na wapige kura kura shauri lipelekwe vipi mahakamani.

CCM wametunza uovu sana kwa miaka mingi kuna wasomali kama marais pele hawaguswi ila sasa kwa vile wanataka jenga himaya ndio wanafanya haya.

Hongera kwa kuja ila hata mkuu wako wa mkoa na rais wake watakauja tuu hapa kujibu hoja.Kama ilivyo kwa wanakijiji wasiojua lugha ya taifa ila maswali yao mnyaogopa ndivyo nahpa utawajibika.hao watoa wa matusi kwa kwa niaba yako hawakujibii ulichofanya na malengo yaliyojificha.wewe tangu uingie leo ndio umeona huo uovu?huo uovu upo miaka mingi ila alipokutuma mwenyekiti ndio ukaona ukasafishe chama na kuweka mizizi ya ccm.
 
ndugu zangu nashukuru wote wakiwemo waliochangia kwa hoja na pia waliokejeli,natoka sitarudi katika uzi huu tena,nilichojifunza wengi wetu humo wanatufahamu kwa muda mfupi tu,mtu anakujaji kwa kuwa alikusikia katika kampeni za uchaguzi mdogo wa arumeru mashariki basi lakini hajui kuwa ulikuwa mwajiriwa uliyetumwa kufanya kazi katika eneo fulani mjadala ni mpana hasa kwa sekta ya habari nitauleta baadaye,kwa bahati mbaya mtoa uzi huu hakurudi tena naamini hakuwepo katika mkutano ule wa kwasadala na wala siyo mkazi wa kwasadala kwani baadaye alisema yeye anatoka rongoi,leo nimeshinda pale kijijini.kila la heri wana jf

pamoja sana NOVA.It show that una ujasiri licha ya kuwa 2na ideology tofauti.NIMECHELEWA MJADALA ulioufunga ila umeonesha njia kwa Ma_DC wengine..Nimependa ulivyopambana ila tambua wengi humu hawana tatizo nawe ila UWEPO WA VYEO VYA U_DC so mnakuwa majeruhi kutokana na position yenyewe.TUTAONANA Mitaa ya hom kwako pale MANDELA ROAD
 
pamoja sana NOVA.It show that una ujasiri licha ya kuwa 2na ideology tofauti.NIMECHELEWA MJADALA ulioufunga ila umeonesha njia kwa Ma_DC wengine..Nimependa ulivyopambana ila tambua wengi humu hawana tatizo nawe ila UWEPO WA VYEO VYA U_DC so mnakuwa majeruhi kutokana na position yenyewe.TUTAONANA Mitaa ya hom kwako pale MANDELA ROAD
sijui unatafuta nini huko mbali hivyo.kwani yeye kuonyesha mfano sifa yake si kama salamu za utambulisho tuu, halafu unakwenda kwenye hoja.Wewe umeshatambua kuwa kajitahidi kufungua mlango,ila haimzuii yeye kujiuliza mswali ya msingi.hawezi fanya maamuzi ya kienyeji hivyo?yule jamaa na wengine hawajateuliwa tuu kama yeye.yeye ange assist tuu.

mbona unajipa vikwazo kwa jitihada tofauti?unaweza pigania nchi yako vitani na kuikomboa ila ukibaka unahukumiwa.nova ajibu maswali watu wampe msaada jinsi ya kuwakama majizi.pia ajue kichefuchefu kingine kwa raia ni wakuu wa wilaya kuwa silaha ya pili ya ccm pale wenyeviti na makatibu wa wilaya wanapokosa meno kwa polisi.Nova ndio kaamua piga ngoja niende.
 
Nova Makunga

Ushauri wangu kwako, Usijekuonekana umeshiriki kwenye zoezi la kumuondoa mwenyekiti alyechaguliwa na watu katika nafasi yake. Sioni mantiki ya wewe kuwaundia tume (kamati) wanakijiji ya kuchunguza tuhuma za mwenyekiti. Ulichotakiwa kufanya ni kuwapa fursa wananchi kuongea kwa uwazi kwenye mkutano huo ikiwa ni pamoja na kuruhusu wao wenyewe kuamua juu ya hatma ya mwenyekiti waliyemchagua. Kumbuka msingi mkuu wa Demokrasia ni maamuzi ya wengi.

Kupitia mkutano huo (au huo ambao umemuomba Mkurugenzi atoe notisi uitishwe ndani ya siku 7) ungetoa fursa kwa Wanakiji kutiririka juu ya tuhuma zinazomkabili mwenyekiti wao na baada ya hapo wape fursa ya kutoa mapendekezo juu ya nini wanataka kifanyike katika kuupata uongozi mzuri na wenye kuwajibika. Wewe kuwa Facilitator tu wa process ya wananchi hao kumwajibisha au hata kumpata kiongozi mpya.

Wewe binafsi kuwapa kazi watu wako kumchunguza na hata kuandaa ripoti ya tuhuma za Mwenyekiti huyo kunaweza kukuletea matatizo zaidi. Wanaweza kuja na ripoti isiyowapendeza wanakijiji na wewe ukaonekana umeshiriki kubaka matakwa ya wengi.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom